BBC Swahili yafungua ofisi za kisasa nchini

BBC Swahili yafungua ofisi za kisasa nchini

Joined
Jun 26, 2014
Posts
48
Reaction score
15
Kwa mara ya kwanza kituo cha BBC ambacho kinarusha vipindi vyake moja kwa moja London toka mwaka 1957 hadi sasa hivi wakati naandika uzi, kwa sasa matangazo yatakuwa yanarushwa dsm Tnzania kwa mara ya kwanza, wandugu mnaonaje,je kiswahili kinakuwa au kinatupwa

BBC Swahili yafungua ofisi za kisasa nchini

Na Mwandishi Wetu, Mwananchi

Ni kwa ajili ya kuhudumia nchi za Afrika Mashariki kupitia redio, simu na tovuti.

Dar es Salaam. Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), limefungua ofisi zake jijini hapa kwenye Jengo la Tangaza, Mikocheni, zenye vifaa vya kisasa vilivyogharimu Dola 1 milioni za Marekani.

Akizungumza katika uzinduzi wa ofisi hizo mwishoni mwa wiki, mhariri wa BBC Africa, Solomon Mugera alisema: "Kwa hakika ni jambo la kujivunia kwa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, kwa sababu ni moja ya idhaa za kimataifa zinazopendwa kutokana na ufanisi wake mkubwa."

BBC imefungua ofisi hiyo kwa ajili ya nchi za Afrika Mashariki kwa matangazo yote ya redio, tovuti na huduma ya habari katika simu za mkononi kupitia Idhaa ya Kiswahili. Alisema wakati mashabiki wa BBC nchini wakisherehekea ujio wa Amka na BBC, wasikilizaji wa Kenya watakuwa wakipokea matangazo ya Dira ya Dunia pamoja na Leo Afrika yanayohama kutoka London, Uingereza.

"Kimsingi Idhaa ya Kiswahili itakuwa imetua nyumbani na kukamilisha safari ndefu ya zaidi ya maili 4,000 na miaka 57 tangu ilipozinduliwa jijini London, wakati huo kuhudumia miliki za Kikoloni. Idhaa ya Kiswahili ilisikika hewani kwa mara ya kwanza Juni 27, 1957," alisema.

Mugera alisema uzinduzi huo ulifanyika wakati nchi zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara zikipigania uhuru. Ulikuwa mwaka wa mabadiliko makubwa ya kisiasa.

Ghana ilikuwa ya kwanza katika eneo hilo kujinyakulia uhuru wake na kuharakisha mchakato huo katika maeneo mengine. Idhaa ya Kiswahili ya BBC ilikuwa mstari wa mbele kuripoti harakati za ukombozi na sherehe za uhuru Tanzania (wakati huo Tanganyika), Uganda, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Rwanda na Burundi. Uhodari wa idhaa hii kuripoti kwa kina na kutangaza, umedhihirika wakati wa matukio mbalimbali, yakiwamo ya mashambulio ya mabomu katika balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania Agosti 1998.

Vita ya Kagera
"Kabla ya hapo, nani atasahau vita vya mwaka 1979 kati ya Tanzania na Uganda? Hapo ndipo Iddi Amin alipojaribu kuvamia Tanzania akipania kunyakua sehemu ya ardhi yake. Ugomvi kati ya Amin na Rais wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ulimalizika kwa mtutu wa bunduki. Wanajeshi wa Uganda walizidiwa nguvu, Amin akakimbilia uhamishoni, akianzia Libya na hatimaye Saudi Arabia hadi alipofariki dunia.

"Bila shaka hilo lilikuwa tukio kubwa katika historia na siasa, siyo tu ya Afrika Mashariki bali ya dunia nzima. Ni kwa sababu hiyo, Idhaa ya Kiswahili iliwakutanisha watoto wa kiume wa marais wawili (Mwalimu Nyerere na Amin) kwa mara ya kwanza tangu mzozo wa mwaka 1979," alisema.

Safari ya mtoto wa Amin
"Mtoto wa Amin, Jaffar, alisafiri takriban kilomita 500 kutoka Arua, Kaskazini mwa Uganda kukutana na mtoto wa Nyerere, Madaraka, anayeishi Butiama. Walikumbatiana huku wakazi wa Butiama wakishangilia," alisimulia.

Mugera alisema Idhaa ya Kiswahili inajulikana kwa ustadi wake katika kufuatilia na kufichua ukweli wa mambo. Mwaka wa 2008 ulighubikwa na matukio mengi ya mashambulio ya kikatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini (albino), baadhi yao waliuawa.

