Ruto hana wapiga kura wa kutosha ni.mpaka kuwe na coalition ya kikanda.
Yaani kama hatakaa sahani moja.na kina Jumwa na kina Balala kutoka Pwani na Lamu, akina Mudavadi kutokea hapa kati kusini, lakini pia apate someone kutokea kisii kuja Migori hawezi kushinda.
Ruto hawezi pata kitu nyanza kabisa bila Raila pia
Central ampate Kalonzo Musyoka labda
Wakalenjin ni kabila kubwa, kumbuka chaguzi mbili zilizopita kolabo ya Wakalenjin na Wakikuyu ilikuwa na 45% ya Wapiga kura. Kwa sasa kinachowasumbua wakongwe ni namna gani ya kumtenganisha Ruto na wapiga kura wa Mount Kenya, Wakikuyu. Mpaka sasa hilo halijafanikiwa ukizingatia kuwa kwa Wakikuyu Raila hakubaliki kabisa, historically kuanzia enzi za Baba yake, Jaramogi.
Kwa sasa Wakikuyu wamegawanyika huku wengi wakiwa wamestick na Ruto ukizingatia uadui na mapigano makubwa ya Wakikuyu na Wakalenjin mwaka 2007 yaliyopelekea Kenyatta na Ruto kwenda ICC, muungano wa Uhuru na Ruto uliyaleta makundi haya mawili pamoja na kufuata makavu ya uadui wa miaka mingi, ikumbukwe, Wakikuyu wengi wanaishi eneo la Rift Valley, nyumbani kwa Wakalenjin.Hali ikibaki ilivyo sasa, Ruto ana nafasi kubwa ya kushinda.
Upande wa Pwani Balala na Jumwa hawana ushawishi kwa sasa, Raila wakati wote amekuwa na nguvu Pwani, japo Ruto huko atapigania tu wala 30%.
Wakisii bado hawajawa na nguvu kwenye siasa za Kenya.
Ruto kubwa analohitaji ni:
1. Ahakikishe anabaki na Wakikuyu, kwa kuchagua Mkikuyu atakayeonekana kama mrithi wa Uhuru kwenye Umakamu au sasa Uwaziri Mkuu. Uchaguzi ukiwa Ruto na Raila Wakikuyu watamchagua Ruto.
2. Ahakikishe anapata nguvu upande wa Magharibi, Waluhya, hawa ni kundi muhimu kwenye uchaguzi, au walau alete ushindani mkubwa.
3. Kwa kuwa Raila amekosana na Kalonzo Musyoka na amekuwa karibu sasa na maadui zake, ajenge ushirikiano na Kalonzo kumhakikishia kupata kuwa za Wakamba, Eastern.
Akifanikiwa haya, urais ni wa kwake.