BBC: Putin hakutarajia haya yatafanyika alipoivamia Ukraine

Gama

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
13,265
Reaction score
4,735

Putin hakutarajia haya yatafanyika alipoivamia Ukraine​

th

CHANZO CHA PICHA, REUTERS

Tarehe 24 Februari 2022, Urusi iliivamia Ukraine katika hatua iliyozidisha mzozo wake nan chi hiyo Jirani tangu kuanza kwa usahama mwaka wa 2014

Uvamizi huo ulisababisha mzozo mkubwa zaidi wa wakimbizi barani Ulaya tangu Vita vya pili vya dunia huku zaidi ya Waukraine milioni nane wakikimbia nchi na theluthi moja ya idadi ya watu kuhamishwa.

Hata hivyo vita hivyo vimeleta matokeo ambayo kamwe rais wa Urusi Vladmir Putin hakuyategemea katika mpango wake na wakuu wake wa kijeshi .

Wadadisi wanasem Putin alikuwa na mpango wa kuingia Ukraine na kuidhibiti serikali yan chi hiyo baada ya wiki chache lakini mgogoro huo umedhihirisha kwamba hali sio rahisi kama alivyofikiri .Kando na athari za vita hivyo kwa dunia nzima ,kuna mambo haya manne ambayo Putin hakufikiria yangefanyika

Unaweza pia kusoma

Nato itazidisha wanachama wake​

th
Nchi ambazo awali zilikuwa haziegemei upande wowote ambazo zinapakana na Urusi sasa zinataka kujiunga na muungano wa kujihami wa Nato . Finland na Sweden ni nchi za hivi punde kuiga hatua katika jitihada zao za kujiunga na muungano huo ambao umejitokeza kama mlinzi mkubwa kwa nchi zinazoonekana kuchokozwa na ubabe wa Urusi.

Urusi inapinga vikali mataifa hayo mawili kujiunga na imetumia upanuzi wa muungano wa kijeshi wa kujihami wa nchi za Magharibi kama kisingizio cha vita vyake nchini Ukraine.

Nchi zote mbili zimeshikilia msimamo wa kutoegemea upande wowote kwa miaka, lakini tangu Urusi ilipovamia Ukraine uungwaji mkono wa wanachama wa Nato umeongezeka sana.

Finland na Uswidi zilitangaza nia yao ya kujiunga na muungano wa kujihami wa nchi za Magharibi wenye wanachama 30 mwezi Mei, ili kukabiliana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Awali Uturuki ilitishia kupinga ombi lao lakini baada ya saa nne za mazungumzo katika mkutano wa Nato mjini Madrid nchi hizo tatu zilifikia mwafaka. Viongozi wa Nato wanatarajiwa kuzialika rasmi Finland na Sweden kuwa wanachama kabla ya kumalizika kwa mkutano huo.

Kwanini zinajiunga sasa?
Vitendo vya Vladimir Putin vimesambaratisha hali ya utulivu iliyodumu kwa muda mrefu kaskazini mwa Ulaya, na kuziacha Sweden na Finland zikihisi hatari.

Waziri Mkuu wa zamani wa Ufini Alexander Stubb alisema kujiunga na muungano huo ni "makubaliano yaliyofanywa" kwa nchi yake mara tu wanajeshi wa Urusi walipoivamia Ukraine mnamo tarehe 24 Februari.

Kwa Wafini wengi, matukio ya Ukraine huleta hali wanayoifahamu vizuri. Wanasovieti walivamia Finland mwishoni mwa 1939. Kwa zaidi ya miezi mitatu jeshi la Finland liliweka upinzani mkali, licha ya kuwa idadi yao ilikuwa ndogo sana.

Waliepuka kutawaliwa lakini waliishia kupoteza 10% ya eneo lao.