Kwa mara ya kwanza katika matukio hayo, mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Vicky Ntetema aliwasaka waganga wa kienyeji walioahidi kumpa damu ya albino, nywele, miguu na viganja kwa Dola 2,000 za Marekani. Walidai viungo hivyo vinaweza kutumika kutengeneza dawa ya kuwapa watu utajiri.

Habari hiyo ilisambaa sehemu mbalimbali duniani na kuzua hamasa kuhusu hatima ya albino. Serikali ya Tanzania ilianzisha uchunguzi na polisi wakaamuriwa kuchukua hatua za kuwasaka, kuwakamata na kuwafungulia mashtaka washukiwa. Tangu wakati huo mauaji ya albino yalipungua.

Ni wazi kwamba ukitaka kumhudumia vyema mteja wako, lazima ufahamu vizuri mahitaji yake. Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2010, Idhaa ya Kiswahili ya BBC ilifahamu kwamba wasikilizaji wake walikuwa na tamaa ya kupata taarifa na jukwaa la kujadiliana.

Kwa kushirikiana na Radio One, pamoja na Radio Free Africa (RFA), Idhaa ya Kiswahili ya BBC iliandaa matangazo maalumu kwa saa 14 kila siku kwa muda wa wiki moja kutoa taarifa, uchambuzi na kuandaa farashani kwa wasikilizaji wa Tanzania na duniani kote. Pia katika kipindi cha miaka 20, kumekuwapo wahariri wanne katika idhaa hiyo, kuanzia Kari Blackburn, Tido Mhando, Solomon Mugera na Ali Saleh. Haupiti mwaka bila kufanya jambo kubwa na la kusisimua.

"Idhaa ilikuwa ya kwanza kuhamisha baadhi ya huduma kwenye eneo la utangazaji mwaka 2006. Sherehe za miaka 50 ya Idhaa ya Kiswahili ‘zilipeperushwa' kwa redio na televisheni kutoka Dar es Salaam," alisema Mugera.


CHANZO:
Mwananchi
 
nashukuru kama yatarushiwa tanzania,nilidhani wangeendelea kuisujudia "Nairobi"
 
Mkuu,studio iliyojengwa KIbaha, mkoani Pwani, ni moja ya studio za BBC, kama ile iliyoko Nairobi, lakini studio kuu ya kurushia matangazo itabakia kuwa London. Upo?

BBC yazindua ofisi mpya Dar es Salaam

140811162415_bbc_studio_512x288_bbc_nocredit.jpg


Wafanyakazi wa BBC wakiwa kazini kupeperusha matangazo ya Dira ya Dunia redio

Idhaa ya kiswahili ya BBC imezindua rasmi studio zake mjini Dar es Salaam kwa mbwembwe na haiba kuu.

Uzinduzi huo ni matokeo ya mkakati na uwekezaji wa miaka mingi wa shirika la BBC duniani kuhakikisha kuwa matangazo yake yanawafikia wasikilizaji katika hali ya ubora wa hali ya juu na ya kisasa zaidi.

Katika hafla hiyo iliyoandaliwa katika ofisi hizo hizo mpya zilizoko eneo la Mikocheni, mkuu wa kitengo cha uandishi wa habari katika BBC, Nicki Clarke, ameshukuru serikali ya Tanzania, kwa kuwaruhusu kujenga studio hizo za kisasa zitakazoinua tasnia ya habari nchini humo na uhuru wa habari kwa ujumla.
Naye mkuu wa ofizi ya Dar es Salaam, Hassan Mhelela mbali na kuwataka wafanyakazi wa BBC Tanzania, kuzidi kuonyesha ushirikiano pamoja na utendaji kazi wa pamoja, pia ametangaza kuanishwa rasmi kwa ushirikiano kati ya BBC na chuo kikuu cha Dar es Salaam kitengo cha uandishi wa habari.
140811170116_nampesia_512x288_bbc_nocredit.jpg


Eric David Nampesya akizipa taabu Tumba kwenye sherehe ya ufunguzi wa ofisi za BBC Dar es Salaam

Ushirikiano huo amesema kuwa unalenga kusaidia kutoa mafunzo kwa wandishi wa habari chipukizi walioko mafunzoni katika chuo hicho, ambao kwa nyakati tofauti, watakuwa wakijiunga na BBC ili kupata mafunzo katika uandaaji vipindi vya redio na televisheni pamoja na utangazaji.

