Uchaguzi 2020 BBC Swahili wamesema kwenye makubaliano yetu na kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick kwenye zile asilimia ni kama tumepigwa

Uchaguzi 2020 BBC Swahili wamesema kwenye makubaliano yetu na kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick kwenye zile asilimia ni kama tumepigwa

You are talking about sheria za kimataifa?! Unataka nilete humu ile video ya wazungu wa Lissu akiwemo Amsterdam na wenzake walichopanga dhidi ya Tanzania...wamepanga kuchochea maandamano na mauaji ili vurugu zitokee na kinachoitwa jumuiya ya kimataifa iitishe mkutano wa usuluhishi na Lissu...wazungu hao wanasema na kuropoka bila aibu kwamba ni lazima damu imwagike Tanzania...kuchomwa kwa ofisi za chadema ni miongoni mwa mikakati hiyo...
Uzushi na upuuzi mtupu!
 
Kama ni waongo basi fungia Star TV ili watu tusisikie "uongo".
No BBC sio waongo, bali wamejikanganya kwa kuwategemea watu fulani fulani walio wadanganya makubaliano ya 2017 yamesainiwa, kitu ambacho sii kweli, that was only a draft, makubaliano yaliyosainiwa ni mkataba mmoja tuu!.
P
 
P kuna baadhi ya hoja za wadau humu umeshindwa kuzijibu nikusaidie mkuu?

Nimeshubiri sana ujibu hoja ya Teamanaconda kwenye post #30. Nilitaka kumjibu nikaona sio ustaarabu kudandia ingali nakuona bado kwenye uzi.

Itapendeza pia kumjibia muheshimiwa barafuyamoto naye naona ametoka kabisa, ile mimi imenitoka kidogo
 
Kuna wakati nalazimika kuamini kuwa hizi hasara tunazopata kama taifa sio kwamba viongozi hawajui(mbumbumbu) au labda inatokea kwa bahati mbaya HAPANA.
Hawa jamaa wanasaini mikataba makusudi kabisa wakijua % ngapi itaingia serikalini na % ngapi itaingia mifukoni mwao. Na ndio maana mtu anaingia kwenye nafasi za juu serikalini kachoka kachakaa, miaka mi-5 ukimwangalia anatoka ana pesa chafu hatari.
Halafu kuna nzi wa kijani wanakomaa na sisi humu kwenye mitandao wakijidai kutetea na kujidai kwamba ni wazalendo, hivi wanaujua uzalendo???
Leo hii sema posho zote zinafutwa na mishahara inapunguzwa, uone kama kuna atakayebaki na kung'ang'ania central zone. HAKUNA MZALENDO HATA M'MOJA PALE LUMBUMBA, WAMEJAZANA WAPIGAJI TUPU.
 
Nimemsikiliza Zuhura Yanus, BBC ni waongo, hakuna mkataba wala makubaliano ya 2017, mkataba ni mmoja tuu, ule uliosainiwa Ikulu 2019!.
Yale ya 2017 yalikuwa ni mapendekezo tuu.
BBC Swahili Iache Uongo!.

NB, uongo kama huu wa BBC pia uliwahi kuletwa na ZZK, baada ya kuona makubaliano yamekuwa initialed, akaandika mkataba umesainiwa.
Tulisaidia kufafanua
Japo Kazi ya Upinzani ni Kupinga, Lakini Sio Kupinga Kila Kitu, Kwenye Maslahi Ya Taifa, Tutangulize Utaifa, Tuwe Wamoja, Wakweli na Tusipotoshe.
P
Kuna chochote kilichobadilika kwenye yale mapendekezo na mkataba uliosainiwa 2019?

Je utekelezaji wa mkataba umefikia hatua gani ?

By the way naipongeza serikali kwa kuanzisha masoko ya madini
 
Kwenye Swala la mikataba hasa madini bila kutoa damu! Bado Mabeberu yataendele kuitwa hivyohivyo!

Hiyo ndiyo inapaswa iwe vita sasa! Zingine hizi za kuoneana Sisi Kwa Sisi, Tatalaaniwa bule

Swala la mikataba ya madini nadhani ipo shida kubwa kuliko tunavyosikia,
Kama ni vita tafadhari zianze upya
Awamu ya tano walikuwa wanatengeneza regime mpya ya kuwawezesha kuiba wao wenyewe tu siyo kwa manufaa ya watanzania.