Kutazama vita nchini Ukraine vikitokea ilikuwa kama kufufua historia hii, alisema Iro Sarkka, mwanasayansi wa siasa katika Chuo Kikuu cha Helsinki. Wafini walikuwa wakitazama mpaka wao wa kilomita 1,340 (maili 830) na Urusi, alisema, na kufikiria: "Je, hii inaweza kutokea kwetu?"

th

CHANZO CHA PICHA, REUTERS

Marekani kuongeza idadi ya wanajeshi wake Ulaya​

Jambo la mwisho ambali Putin alitegemea vita vyake vitasababisha ni hasimu wake mkubwa Marekani kuapa kuongeza idadi ya wanajeshi na silaha karibu na mipaka yake .Kutokana na umoja wan chi za Ulaya na Marekani katika kulaani uvamizi wa Ukraine, Marekani sasa imejipata na fursa ya kuongeza nguvu zake za kijeshi barani Ulaya na karibu na mipaka ya Urusi.

Marekani itaongeza uwepo wake wa kijeshi kote Ulaya kwani Nato ilikubali "mabadiliko ya kimsingi" katika kukabiliana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Makao makuu ya jeshi ya kudumu yataundwa nchini Poland, wakati meli mpya za kivita za Marekani zitaenda Uhispania, ndege za kivita nchini Uingereza na wanajeshi wa ardhini kuelekea Romania.

Bw Biden alisema Nato "inahitajika zaidi kuliko ilivyowahi kuwa".

Muungano huo una maboresho makubwa zaidi tangu Vita Baridi, mkuu wa Nato Jens Stoltenberg alisema.
Mpango huo mpya katika kukabiliana na uvamizi wa Urusi utamaanisha zaidi ya wanajeshi 300,000 walio tayari zaidi mwaka ujao, kutoka kiwango cha sasa cha 40,000.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza (MoD) pia imesema inaongeza kwa kiasi kikubwa vikosi kwa ulinzi wa pamoja wa Nato, na meli zaidi za kivita, ndege za kivita na vikosi vya ardhini vikiwa tayari - ingawa MoD ilisema haitatoa maelezo juu ya idadi kama zilivyo.

Tangazo la Marekani linaona kwamba inaboresha uwepo wake katika bara zima lakini hasa katika Ulaya ya Mashariki ambako makao makuu mapya ya Kikosi cha 5 cha Jeshi yatawekwa.

Bwana Biden alirudia ahadi ya muungano wa "kulinda kila inchi" ya eneo lake, akisema: "Tunamaanisha hivyo tunaposema shambulio dhidi ya mtu mmoja ni shambulio dhidi ya wote.

Kutengwa zaidi na nchi za magharibi​

th

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Vikwazo Zaidi vimezidi kuifuata Urusi na watu mashuhuri katika serikali ya Urusi .

Kampuni kadhaa za kigeni zimeendelea pia kuondoka Urusi na kuitenga Zaidi nchi hiyo kutoka jamii ya kimataifa .

Hatua hiyo imeifanya Urusi kujipata ikiwatafuta washirika wapya hasa barani Afrika na Asia ili kuendelea na ushirikiano wa kibiashara na mauzo ya bidhaa zake .

Vita vya Ukraine kudumu kwa muda mrefu​

th

CHANZO CHA PICHA, AFP
Wadadisi wanakubali kwamba Putin na makamanda wake walijua kwamba uvamizi wa Ukraine ungedumu tu kwa wiki chache.

Hata hivyo hatua ya Ukraine kuanzisha vita vya kujilinda iliwashangaza wengi Mambo yalizidi kuwa mabaya wakati nchi za Ulaya zilipoanza kuipa Ukraine misaada ya kijeshi ili kupambana na Urusi.

Kadri vita hivyo vinavyoendelea kwa kipindi kirefu ndivyo mzozo huo unavyozidi kuwa mbaya kwa pande zote mbili.
 
Putin aliahidi atarusha satan 2 na kulipua nyuklia bomu. Sasa sijui anasubiri nini. Yani watu tuna hamu ya kuvuta iyo mionzi ya nyuklia na kupata ladha yake kabla hatujaonana na Yesu.
 
