Wapendwa wa safu hii mbona kimya sana? Au BBA ya mwaka huu haina msisimko? Au game bado halijaanza?
Sijajua Biggie mwaka huu ana plan gani? Maana mpaka sasa naona bado anacheza makida makida. Sammi na Hannington naona wote 2 watarudi Jumbani siku ya Jumapili. Ambacho sijaelewa bado ni kwamba je, eviction ya Jumapili itakuwa ya kikweli au ni ya kiungo uongo?
Mabadiliko? YES
Naona Yacob na Paloma wamejitahidi sana kubadilika. Yacob siyo mzee wa strategy tena this season na Paloma amekuwa mpole utadhani siye yule aliyekuwa akiwakoromea wasichana last season. Sheila amepunguza uvivu kwa kiasi kikubwa. Uti sijaona tena kama bado ana zile hasira zake za season 3. Munya sijui ana over confidence? Maana this time naona ameanza kuchemka mapema sana. Hannington pia naona amebadilika sana, si yule wa season 4. Mwisho na Meryl sijaona kama wamebadilika, japo mahusiano yao yanaweza kumuweka Mwisho mahali pabaya ama pazuri.
Alliances? YES
Naona tayari kuna informal alliance moja ambayo inazidi kuwa wazi kwa kadri siku zinavyozidi kusonga mbele. Meryl, Lerato, Sheila, na Uti; hawa naona wako kambi moja na ninaona Mwisho na Yacob wanaelekea huko maana Yacob naona ana dalili za kumtaka Lerato japo hasemi na Mwisho tayari ni buddy buddy wa Meryl.
Vulnerable persons: Tatiana na Munya naona wameanza na mguu mbaya na wanaweza kuondoka mapema sana. Lerato anahisi Tatiana bado ana mission ya season 2, na Tatiana nae ana hisia hizo hizo, maana walikuwa kwenye kambi 2 tofauti na Lerato na kambi yake walipoteza game baada ya kusalitiana wao kwa wao.
The rest of housemates hata sijui nisemeje, lakini naona K1, Munya, na Yacob wako against Uti and along that line wameungana informally na Paloma kwenye ka-alliance kao.
Jen hajulikani anaelemea wapi.
Hannington na Sammi wakirudi ndani ya Jumba game plan inaweza kubadilika sana.
Generally, season hii kuna badiliko kubwa moja, when it comes to nominations hakuna open discussions kama ilivyokuwa last season. Kilichosababisha nadhani ni kwamba whoever aliyekuwa anaongoza mikakati ya nominations alikuwa anachukiwa na Afrika na siri ikivuja the other group wanam-target.
Sasa sijui alliance za mwaka zita-operate kwa misingi ipi. Ngoja evictions za kikweli zianze may be watu wataanza kucheza game kikweli kweli.
Mwisho: I guess anaweza kufika mbali sana kwa kuwa sioni kama yuko kwenye alliance yeyote na pia haonyeshi anaelemea wapi. Hiyo inaweza kum-save na sidhani kama Meryl na alliance yake wanaweza kum-target Mwisho.