BBC Swahili yafungua ofisi za kisasa nchini

Hao BBC ni wanafiki wakubwa.
Wanachagua kipi watangaze na kipi watie kapuni.

Wabaguzi sana hawa. Bado ukoloni umejaa kila kona ndani ya BBC.

Uchafu mtupu. Bora RTD yetu mara milioni.
 
Picha juu inamuonyesha moja ya Kiongozi mkubwa wa Vyama vya Upinzani Nchini Bw.Lipumba akishangaa na kufurahia kufunguliwa kwa Kituo cha Kurushia Matangazo cha Serikali ya Uingereza, BBC hapa nchini!

Akiwa kama kiongozi mwenye nia ya kuleta mabadiliko alipaswa awe wa kwanza KUPINGA kufunguliwa kwa kituo hicho Hapa nchini na badala yake kupigania TBC kupewa umuhimu na kuwezeshwa!

Kwa mtu mwenye akili na uwezo (wa kawaida) wa kufikiri atatambua kwamba BBC inaendeshwa na Serikali ya Uingereza na ipo kwa ajili ya Maslahi ya Serikali ya Nchi hiyo, hivyo kufunguliwa kwa hiyo studio hapa kuna lengo hilo hilo, na ndio maana nchi zenye Watu na Viongozi wenye akili huwa wanapigania kuwa na Vituo vyao na kuviendeleza!

Sasa hii maana yake ni nini? Ni kwamba Vyanzo vikubwa vya Habari tutakazokuwa tunazipata zitakuwa ni Habari zilizochujwa na kupikwa na Watu wa BBC (Serikali ya Uingereza) ili zikidhi matakwa yao, hivyo kwangu mimi kwa Kiongozi ambaye anasema anataka kukomboa TZ kwenda kufurahia kufunguliwa kwa kituo kama hicho, Ni Bora CCM wabaki kwani tayari nawajua kwamba ni Majambazi!

kuna tofauti kubwa kati ya mtu Bright na Clever. usilolijua Lipumba ni bright ila sio clever kwa hiyo kukurupuka ni kawaida yake.
 
Agosti 11 2014. BBC Idhaa ya Ulimwengu, imezindua ofisi zake jijini Dar es Salaam. Ofisi za Dar es Salaam zina studio ambazo zinatumika kuandaa matangazo maarufu ya redio ya asubuhi, Amka na BBC, na pia kuendesha tovuti ya bbcswahili.com. Katika kuadhimisha uzinduzi huo, vipindi vingine viwili vya BBC Idhaa ya Kiswahili, Dira ya Dunia ya redio na ya TV vitaandaliwa kutoka Dar es Salaam katika siku hiyo ya Jumatatu Agosti 11.

Ufunguzi wa ofisi za Dar es Salaam ni matokeo ya mikakati ya BBC Idhaa ya Ulimwengu ya kuhamisha uandaaji wa vipindi vya redio na tovuti kutoka London kwenda Afrika Mashariki. Ofisi mpya ina vifaa vya kisasa vinavyoweza kutayarisha vipindi vya redio, TV na huduma za habari kwa njia ya simu za mkononi.

Amka na BBC, kipindi cha nusu saa ambacho hutangazwa Jumatatu hadi Ijumaa humulika matukio na taarifa zitakazojiri katika siku, sasa kitaandaliwa Dar es Salaam na watayarishaji na watangazaji 15. Ofisi mpya pia zina watayarishaji wanaoandaa taarifa mbalimbali za kanda ya Afrika Mashariki na Kati kwa ajili ya vipindi vya TV vya Focus on Africa na Dira ya Dunia.

Mkuu wa Habari wa BBC Idhaa ya Ulimwengu Nikki Clarke amesema: "Uzinduzi wa ofisi zetu za Dar es Salaam ni hatua kubwa katika safari yetu iliyoanza muda mrefu kidogo, katika kuwapa wanachotaka wasikilizaji katika nchi zinazozungumza Kiswahili, na ambao husikiliza BBC wanapotaka kupata taarifa wanazoziamini na zenye uhakika. Takriban watu milioni 12.4 - ambao ni kama nusu ya idadi ya watu wazima nchini Tanzania, husikiliza matangazo ya redio ya BBC kila wiki. Na sasa moja ya kipindi maarufu cha BBC, Amka na BBC, kimekuja karibu zaidi na wasikilizaji."

Ofisi ya Dar es Salaam, ina studio mbili za redio ambazo zinaweza kutumika na hadi watu sita kwa wakati mmoja, na hivyo ni muafaka kabisa kwa kipindi kichangamfu cha Amka na BBC kwa ajili ya mijadala na mahojiano ya kuvutia.

Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Ali Saleh anasema : "Ofisi mpya zinatoa nafasi bora kabisa kwa watayarishaji wa BBC nchini Tanzania kuimarisha ukusanyaji wa habari na kutoa taarifa kutoka katika eneo la Afrika Mashariki na Kati. Amka na BBC itakuwa na uwezo mkubwa zaidi kutoa taarifa na habari mchanganyiko, za Afrika Mashariki na pia za dunia, pamoja na mahojiano ya moja kwa moja na watu mbalimbali, lakini pia makala na habari za kijamii."

Idhaa ya Kiswahili ya BBC imekuwa kitovu cha hatua ya BBC Idhaa ya Ulimwengu ya kuimarisha kuwepo kwake katika sekta ya habari barani Afrika. Baada ya ufunguzi wa ofisi ya Nairobi mwaka 1998, BBC Idhaa ya Ulimwengu ilikuwa shirika la kwanza la habari la kimataifa kuwa na kituo cha uandaaji habari barani Afrika. Mwaka 2006 Amka na BBC ilihamishwa kutoka London kwenda Nairobi, na BBC Idhaa ya Ulimwengu, kwa mara nyingine tena ikawa shirika la kwanza la kimataifa la habari kuandaa na kutangaza vipindi kutoka barani Afrika. Katika hatua ya kuhamisha utayarisaji wa vipindi na taarifa za kwenye tovuti, kipindi maarufu cha jioni cha redio, Dira ya Dunia sasa kinatayarishwa Nairobi
 
Agosti 11 2014. BBC Idhaa ya Ulimwengu, imezindua ofisi zake jijini Dar es Salaam. Ofisi za Dar es Salaam zina studio ambazo zinatumika kuandaa matangazo maarufu ya redio ya asubuhi, Amka na BBC, na pia kuendesha tovuti ya bbcswahili.com. Katika kuadhimisha uzinduzi huo, vipindi vingine viwili vya BBC Idhaa ya Kiswahili, Dira ya Dunia ya redio na ya TV vitaandaliwa kutoka Dar es Salaam katika siku hiyo ya Jumatatu Agosti 11.

Ufunguzi wa ofisi za Dar es Salaam ni matokeo ya mikakati ya BBC Idhaa ya Ulimwengu ya kuhamisha uandaaji wa vipindi vya redio na tovuti kutoka London kwenda Afrika Mashariki. Ofisi mpya ina vifaa vya kisasa vinavyoweza kutayarisha vipindi vya redio, TV na huduma za habari kwa njia ya simu za mkononi.

Amka na BBC, kipindi cha nusu saa ambacho hutangazwa Jumatatu hadi Ijumaa humulika matukio na taarifa zitakazojiri katika siku, sasa kitaandaliwa Dar es Salaam na watayarishaji na watangazaji 15. Ofisi mpya pia zina watayarishaji wanaoandaa taarifa mbalimbali za kanda ya Afrika Mashariki na Kati kwa ajili ya vipindi vya TV vya Focus on Africa na Dira ya Dunia.

Mkuu wa Habari wa BBC Idhaa ya Ulimwengu Nikki Clarke amesema: "Uzinduzi wa ofisi zetu za Dar es Salaam ni hatua kubwa katika safari yetu iliyoanza muda mrefu kidogo, katika kuwapa wanachotaka wasikilizaji katika nchi zinazozungumza Kiswahili, na ambao husikiliza BBC wanapotaka kupata taarifa wanazoziamini na zenye uhakika. Takriban watu milioni 12.4 - ambao ni kama nusu ya idadi ya watu wazima nchini Tanzania, husikiliza matangazo ya redio ya BBC kila wiki. Na sasa moja ya kipindi maarufu cha BBC, Amka na BBC, kimekuja karibu zaidi na wasikilizaji."

Ofisi ya Dar es Salaam, ina studio mbili za redio ambazo zinaweza kutumika na hadi watu sita kwa wakati mmoja, na hivyo ni muafaka kabisa kwa kipindi kichangamfu cha Amka na BBC kwa ajili ya mijadala na mahojiano ya kuvutia.

Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Ali Saleh anasema : "Ofisi mpya zinatoa nafasi bora kabisa kwa watayarishaji wa BBC nchini Tanzania kuimarisha ukusanyaji wa habari na kutoa taarifa kutoka katika eneo la Afrika Mashariki na Kati. Amka na BBC itakuwa na uwezo mkubwa zaidi kutoa taarifa na habari mchanganyiko, za Afrika Mashariki na pia za dunia, pamoja na mahojiano ya moja kwa moja na watu mbalimbali, lakini pia makala na habari za kijamii."