Hapo hakuna hata moj aambalo anashindwa kukabiliana nalo. Halafu putin alishajiandaa kupigana na NATO ndio mana propaganda za waNATO kama hizi hazipungui kwenye vyombo vyao vya habari,
We Nazi kweli
 
Hapo hakuna hata moj aambalo anashindwa kukabiliana nalo. Halafu putin alishajiandaa kupigana na NATO ndio mana propaganda za waNATO kama hizi hazipungui kwenye vyombo vyao vya habari.
Kwasasa imedhihirika kuwa ameishiwa silaha. Imeonekana ameanza kutumia makombora yaliyoundwa miaka ya 1960

TAZAMA EXTRACT HII KUTOKA BBC

Makombora yaliyotumiwa katika mashambulizi ya Urusi katika eneo la Odesa na kusababisha vifo vya takriban watu 19, akiwemo mtoto mmoja, yalikuwa ya aina sawa na yale yaliyotumiwa dhidi ya jumba la maduka la Kremenchuk Jumatatu wiki jana Ukraine imesema.

Wizara ya ulinzi ya Kyiv ilizitaja silaha hizo kuwa ni Kh-22 (X-22) - aina ya kombora la zamani la kusafiri lililotengenezwa miaka ya 1960.

Tulilitazama kombora hilo kwa undani zaidi mapema wiki hii - wachambuzi wa masuala ya ulinzi wanapendekeza matumizi yake yanamaanisha kuwa Moscow inapoteza makombora ya kisasa zaidi.

Yanarushwa kutumia ndege za kivita za Tupolev-22, na ni silaha ya masafa ya kati na katika hali yao ya asili hayakuwa sahihi. Kwa miaka mingi mfumo wa mwongozo ungeweza kuboreshwa, lakini hatujui ikiwa hii inatumika kwa silaha zilizofyatuliwa hivi majuzi.

Hawa waliosema RUSSIA kabakisha msosi wasiku tatu[emoji23][emoji23][emoji23]
Kama kaishiwa na silaha sasa niwakati muafaka wa NATO kwenda kuisaidia UKRAINE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Putin hakutarajia haya yatafanyika alipoivamia Ukraine​

th

CHANZO CHA PICHA, REUTERS

Tarehe 24 Februari 2022, Urusi iliivamia Ukraine katika hatua iliyozidisha mzozo wake nan chi hiyo Jirani tangu kuanza kwa usahama mwaka wa 2014

Uvamizi huo ulisababisha mzozo mkubwa zaidi wa wakimbizi barani Ulaya tangu Vita vya pili vya dunia huku zaidi ya Waukraine milioni nane wakikimbia nchi na theluthi moja ya idadi ya watu kuhamishwa.

Hata hivyo vita hivyo vimeleta matokeo ambayo kamwe rais wa Urusi Vladmir Putin hakuyategemea katika mpango wake na wakuu wake wa kijeshi .

Wadadisi wanasem Putin alikuwa na mpango wa kuingia Ukraine na kuidhibiti serikali yan chi hiyo baada ya wiki chache lakini mgogoro huo umedhihirisha kwamba hali sio rahisi kama alivyofikiri .Kando na athari za vita hivyo kwa dunia nzima ,kuna mambo haya manne ambayo Putin hakufikiria yangefanyika

Unaweza pia kusoma

Nato itazidisha wanachama wake​

th
Nchi ambazo awali zilikuwa haziegemei upande wowote ambazo zinapakana na Urusi sasa zinataka kujiunga na muungano wa kujihami wa Nato . Finland na Sweden ni nchi za hivi punde kuiga hatua katika jitihada zao za kujiunga na muungano huo ambao umejitokeza kama mlinzi mkubwa kwa nchi zinazoonekana kuchokozwa na ubabe wa Urusi.

Urusi inapinga vikali mataifa hayo mawili kujiunga na imetumia upanuzi wa muungano wa kijeshi wa kujihami wa nchi za Magharibi kama kisingizio cha vita vyake nchini Ukraine.

Nchi zote mbili zimeshikilia msimamo wa kutoegemea upande wowote kwa miaka, lakini tangu Urusi ilipovamia Ukraine uungwaji mkono wa wanachama wa Nato umeongezeka sana.

Finland na Uswidi zilitangaza nia yao ya kujiunga na muungano wa kujihami wa nchi za Magharibi wenye wanachama 30 mwezi Mei, ili kukabiliana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Awali Uturuki ilitishia kupinga ombi lao lakini baada ya saa nne za mazungumzo katika mkutano wa Nato mjini Madrid nchi hizo tatu zilifikia mwafaka. Viongozi wa Nato wanatarajiwa kuzialika rasmi Finland na Sweden kuwa wanachama kabla ya kumalizika kwa mkutano huo.

