Behewa 44 za mizigo kuwasili nchini

Behewa 44 za mizigo kuwasili nchini

Tanzania Railways Corp

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2018
Posts
251
Reaction score
595
Picha tofauti zikionesha Behewa mpya 44 za Mizigo zilizonunuliwa na Shirika la Reli Tanzania - TRC kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Reli ya Kati - TIRP zilipokuwa bandarini nchini China kabla ya kuanza safari kuja Tanzania. Meli yenye jina 'Kaley and IMO' iliyobeba Behewa hizo ilianza safari hivi karibuni mwezi Agosti na inatarajiwa kufika nchini mwishoni mwa mwezi Septemba 2021.

TIRP 5.jpg
Wagon 2.jpg
Wagon 1.jpg
78c344bdb12890b529b06c756784fec.jpg
189df3d6ccd11f45035b0adeab2ee08.jpg
a6bbe0a72039359b0dcbbaa6501aaf7.jpg
fd11e9303c3fafe24b58ebfabeab7dd.jpg
 
Tanzania Railways Corp ,

..Ujenzi wa sgr, awamu ya 3, kipande cha Makutopora -- Tabora-- Isaka, utaanza lini?

..Kwanini ujenzi wa Isaka--Mwanza, awamu ya 4, umetangulia ujenzi wa kipande nilichokitaja hapo juu?

..Mantiki ya kujenga awamu ya 3 kwanza ni kufikisha sgr ktk bandari kavu ya Isaka ili sgr ianze kutumika kwa mizigo mapema zaidi.
 
Zile nzee za mizigo zilizokuwepo vipi bado zipo, hizi tunaongezea ?

Nauliza tu tusije zipeleka vyuma chakavu kumbe huenda zinaweza fanyiwa maintenance (ukizingatia ni mizigo)..., nimeona niulize sababu haya mambo na hizi tozo nyingi tusije ambiwa imeongezeka tena kununulia mabehewa..,

By the way vile vichwa vya Treni bandarini viliishia wapi ?
 
Picha tofauti zikionesha Behewa mpya 44 za Mizigo zilizonunuliwa na Shirika la Reli Tanzania - TRC kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Reli ya Kati - TIRP zilipokuwa bandarini nchini China kabla ya kuanza safari kuja Tanzania. Meli yenye jina 'Kaley and IMO' iliyobeba Behewa hizo ilianza safari hivi karibuni mwezi Agosti na inatarajiwa kufika nchini mwishoni mwa mwezi Septemba 2021.

View attachment 1904981View attachment 1904983View attachment 1904985View attachment 1904986View attachment 1904987View attachment 1904988View attachment 1904989
Vile vichwa mlivyookota bandarini viko wapi,au mmepaki chato
 
Hayo mabehewa yana mwenyewe maana hamshindwi kusema mmeokota bandarini.
 
Mdogo mdogo tu mpaka tutafika Inshallah.ingawa maadui wa ndani na wa nje hawapendi haya mambo mazuri kwa nchi yetu.
 
Halafu za zamani badala ya kuzifanyia ukarabati nyie mnaenda
Kukata scraper, why?!
 
Back
Top Bottom