BBC na propaganda za kisiasa, kumuongezea maneno Rais Magufuli

BBC na propaganda za kisiasa, kumuongezea maneno Rais Magufuli

Wengi wao ni wakenya! Mkenya akiona mzungu anaweza kukaa chini kwa kumsujudia, ni kama Lisu tu
Ni kweli watangazaji wa Kiswahili wa BBC wengi ni Wakenya na wachache Wanyarwanda kwa sababu wanajua Kingereza na Kiswahili kizuri kwani Kisukuma na Kiswahili cha mitaani (creole) hakitakiwi BBC, Shirika la Serikali ya Uingereza. Wabongo wajuwe hawawezi kufundisha au kutangaza kwa Kiswahili nchi za nje kama hawajui lughà zao, wao wafie TBC na media zingine zinazounga mkono juhudi.
 
Ni kweli wengi wao ni Wakenya kwa sababu wanajua Kingereza na Kiswahili kizuri kwani Kisukuma na Kiswahili cha mitaani hakitakiwi BBC, Shirika la Serikali ya Uingereza. Huwezi kufundisha au kutangaza kwa Kiswahili nchi za nje kama hujui lughà zao!
Ndio maana mnawainamia sana hao wazungu?
 
Ndio maana mnawainamia sana hao wazungu?
Afadhali kuwainamia wazungu wema wanatoa ajira kwa Watanzania wenzetu kuliko kuwainamia mashetani wa Kisukuma wanaotoa ajira kwa Wasukuma wenzao wasio wasomi wakiwaacha wasomi wa makabila mengine wakizunguka na bahasha za khaki wakitafuta kazi bila mafanikio.
 
Katika hili mbona alisema kabisa kuwa wakulima walime chakula cha kutosha kwaajili ya watu watakao kosa chakula kipindi cha Corona...
BBC wameweka lugha rahisi tuu kuwa ametabiri na hilo jambo liko wazi kabisa kuwa lazima kutakuwa na uhaba wa chakula kutokana na Corona....
Nafikiri hakuna propaganda yeyote ile hapo
 
View attachment 1681732
Magufuli awataka wakulima wa taifa hilo kulisha dunia baada ya corona


Rais Magufuli wa Tanzania.
View attachment 1681733

Rais wa Tanzania John Magufuli, amesihi wakulima nchini humo kuongeza kiwango cha uzalishaji wa chakula akibashiri uhaba wa chakula duniani baadaye mwaka huu kwasababu ya janga la virusi vya corona.

Aliwataka wakulima kutumia vizuri fursa ya kupungua kwa uzalishaji kwa nchi ambazo huwa ni wazalishaji wakubwa wa chakula kwasababu ya masharti ya afya yaliyowekwa kote duniani.

"Mwaka huu kuna uwezekano wa kutokea kwa baa kubwa la jaa duniani kwasababu watu wengi wanazingatia hatua za kutotoka nje kujikinga dhidi ya corona, lakini hilo halistahili kutukatisha tamaa kwasababu hata sheria hizo zikiwekwa bado watahitaji kula, tutakuza mazao na kuyauza," amezungumza na wananchi kaskazini magharibi mwa mji wa Bukoba.

Rais wa Tanzania amekuwa akikosolewa kwa kutozingatia sana ukubwa wa madhara ya janga la corona, na kusema mara kadhaa kwamba mgogoro wa afya umekuzwa na kukejeli wanaovaa barakoa.

Mnamo mwezi Juni alitangaza kuwa nchi hiyo "haina virusi vya corona" kwasababu ya maombi ya wananchi.

Shirika la Afya Dunia (WHO) limeonesha wasiwasi wake juu ya mkakati wa serikali ya nchi hiyo katika kukabiliana na Covid-19

SAWALI KWAKO WEWE MTANZANIA, NI KWELI KUWA RAIS MAGUFULI ALITAMKA MANENO KAMA HAYO NA JINSI YALIVYO ELEZWA NA BBC?
Ina maana ukijifungia ndani hutafanya uzalishaji, na ukitoka unahitaji kula. Waliokuwa nje itabidi watoe chakula kwa waliokuwa ndani. Ni fursa ya kuzalisha kwa wingi ili kuuza kwa wingi.
 
Amesema watu wamejifungia ndani kuongopa corona hawalimi - watanzania limeni hawa wanaweza kuwa na njaa mtawauzia chakula kwa bei nzuri-- Sasa huo si UTABIRI ndugu?
 
Amesema watu wamejifungia ndani kuongopa corona hawalimi - watanzania limeni hawa wanaweza kuwa na njaa mtawauzia chakula kwa bei nzuri-- Sasa huo si UTABIRI ndugu?
Soma vizuri hiyo habari mkuu
 
Nilisikiliza vizuri tu hotuba ya rais. Kweli alisema hivyo. Hakuna ubishi. Kama una "clip" ya hotuba hiyo, rudia kuisikiliza. Lakini hata hivyo rais amekuwa akitusisitiza pamoja na wakulima, tuchape kazi. Mungu ametuepusha na janga la Corona. Tumpongeze rais wetu.
Usidanganyike ndugu yangu chukua taadhari corona ipo,ulishawahi sikia mtu amekufa kwa ukimwi( yaani Daktari akaandika marehemu amekufa kwa HIV ) ?? nadhani hakuna, basi na corona iko hivyo
 
Hilo swali siwezi kujibu kwani sijabahatika kumsikiliza.

Ila kuhusu uhaba wa chakula nilishawasikia FAO wakilielezea tu mara kadhaa.
 
Back
Top Bottom