Kwanini zinajiunga sasa?
Vitendo vya Vladimir Putin vimesambaratisha hali ya utulivu iliyodumu kwa muda mrefu kaskazini mwa Ulaya, na kuziacha Sweden na Finland zikihisi hatari.

Waziri Mkuu wa zamani wa Ufini Alexander Stubb alisema kujiunga na muungano huo ni "makubaliano yaliyofanywa" kwa nchi yake mara tu wanajeshi wa Urusi walipoivamia Ukraine mnamo tarehe 24 Februari.

Kwa Wafini wengi, matukio ya Ukraine huleta hali wanayoifahamu vizuri. Wanasovieti walivamia Finland mwishoni mwa 1939. Kwa zaidi ya miezi mitatu jeshi la Finland liliweka upinzani mkali, licha ya kuwa idadi yao ilikuwa ndogo sana.

Waliepuka kutawaliwa lakini waliishia kupoteza 10% ya eneo lao.

Kutazama vita nchini Ukraine vikitokea ilikuwa kama kufufua historia hii, alisema Iro Sarkka, mwanasayansi wa siasa katika Chuo Kikuu cha Helsinki. Wafini walikuwa wakitazama mpaka wao wa kilomita 1,340 (maili 830) na Urusi, alisema, na kufikiria: "Je, hii inaweza kutokea kwetu?"

th

CHANZO CHA PICHA, REUTERS

Marekani kuongeza idadi ya wanajeshi wake Ulaya​

Jambo la mwisho ambali Putin alitegemea vita vyake vitasababisha ni hasimu wake mkubwa Marekani kuapa kuongeza idadi ya wanajeshi na silaha karibu na mipaka yake .Kutokana na umoja wan chi za Ulaya na Marekani katika kulaani uvamizi wa Ukraine, Marekani sasa imejipata na fursa ya kuongeza nguvu zake za kijeshi barani Ulaya na karibu na mipaka ya Urusi.

Marekani itaongeza uwepo wake wa kijeshi kote Ulaya kwani Nato ilikubali "mabadiliko ya kimsingi" katika kukabiliana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Makao makuu ya jeshi ya kudumu yataundwa nchini Poland, wakati meli mpya za kivita za Marekani zitaenda Uhispania, ndege za kivita nchini Uingereza na wanajeshi wa ardhini kuelekea Romania.

Bw Biden alisema Nato "inahitajika zaidi kuliko ilivyowahi kuwa".

Muungano huo una maboresho makubwa zaidi tangu Vita Baridi, mkuu wa Nato Jens Stoltenberg alisema.
Mpango huo mpya katika kukabiliana na uvamizi wa Urusi utamaanisha zaidi ya wanajeshi 300,000 walio tayari zaidi mwaka ujao, kutoka kiwango cha sasa cha 40,000.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza (MoD) pia imesema inaongeza kwa kiasi kikubwa vikosi kwa ulinzi wa pamoja wa Nato, na meli zaidi za kivita, ndege za kivita na vikosi vya ardhini vikiwa tayari - ingawa MoD ilisema haitatoa maelezo juu ya idadi kama zilivyo.

Tangazo la Marekani linaona kwamba inaboresha uwepo wake katika bara zima lakini hasa katika Ulaya ya Mashariki ambako makao makuu mapya ya Kikosi cha 5 cha Jeshi yatawekwa.

Bwana Biden alirudia ahadi ya muungano wa "kulinda kila inchi" ya eneo lake, akisema: "Tunamaanisha hivyo tunaposema shambulio dhidi ya mtu mmoja ni shambulio dhidi ya wote.

Kutengwa zaidi na nchi za magharibi​

th

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Vikwazo Zaidi vimezidi kuifuata Urusi na watu mashuhuri katika serikali ya Urusi .

Kampuni kadhaa za kigeni zimeendelea pia kuondoka Urusi na kuitenga Zaidi nchi hiyo kutoka jamii ya kimataifa .

Hatua hiyo imeifanya Urusi kujipata ikiwatafuta washirika wapya hasa barani Afrika na Asia ili kuendelea na ushirikiano wa kibiashara na mauzo ya bidhaa zake .