Kwa upande wa BBC, kuanzishwa kwa ofisi hii, yenye studio za kisasa kabisa za redio na televisheni mbali na kuongeza ubora wa vipindi lakini pia kutawezesha matangazo ya redio na televisheni kufanyika moja kwa moja kutokea Dar es Salaam.
Na kuanzia sasa matangazo ya Amka na BBC yatakuwa yakiandaliwa Dar es Salaam.
Itakumbukwa kuwa Tanzania mbali na kuwa na wasikilizaji wengi wa idhaa ya kiswahili ya BBC, lakini pia ndiko kunakozungumzwa zaidi lugha ya kiswahili.
Tanzania pia ina rekodi ambapo mtangazaji wa kwanza au sauti ya kwanza iliyosikika mwaka 1957, ilikuwa ya mtanzania Oscar Kambona ambapo alikuwa mwanafunzi mjini London.

CHANZO: BBC
 
Kwa mara ya kwanza kituo cha BBC ambacho kinarusha vipindi vyake moja kwa moja London toka mwaka 1957 hadi sasa hivi wakati naandika uzi, kwa sasa matangazo yatakuwa yanarushwa dsm Tnzania kwa mara ya kwanza, wandugu mnaonaje,je kiswahili kinakuwa au kinatupwa

Imekaa vizuri lakini si walishaanza kenya siku nyingi au!
Kwa Tanzania imechelewa sana, kwani ndiyo chimbuko la kiswahili. Lakini walipapuuza wakaenda Kenya ambako siyo chimbuko la Kiswahili. Hata hivyo tunashukuru
 
Ni kwamba wamegawa.
Dira ya Dunia; yaani matangazo ya Jioni, yatarushwa kutokea Nairobi.
Amka na BBC; yaani matangazo ya asubuhi, yatarushwa kutokea Studio za Dsm.
Dira ya Dunia Tv imebaki London
 
nashukuru kama yatarushiwa tanzania,nilidhani wangeendelea kuisujudia "Nairobi"

NAIROBI YATARUSHIWA HUKO HUKO TU.POLE!!!!!!!!!!!!!!!
MUGERA: BBC Swahili’s East Africa homecoming

Posted Monday, August 11 2014 at 11:21
In Summary

  • BBC Swahili’s $1m state-of-the-art broadcasting facilities will be officially inaugurated in Dar es Salaam today
It is now official. The entire BBC Swahili service radio programming and production team will be based in East Africa.

This is truly a homecoming for one of the BBC’s most loved and successful language broadcasting services.

BBC Swahili’s $1m state-of-the-art broadcasting facilities will be officially inaugurated in the Tanzania’s commercial capital, Dar es Salaam, today.


It is from here that the flagship breakfast show, Amka na BBC, will be produced. The afternoon show ‘Dira ya Dunia’ and the late evening ‘Leo Afrika’ move from London to Nairobi.
 
Imekaa vizuri lakini si walishaanza kenya siku nyingi au!
Kwa Tanzania imechelewa sana, kwani ndiyo chimbuko la kiswahili. Lakini walipapuuza wakaenda Kenya ambako siyo chimbuko la Kiswahili. Hata hivyo tunashukuru

Lakini ndugu kuna msemo kuwa 'mwenye afya hamuhitaji daktari' unaufahamu?
 
Wakaribie ila wajipambanue na redio za kibongo ambazo zimekaa kiitikadi, kiimani na kimtazamo. Na ningewashauri wasijaze watangazaji wengi wa kibongo watawaharibia kazi maana akili zao ziko kinazi sana.
 
Ni kwamba wamegawa.
Dira ya Dunia; yaani matangazo ya Jioni, yatarushwa kutokea Nairobi.
Amka na BBC; yaani matangazo ya asubuhi, yatarushwa kutokea Studio za Dsm.
Dira ya Dunia Tv imebaki London

online service, dira ya dunia na leo afrika sio london ni nairobi!!!!!!!

It is from here that the flagship breakfast show, Amka na BBC, will be produced. The afternoon show 'Dira ya Dunia' and the late evening ‘Leo Afrika' move from London to Nairobi.
 
wasije wakatumika tuu ,maana radio za hapa tz nying zina unazi,bora wangebak nairob
 
Kwahiyo Mwalekwa na kayanda watarudi tz? Wamekaa londoni kwa mda mchache sana!
 
Kwahiyo Mwalekwa na kayanda watarudi tz? Wamekaa londoni kwa mda mchache sana!

Nina wasiwasi BBC wasipokuwa makini itageuka kuwa clouds2 maana naona hizi ni products za pale!! full unazi wa chama chetu!
 
Mkuu,studio iliyojengwa KIbaha, mkoani Pwani, ni moja ya studio za BBC, kama ile iliyoko Nairobi, lakini studio kuu ya kurushia matangazo itabakia kuwa London. Upo?
wamejenga studio kibaha maeneo gani? maana tulishazoea studio kuwa dsm, basi watakuwa watofauti aisee.
 
Back
Top Bottom