Napenda mnavyojiliwaza ila ndio ukweli wenyewe, Uganda kaweka UPDF kabisa mpakani, hamna tena kuingia kwao kinyemela, utachezea vichura hadi ukome, ukifika hapo mpakani panua mdomo hadi jino la mwisho, kisha kifaa cha kupima corona kitumbukizwe humo, ukipita huo mtihani ndio uruhusiwe kuingia kwenye taifa la Abaganda.
Kwanza hawa wanalazimisha hata baina ya ndugu, bora sisi kiaina tunafumba macho kwa watu mpakani haswa wale tunaochangia makabila kwa mfano Wadigo, Wamaasai n.k.