BBC: Wanajeshi waliouawa ni kutoka Afrika Kusini, Malawi na Tanzania. Hao Watanzania mbona hatuambiwi na mmefanya kimya?

Siku za kwanza walivamia kambi ya Tanzania ili kuwazuia kujitokeza na kuwa kikwazo kwao ndipo wakaendelea na kuvamia kambi zingine hususani zile zilizopo jirani na migodi ya madini
 
..SADC wametoa pole kwa South Africa, Malawi, na Tanzania, kwa kupoteza askari.

..Taarifa Rasmi ya kikao cha Maraisi wa SADC ndio imetoa rambirambi hizo.

..Je, SADC nao wamekosea?
Siri imevuja sasa, wao walificha lakini salam ya pole imewaumbua na chadema watapita na hiyo pole kubaini ukweli halisia
 
Mama amwachie jk uamirijeshimkuu kwa siku 2 tu ili akamshikishe adabu kagame ili kongo kutulie
 
Protocol hairuhusu.
 
Our CIC, samia is weak, she is easily intimidated, kama anatishwa na maneno ya Lisu, Ndugai, akipigwa mkwara na Kagame, ni mishuzi tu, CDF wetu,na yeye ni mwendo wa porojo, mipasho kama machawa wa ccm, ukiona wanaficha taarifa,ujue majanga ni makubwa!
 
Ili Rwanda ipate akili, itapasa uwanja wa vita uhamie katika ardhi ya nchi yao wenyewe. Kuikalia kimya chokochoko zake katika ardhi ya DRC ni jambo ambalo halikubaliki hata kidogo.
 
..SADC wametoa pole kwa South Africa, Malawi, na Tanzania, kwa kupoteza askari.

..Taarifa Rasmi ya kikao cha Maraisi wa SADC ndio imetoa rambirambi hizo.

..Je, SADC nao wamekosea?
Tanzania wanaogopa kutangaza wanajeshi wao wamepigwa na M23 maana huwa hakuna mahusiano mazuri kati ya polisi wa Tanzania na wananchi wanaodai haki zao.
 
Nimeiona hiyo, Afrika kusini imewekwa wazi. Tanzania inafanya siri aidha inaogopa kutoa tamko kali kumuuudhi Kagame au haiwajali wanajeshi wake kivile hata kama wameuwawa.
Tanzania imewahi kupeleka walinda amani nchi nyingi na haikuwahi kutangazwa idadi kamili ya waliokufa vitani.
Nchi karibu zote ndiyo hivyo hutaja wachache au hawataji kabisa kwa sababu fulani za kiusalama na mbinu za kivita.
 
Ifike hatua ile vita ufanyike umafia mkubwa ndo itaisha hivi kutafuna unaacha wanajijenga tena, unatafuna unaacha litakuja kuwa sugu lisilotibika lisambae!
Umafia upi? Mtawauwa wale Watusi (Banyamulenge) au itakuaje?
 
Kila nchi ina utaratibu wake kwenye masula ya ulinzi. Usilazimishe tufanane. Kwenye masuala ya ulinzi si sawa na masuala ya kijamii. Taarifa za jeshi si za kuzagaa kwenye mitandao. Kaa kwa kutuli kwani kukiwa na ulazima wa kuambiwa utaambiwa kama haupo tulia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…