Wangekuwa na dhamira njema wangeshapeleka mikataba ya madini kujadiliwa bungeni kama sheria inavyotaka
 
You are talking about sheria za kimataifa?! Unataka nilete humu ile video ya wazungu wa Lissu akiwemo Amsterdam na wenzake walichopanga dhidi ya Tanzania...wamepanga kuchochea maandamano na mauaji ili vurugu zitokee na kinachoitwa jumuiya ya kimataifa iitishe mkutano wa usuluhishi na Lissu...wazungu hao wanasema na kuropoka bila aibu kwamba ni lazima damu imwagike Tanzania...kuchomwa kwa ofisi za chadema ni miongoni mwa mikakati hiyo...
Mkuu haya weka hapa tujionee wenyewe.
 
Hata mm nashangaa maana tuliambiwa na lisu kuwa tutashitakiwa MIGA matokeo yake hatujashitakiwa wala nn,pia tuliambiwa na Serikali kuwa makinikia hayataondoka na tutajenga smelter hapa hapa,lakini matokeo yake makinikia bado yanaondoka pia smelter haijengwa mpaka leo,Sasa sisi wakazi wa huku Katoro tuamini kuwa lissu alitudanganya na Serikali pia imetudanganya?au nyinyi wa huko mjini mnaonaje huko?

Mkuu nitakujibu huja zako zote ngoja wenzangu watangulie kwanza. Kwenye hili Raisi amepambana haswa tuache kubeza..

Hata ile kuyazuia kwa muda makinikia japo yalikuja kuendelea kutoka, ilitosha kuwatia presha barrick na kuwaleta kwenye makubaliano mapya bila kuathirika na mikataba tuliyosaini kimakosa huko nyuma.

Kuhusu smelter nadhani hizo zilikuwa hoja za kuwapa hope wanachi na kuwafanya kuwa positive katika kile tunajaribu kufanya. Hata unapofungua biashara yoyote nadhani kuna hopes unakuwa nazo na hata kuziandika kabisa katika strategic plan japo kuna uwezekano usizifikie labda mpaka baada ya muda mrefu.
 
..barrick wametupiga.

..serikali ilisema tumeibiwa usd 191 billion.

..baada ya "majadiliano" tukakubali kulipwa usd 300 million.

..hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuibiwa 191 billion halafua akaridhika kulipwa 300 million.

..hapo ndipo barrick walipotupiga.
 
Ni kweli tumerudi kuwapigia magoti mabeberu, oooh tutachenjua mchanga hapahapa, kiko wapi sasa?
 
Mkuu nisaidie kuelewa kidogo hapa. Economic benefits tutakazogawana 50/50 ni zipi tofauti na hii share of profit?
Mambo mengi yaliyoanishwa kwenye hii 50/50 economic ni mambo yanayofall kwenye corporate social responsibility tu.
 
Mkuu haya weka hapa tujionee wenyewe.
Nikiweka hapa itakuwa issue kubwa mno...binafsi nimeiangalia ile video nikashangaa na kuogopa namna wazungu wale walivyoandaa mipango...yaani bila hata aibu wanataka watu wafe Tanzania ili iwe vurugu kubwa ...
 
You are talking about sheria za kimataifa?! Unataka nilete humu ile video ya wazungu wa Lissu akiwemo Amsterdam na wenzake walichopanga dhidi ya Tanzania...wamepanga kuchochea maandamano na mauaji ili vurugu zitokee na kinachoitwa jumuiya ya kimataifa iitishe mkutano wa usuluhishi na Lissu...wazungu hao wanasema na kuropoka bila aibu kwamba ni lazima damu imwagike Tanzania...kuchomwa kwa ofisi za chadema ni miongoni mwa mikakati hiyo...
Video ?.
 
Nikiweka hapa itakuwa issue kubwa mno...binafsi nimeiangalia ile video nikashangaa na kuogopa namna wazungu wale walivyoandaa mipango...yaani bila hata aibu wanataka watu wafe Tanzania ili iwe vurugu kubwa ...
Niwekee PM au nipe link niitafute.
 
Back
Top Bottom