Walicho eleza ni kwamba kampuni ya Barrick na Serikali ya Tanzania wana gawana faida 50% kwa 50% ila umiliki wa kampuni ya Barrick ni 84%- Barrick, 16% Serikali. Unaweza kufikiri kwamba Barrick wame tudhulumu kwa umiliki wao wa asilimia 84 lakini umiliki wa kampuni una maanisha mambo mengi. Kwanza kabisa sisi kama Tanzania hatu miliki vifaa na teknolojia zinazo hitajika kwenye uchimbaji wa madini. Hii inaweza ikawa sababu moja ya sisi kutokuwa na asilimia kubwa kwenye umiliki. Lazima tukubali kwamba kampuni ni yao, wao wanakuja na teknolojia ambayo sisi hatuna na ambayo hawawezi kutu fundisha kwasababu hiyo ndiyo biashara yao. Kingine kikubwa kinacho husiana na umiliki ni uendeshaji wa kampuni. Lazima kwa njia moja au nyingine, waajiriwa wengi wa kampuni hiyo, wana lipwa na Barrick wenyewe. Kwangu mimi naona ni wazo zuri kwa sisi kuwa na watu wachache kuangalia uendeshaji wa Kampuni bila kubeba mzigo wa kusimamia kila kitu. Mwisho wa siku faida tuna gawana sawa. Mfano ni kumruhusu mtu aendeshe biashara yako bila wewe kuhusika kwa kiasi kikubwa na baadaye kugawana mapato.