ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 937



Kuna wakati niliwahi kuwaleta hapa taarifa kuhusu ubovu wa baadhi ya bidhaa zinazouzwa katika maduka makubwa ya bidhaa (supermarkets) zinazomilikiwa na "wakoloni" nchini hasa zile za vyakula.
Jana jioni (tarehe 20.03.2011) nilipitia pale Shoprite Mlimani City, moja ya mambo niliyoweza kushuhudia katika harakati zangu ni kukuta baadhi ya bidhaa za matunda zikiwemo "appels" picha zikiwa zimewekwa kwenye makabati ya kuuzia bidhaa (shelves) ili hali muda wake wa kuuzwa umekwisha (expired).
Hayo ma "appels" yalipaswa kuwa yameuzwa kabla ya tarehe 12.03.2011 lakini cha kusikitisha, bado yamefungwa na vifungashio vyake kuonyesha bei na lini yalipaswa kuuzwa, inaonekana manajimenti ya duka hilo kubwa hapa nchini kama halina nia ya kujitegenezea faida kwa stahili ya kuuza bidhaa zisizofaa basi haipo makini katika kuhakiki bidhaa dukani.
Katika jitihada za kujaribu kuwafahamisha wadau yale ambayo "wawekezaji" wanatufanyia hapa nchini, niliamua kununua furushi moja kwa Tshs. 6,500 na baada ya kufungua, nakutana na moja ya tunda katika furushi hilo likiwa tayari limeoza (kama mnavyoweza kuona pichani).
Bidhaa hizi na nyingine ambazo hazina muda wa kutumika katika vifungashio bado mpaka tarehe ya leo (21.03.2011) zipo kwenye makabati ya kuuzia vitu pale Shoprite (kama mtu akiweza kupita hapo achungulie)! Kama upo makini, ukienda kununua, ukishtukia "expiry date" wanachokifanya ni kukubadilishia tu (haijulikani hata yale wanayokubalishia yaliingia lini nchini kutoka huko Afrika ya Kusini yanakozalishwa).
Kwa utaratibu huu, pengine tunaweza kuamini, vyombo vyetu vyenye dhamana na afya ya walaji kama TFDA havina uwezo wowote wa kupita kwenye maduka ya wawekezaji wakubwa na kuachukulia hatua stahili.
Cha msingi ni watanzania wenyewe tuwe makini na haya mambo ya bidhaa toka nje hasa za "supermakerts". zinatumaliza kimya kimya.