Idhaa ya Kiswahili ya BBC imekuwa kitovu cha hatua ya BBC Idhaa ya Ulimwengu ya kuimarisha kuwepo kwake katika sekta ya habari barani Afrika. Baada ya ufunguzi wa ofisi ya Nairobi mwaka 1998, BBC Idhaa ya Ulimwengu ilikuwa shirika la kwanza la habari la kimataifa kuwa na kituo cha uandaaji habari barani Afrika. Mwaka 2006 Amka na BBC ilihamishwa kutoka London kwenda Nairobi, na BBC Idhaa ya Ulimwengu, kwa mara nyingine tena ikawa shirika la kwanza la kimataifa la habari kuandaa na kutangaza vipindi kutoka barani Afrika. Katika hatua ya kuhamisha utayarisaji wa vipindi na taarifa za kwenye tovuti, kipindi maarufu cha jioni cha redio, Dira ya Dunia sasa kinatayarishwa Nairobi.
 
Huu uandishi ni wa mtu mkubwa sana hapo mjengoni. Sio kama kibonde.
 
Kule Nairobi kulikuwa na studio gani tena??
 
Mayb wanataka wahame toka Nairobaa kabsa kuja Dar coz ya Al- Shaabab
 
Picha juu inamuonyesha moja ya Kiongozi mkubwa wa Vyama vya Upinzani Nchini Bw.Lipumba akishangaa na kufurahia kufunguliwa kwa Kituo cha Kurushia Matangazo cha Serikali ya Uingereza, BBC hapa nchini!

Akiwa kama kiongozi mwenye nia ya kuleta mabadiliko alipaswa awe wa kwanza KUPINGA kufunguliwa kwa kituo hicho Hapa nchini na badala yake kupigania TBC kupewa umuhimu na kuwezeshwa!

Kwa mtu mwenye akili na uwezo (wa kawaida) wa kufikiri atatambua kwamba BBC inaendeshwa na Serikali ya Uingereza na ipo kwa ajili ya Maslahi ya Serikali ya Nchi hiyo, hivyo kufunguliwa kwa hiyo studio hapa kuna lengo hilo hilo, na ndio maana nchi zenye Watu na Viongozi wenye akili huwa wanapigania kuwa na Vituo vyao na kuviendeleza!

Sasa hii maana yake ni nini? Ni kwamba Vyanzo vikubwa vya Habari tutakazokuwa tunazipata zitakuwa ni Habari zilizochujwa na kupikwa na Watu wa BBC (Serikali ya Uingereza) ili zikidhi matakwa yao, hivyo kwangu mimi kwa Kiongozi ambaye anasema anataka kukomboa TZ kwenda kufurahia kufunguliwa kwa kituo kama hicho, Ni Bora CCM wabaki kwani tayari nawajua kwamba ni Majambazi!

Kwani umemuona lipumba peke yake. Au unawashiwa na ukawa. . Huu sio muda wa yeye kupigia kelele TBC. Maana anajua ni radio ya chama tawala (rejea kuondoka kwa tido muhando. ) je ukweli na uhakika upon?. Hivi vitu haviongozwi kwa utashi wa kisiasa. Vinaongozwa na standard
eg. ITU. Tcra, IEEE .

Usikimbilie kuzuia BBC kataa kwanza misaada, kisha ndio usimame.

Kwa taarifa yako wengi tu wapo njiani kuja bongo.
Eg. RFI, „RCI, VOA, DW
 
Kule Nairobi kulikuwa na studio gani tena??

BBC walifungua bureau yao ya kwanza Nrb mwaka 1998, so itakua pale tu haiendi popote. Ila kipindi chake cha asubuhi, Amka na BBC watakihamisha na kukipeleka Dar na cha afternoon kitakua Nairobi. Lakini website yao bbcswahili.com itashughulikiwa na nchi zote mbili.
 
Umeshaambiwa Dar es Salaam, acha ligi
 
Ndiyo mwisho wa BBC kuwa na redio washirika au wataendelea na utaratibu wa kawaida?
 
Regina mwalekwa na mwenzie Hawajawahi kwenda London siku zote huwa wanatangaza wakiwa hapa hapa Dar, kwenye ofisi zao zilizoko Tangaza house mikocheni King Kong III
 
Last edited by a moderator:
Nawashangaa Mnaoshabikia Hizi Idhaa Za MABEBERU Hawa Huwa Wanatangaza HABARI MBAYA TU ZA AFRICA LAKINI ZA KWAO WANAZIWEKA KWAPANI HATUZISIKII Wamekalia KILA WAKATI KUMSEMA VIBAYA MUGABE Na Wakati Kile KIBIBI CHAO WANAKIACHA. Pia Huwa Sifurahi Radio Zetu Kutoa Airtime Kwa Hizi Idhaa Za Kishetani Bado UKOLONI MAMBO LEO UNATUSUMBUA.
 
Je, wanajua kwamba huku walikohamia watangazaji wanaoeleza ukweli kucha zao huwa hatarini?
 
Wanatakiwa wasiwe biased. Na wakiwa hivyo basi BBC itatupwa kwenye kapu moja na TBC
 
Back
Top Bottom