=============
Housemates evicted so far:
- Hannington
- Sammi
- Lerato
- Tatiana
- Yakob
- Sheila
- Code
- Paloma
- Jen
- Meryl
Jumapili ya 18/7/2010 ile show maarufu ya Big Brother Africa itazinduliwa rasmi. Maandalizi yamekamilika na washiriki tayari wanajifahamu.
Washiriki watakuwa ni wawakilishi wa nchi shiriki ambazo ni 13 na Rest of Africa ambayo haina mwakilishi lakini ina haki ya kupiga kura. Tutawaona baadhi ya nyota walio shiriki kwenye seasons nne zilizotangulia kuanzia BBA I mpaka BBA IV.
Nina hisia tofauti kidogo kuhusu show ya mwaka huu. Kuna uwezekano mkubwa show ikakosa msisimko kwa kuwa washiriki watakuwa wanafahamiana strategies zao. Tayari kuna watu wanajulikana kwa sifa ya kuwa snakes, wengine walitumia mahusiano kama strategy, na wengine walitumia ukimya ama kutokuongea kabisa na hivyo wanasahaulika kama wapo.
Mtu kama Richird akirudi na akamtokea demu, hakuna demu atamwamini tena kutokana na kile tulichokiona kwa RICHIANA. Mtu kama Sheila (Kenya, BBA III) akirudi hakuna mwanaume atamwamini, maana siku Sheila anatoka, TK (Zambia, BBA III) alilia kama mtoto mdogo, kumbe Sheila alikuwa anamtumia tu ili aendelee kubaki ndani ya jumba.
Mtu kama Kwaku a.k.a Kwaku-T (Ghana, BBA II) ambaye alikuwa anabadilisha wasichana pindi gf anapotolewa. Au mtu kama Code (Malawi, BBA II) ambaye alikuwa anamsalendia Maurine (Uganda) kumbe nje ya Jumba ameacha gf mjamzito. Kuna washiriki walitumia ukimya na kazi za jikoni + usafi wa jumba kama strategy na iliwasaidia kufika mbali, mfano: Hazel (Malawi, BBA III), Geraldine (Nigeria, BBA IV), Cherise (Zambia BBA I) na Ofuneka (Nigeria BBA II).
Kwenye show kama hizi inapendeza zaidi wakiletwa washiriki ambao hawajuani kabisa na kila mtu anakuwa na strategy yake moyoni na hata kama ataitoa kwa wengine ni kwa malengo ya alliance. Lakini kwa show ya mwaka huu, already washiriki watakuwa wanajua true colors za washiriki wenzao.
Katika BBA seasons zilizotangulia the top 3 walikuwa ni hawa:
BBA I: Cherise (Zambia, winner); Mwisho Mwampamba (Tanzania); na Tapuwa (Zimbabwe).
BBA II: Richard (Tanzania, winner); Ofuneka (Nigeria); Tatiana (Angola).
BBA III: Ricco (Angola, winner); Hazel (Malawi); Munya (Zimbabwe).
BBA IV: Kevin (Nigeria, winner); Emma (Angola); Eddie (Namibia).
Washiriki wengi wa season ya kwanza kabisa kwa sasa watakuwa na maisha ya tofauti kabisa na inawezekana umri umeenda, kwa hiyo uwezekano wa kuwaona ma-star wa BBA I ni mdogo.
Ambao ningependa kuwaona tena ni pamoja na hawa wafuatao: Kwaku-T (Ghana, BBA II), Sheila (Kenya, BBA III), LaToya (TZ, BBA III), Phil (Uganda, BBA IV), Liziwe (South Africa, BBA IV), Uti (Nigeria, BBA III), Munya (Zimbabwe, BBA III), Bertha (Zimbabwe, BBA II), Meryl (Namibia, BBA II); Maxwell (Zambia, BBA II), Lerato (South Africa, BBA II); Emma (Angola, BBA IV)
Jumapili saa mbili usiku kwa saa za hapa kwetu siyo mbali sana, tutawaona hao nyota waliowahi kuwika kwenye seasons zilizopita ili tuone watakuja na kipya kipi katika show ya mwaka huu.
Wapenzi na mashabiki wa BBA karibuni tena kwenye kijiwe chetu, maana kuna wengine walishapotea kabisa, mfano Kelelee sijawahi kumuona tena. Nemesis na Mbogela najua wao ni permanent members wa vijingine.