Hongera kwa mara ingine Richard.
Wana JF, wakati mwingine tunakuwa wanafiki kupita kiasi, na wengi wameonyesha unafiki wao kwa kusema huyu dogo ni mzinzi ila jiulize yafuatayo.
Umefanya ngono na watu wangapi maishani mwako ukiwa ndani ya ndoa au kabla ya ndoa.
Richie walau kaongeza pato la taifa kwa 139,000,000 kwa mwaka huu wa fedha bila kujali ameipataje. Wewe umeliongeza kiasi gani hata kwa kuuza bangi, madawa ya kulevya au haata kwa fedha halali?
Richie tangu aliiingia kweny lile jumba amekuwa akisifia Serengeti, Ngorongoro, na kusifia tanzania kwa ujumla na hata kupepea bendera ya Tanzania ndani na nje ya jumba hilo na tayari baadhi ya washiriki wameahidi kwenda Tz kutembelea mbuga hizo, Je wewe mwana JF umefanya lipi?
Kuna msemo unaosema fanya kazi kama mtumwa mwishoni uishi kama mfalme, na mwingine mtumikie kafiri upatee.... Huoni ndicho alichokifanya mwenzetu?
Watz wangapi wanishi ulaya na US illegally lakini wanatafuta maisha na bado tunawapongeza pale wanaposaidia maendeleoya nyumbani kwao, wangapi wanauza madawa bongo, wanafanya umalaya, Ufisadi, ujambazi, wanakwepa kulipa kodi kisha wanajenga majumba ya kifahari tunawasifia kuwa wajanja. Inapofika kwa Richie eti ni kichefuchefu?
Kwa mtazamono wangu Richie kufanya ngono ni kuonesha kwamba yeye alikua kijana rijali mwenye feelings na alikua na mmoja tu ndani ya ile nyumba kuonesha kwamba bado alikua mwaminifu katika ''Dunia'' ile aliyopelekwa maana walitenganisha na outside world.
Bigup Richie. Hoja hujibiwa kwa hoja.
Nawakilisha