Hata mm nashangaa maana tuliambiwa na lisu kuwa tutashitakiwa MIGA matokeo yake hatujashitakiwa wala nn,pia tuliambiwa na Serikali kuwa makinikia hayataondoka na tutajenga smelter hapa hapa,lakini matokeo yake makinikia bado yanaondoka pia smelter haijengwa mpaka leo,Sasa sisi wakazi wa huku Katoro tuamini kuwa lissu alitudanganya na Serikali pia imetudanganya?au nyinyi wa huko mjini mnaonaje huko?
..inabidi uelewe barrick ni nani, na accacia ni nani ili usiweze kudanganyika ktk issue hii.
..barrick ndio walioanzisha kampuni ya accacia. walianza kwa kuimiliki 100% lakini baadae wakauza nadhani 35%++ ya hisa zao.
..wakati mgogoro huu unatokea barrick walikuwa ni majority share holders wa accacia, huku shares zilizobaki zikimilikiwa na watu wengine.
Nini kilitokea?
..serikali ilitoa ripoti za uchunguzi kwamba accacia wameiba madini na kukwepa kodi kiwango cha usd 191 billion.
..baada ya ripoti hiyo kutoka accacia waliipinga kupitia wasemaji wao mbalimbali. wakati huohuo ceo wa barrick alikuja hapa nchini na kukutana na Jpm ikulu.
..kwa upande mmoja serikali ikawa inasema accacia ni wezi. Na upande wa pili ikawa inasema barrick ni watu wazuri na tunafanya mazungumzo nao.
Tundu Lissu alisema nini?
..alisema kwamba ripoti zile haziaminiki. Na alisema tafiti za huko nyuma, zilizofanywa na makampuni mbalimbali, pamoja na SERIKALI yenyewe, zinaonyesha kwamba ripoti za Prof.Mruma na Prof.Ossoro zina walakini.
..vilevile Tundu Lissu alidai kwamba ripoti hizo na jinsi zilivyoandaliwa haziwezi kutusaidia ikiwa tutaamua kuwapeleka accacia mahakamani, au ikiwa accacia watatushitaki. Na alikwenda mbali na kusema ikiwa accacia watatushitaki watatushinda.
Je, tulishitakiwa?
..NDIO, tulishitakiwa.
..accacia walifungua kesi dhidi ya serikali ktk mahakama ya kimataifa wakipinga madai ya kudaiwa kodi ya usd 191 billion.
..kesi ya accacia dhidi ya serikali ya Tz ilisitishwa baada ya barrick kufika bei na kuwanunua minority share holder. hivyo basi accacia ikarudi kuwa mikononi mwa barrick 100%.
Matokeo ya kufutwa kesi ni nini?
..kesi ilipositishwa ndipo barrick sasa walipoweza kuendelea na ahadi ya kuilipa serikali " kishika uchumba " cha usd 300 million walichokuwa wameahidi mwaka 2017. serikali ya Tanzania nayo iliachana na madai yake ya usd 191 billion. Pia tulikubaliana kuanzisha kampuni ya ubia inayoitwa Twiga. Makinikia yalianza kusafirishwa tena kwenda ng'ambo.
Usd 191 billion vs Usd 300 million.
..ukichukua 191 billion ukagawanya na 300 million unapata 636.666.
..maana yake ni kwamba barrick wakiamua kulipa 300 million kila mwaka itawachukua miaka 637 kumaliza deni la usd 191 billion.
..pia ukiibiwa 191 billion halafu ukakubali na kuridhika kulipwa 300 million, basi wewe huna tofauti na mtu aliyeibiwa shilingi 637 halafu ukakubali kulipwa shilingi 1.
Yatokanayo.
..Tundu Lissu aliitwa msaliti na kumiminiwa risasi 16 ili afe.
..Inasemekana alipigwa risasi kama adhabu kwa kuongea na Deo Mwanyika, Mtanzania mtendaji wa ngazi ya juu ktk accacia na barrick.
..Deo Mwanyika na wenzake walifunguliwa kesi na serikali wakidaiwa kuisaida accacia kukwepa kodi.
..Deo Mwanyika na wenzake walilipishwa faini ya mabilioni ya shilingi baada ya majadiliano na Dpp.
..Wiki chache baada ya kutoka kizuizini Deo Mwanyika alichaguliwa na kupitishwa na Kamati Kuu ya CCM kugombea ubunge wa Njombe mjini.
cc
Abdul Mganyizi