Vita vya Ukraine kudumu kwa muda mrefu​

th

CHANZO CHA PICHA, AFP
Wadadisi wanakubali kwamba Putin na makamanda wake walijua kwamba uvamizi wa Ukraine ungedumu tu kwa wiki chache.

Hata hivyo hatua ya Ukraine kuanzisha vita vya kujilinda iliwashangaza wengi Mambo yalizidi kuwa mabaya wakati nchi za Ulaya zilipoanza kuipa Ukraine misaada ya kijeshi ili kupambana na Urusi.

Kadri vita hivyo vinavyoendelea kwa kipindi kirefu ndivyo mzozo huo unavyozidi kuwa mbaya kwa pande zote mbili.
Ni Putin au wao ndo hawakutarajia yatawakuta hayo ya kumwekea vikwazo wanalia wao?
 
Afu kuna watu wanafikiri kwamba hata kama Putin atapigana vita hii kwa miaka 3 kwamba hataathirika kiuchumi ni ujinga.
 
Jamaa amempa uhalali Marekani na washika wake NATO kwa ujumla kujipanua zaidi..wazungu ambao wanajua kujitoa sadaka ili kufanikisha mambo yao.. Russia alitaka ushindi wa muda mfupi ila wao wanaendelea kummenya mdogo mdogo na tena hawataki hii vita viishe...
 
Bwana Putin mwenyewe keshasema hawezi kuuza usalama wa nchi yake kwa manufaa kiduchu ya uchumi

Yuko wapi Ghadaff aliyepiga chini mipango yake ya kumiliki nyuklia kwa ahadi za uongo toka kwa UK
 
Afu kuna watu wanafikiri kwamba hata kama Putin atapigana vita hii kwa miaka 3 kwamba hataathirika kiuchumi ni ujinga.
Sio ujinga, ni uzezeta. Vyombo vya habar vyote huko russia vimepigwa pini, la sivyo tungesikia mengi.
 
Jamaa amempa uhalali Marekani na washika wake NATO kwa ujumla kujipanua zaidi..wazungu ambao wanajua kujitoa sadaka ili kufanikisha mambo yao.. Russia alitaka ushindi wa muda mfupi ila wao wanaendelea kummenya mdogo mdogo na tena hawataki hii vita viishe...
wanamchosha tu mdogo mdogo wanajua watamnasia wapi, ogopa sana intelligensia ya watu wa magharibi + US. Hapo Putin ajiandae kisaikologia, vita inakwenda miaka 3 na zaidi huku Ukraine akipata support zote.
 
Mkuu vita ya Syria ina umri gani ?
 
Kwasasa imedhihirika kuwa ameishiwa silaha. Imeonekana ameanza kutumia makombora yaliyoundwa miaka ya 1960

TAZAMA EXTRACT HII KUTOKA BBC

Makombora yaliyotumiwa katika mashambulizi ya Urusi katika eneo la Odesa na kusababisha vifo vya takriban watu 19, akiwemo mtoto mmoja, yalikuwa ya aina sawa na yale yaliyotumiwa dhidi ya jumba la maduka la Kremenchuk Jumatatu wiki jana Ukraine imesema.

Wizara ya ulinzi ya Kyiv ilizitaja silaha hizo kuwa ni Kh-22 (X-22) - aina ya kombora la zamani la kusafiri lililotengenezwa miaka ya 1960.

Tulilitazama kombora hilo kwa undani zaidi mapema wiki hii - wachambuzi wa masuala ya ulinzi wanapendekeza matumizi yake yanamaanisha kuwa Moscow inapoteza makombora ya kisasa zaidi.

Yanarushwa kutumia ndege za kivita za Tupolev-22, na ni silaha ya masafa ya kati na katika hali yao ya asili hayakuwa sahihi. Kwa miaka mingi mfumo wa mwongozo ungeweza kuboreshwa, lakini hatujui ikiwa hii inatumika kwa silaha zilizofyatuliwa hivi majuzi.

Nani hajui kwamba BBC inatumika kama his masters Voice ie kusambaza propaganda za magharibi by demonising Russia/Putin hilo ndilo lengo kuu la BBC pamoja MSM media za huko Merikani - habari nyingi kuhusu vita ya Ukraine ni habari za kutunga tu.
 
Back
Top Bottom