BBC na propaganda za kisiasa, kumuongezea maneno Rais Magufuli

BBC na propaganda za kisiasa, kumuongezea maneno Rais Magufuli

Dam55

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2015
Posts
5,641
Reaction score
11,958
Screenshot_20210120-094020.png

Magufuli awataka wakulima wa taifa hilo kulisha dunia baada ya corona


Rais Magufuli wa Tanzania.
IMG_20210120_094044.jpg


Rais wa Tanzania John Magufuli, amesihi wakulima nchini humo kuongeza kiwango cha uzalishaji wa chakula akibashiri uhaba wa chakula duniani baadaye mwaka huu kwasababu ya janga la virusi vya corona.

Aliwataka wakulima kutumia vizuri fursa ya kupungua kwa uzalishaji kwa nchi ambazo huwa ni wazalishaji wakubwa wa chakula kwasababu ya masharti ya afya yaliyowekwa kote duniani.

"Mwaka huu kuna uwezekano wa kutokea kwa baa kubwa la jaa duniani kwasababu watu wengi wanazingatia hatua za kutotoka nje kujikinga dhidi ya corona, lakini hilo halistahili kutukatisha tamaa kwasababu hata sheria hizo zikiwekwa bado watahitaji kula, tutakuza mazao na kuyauza," amezungumza na wananchi kaskazini magharibi mwa mji wa Bukoba.

Rais wa Tanzania amekuwa akikosolewa kwa kutozingatia sana ukubwa wa madhara ya janga la corona, na kusema mara kadhaa kwamba mgogoro wa afya umekuzwa na kukejeli wanaovaa barakoa.

Mnamo mwezi Juni alitangaza kuwa nchi hiyo "haina virusi vya corona" kwasababu ya maombi ya wananchi.

Shirika la Afya Dunia (WHO) limeonesha wasiwasi wake juu ya mkakati wa serikali ya nchi hiyo katika kukabiliana na Covid-19

SAWALI KWAKO WEWE MTANZANIA, NI KWELI KUWA RAIS MAGUFULI ALITAMKA MANENO KAMA HAYO NA JINSI YALIVYO ELEZWA NA BBC?
 
SAWALI KWAKO WEWE MTANZANIA, NI KWELI KUWA RAIS MAGUFULI ALITAMKA MANENO KAMA HAYO NA JINSI YALIVYO ELEZWA NA BBC?
Mkuu ulisikiliza kweli au unapinga wakati hata mkutano wake hukusikiliza?
 
Kwani BBC wakisema Rais JPM kasema kutakuwa na Njaa duniani na inajulikana hata FAO nao walishasema hivyo hivyo BBC wana tatizo gani pia?
 
Nilisikiliza vizuri tu hotuba ya rais. Kweli alisema hivyo. Hakuna ubishi. Kama una "clip" ya hotuba hiyo, rudia kuisikiliza. Lakini hata hivyo rais amekuwa akitusisitiza pamoja na wakulima, tuchape kazi. Mungu ametuepusha na janga la Corona. Tumpongeze rais wetu.
 
Nilidhani umesikiliza alichosema rais, kumbe umekuja na jicho hasi dhidi ya bbc ili kumtetea Magufuli! Ungekaa kimya tu.
Soma hiyo habari kwa makini halafu nenda sikiliza hotuba ya Rais ya jana hatua kwa hatua ndio utajua uhuni walio ufanya hao weledi wa habari duniani.

Nikae kimya kwasababu wewe ndio mwenye haki ya kuongea sivyo?

Lete hapa hiyo clip ya Rais aliposema kuwa tuilishe dunia kwa chakula kitacho zalishwa Tanzania.
 
Back
Top Bottom