Behewa za kisasa za reli ya SGR zimewasili

Behewa za kisasa za reli ya SGR zimewasili

Mnada wa Mhunze

Senior Member
Joined
Mar 1, 2023
Posts
168
Reaction score
819

Ni behewa za kisasa na zenye mwonekano wa kupendeza zinazotarajiwa kuanza kubeba abiria mapema mwezi ujao kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro.

Ni ndoto iliyootwa na ndugu hayati Magufuli na sasa rasmi inaenda kuanza kutimilika hivi karibuni.

Hongera hayati Magufuli na hongera Rais Samia.

Soma pia: Uzi mkuu unaoonesha yaliyojiri kwenye mradi wa SGR tangu kuanza kwake mpaka mradi ulipofikia hivi sasa

View attachment 2648228
Ni behewa za kisasa na zenye mwonekano wa kupendeza zinazotarajiwa kuanza kubeba abiria mapema mwezi ujao kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro.

Ni ndoto iliyootwa na ndugu hayati Magufuli na sasa rasmi inaenda kuanza kutimilika hivi karibuni.

Hongera hayati Magufuli na hongera Rais Samia.
Tutaibifsisha hii SGR

USSR

Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app
 
View attachment 2648228
Ni behewa za kisasa na zenye mwonekano wa kupendeza zinazotarajiwa kuanza kubeba abiria mapema mwezi ujao kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro.

Ni ndoto iliyootwa na ndugu hayati Magufuli na sasa rasmi inaenda kuanza kutimilika hivi karibuni.

Hongera hayati Magufuli na hongera Rais Samia.
Hata iweje hakuna treni ya itaanza safari mwezi ujao kwenda Moro. Halafu yale mabasi mekundu mapya yaende wapi?
 
Kwa muonekano kweli vipo classic.. Ila Sasa tusubirie hujuma au ugaigai .. kutoka kwa wasafirishaji wa mabasi...

Wana chosahau mi kuwa usafiri wa mabasi huwa una pungua matumizi kadri teknoljia inavyokua...
Wakati Tz hakuna hata kituo kimoja cha TV, ilidhaniwa mpira mpira ukanyeshwa kwenye luninga watu hawatoenda uwanjani kutazama huo mpira, lkn je mpaka sasa hali iko hivyo?
 
1686076143380.png

Mabehewa sita ya ghorofa kati ya mabehewa 30 kwa ajili ya reli ya kiwango cha SGR tayari yamewasili kwenye Bandari ya Dar es salaam yakitokea nchini Ujerumani leo June 6 2023 yakiwa aina mbili ambapo daraja la pili lina uwezo wa kubeba abiria 123 na daraja la tatu lina uwezo wa kubeba Watu 140.

Mabehewa hayo yameboreshwa na kampuni ya Luckmier Transport & Logistic ya Ujerumani ambapo mabehewa 24 yaliyosalia na vichwa viwili bado matengenezo yake yanaendelea.

Kuwasili kwa mabehewa haya ni ishara ya kujiandaa na kuanza kwa safari za treni ya kisasa ambapo itakumbukwa hivi karibuni Serikali ilisema reli ya kisasa ya SGR kutoka Dar es salaam kwenda Morogoro (KM 300) itaanza majaribio mwezi wa saba na kutoa huduma mara baada ya majaribio kukamiilika mwaka huu.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete akijibu swali Bungeni aliahidi kwamba mwezi wa sita wanategemea kupokea mabehewa yenye ghorofa na mwezi wa saba mwishoni watapokea kichwa ambapo miundombinu yote ipo tayari kwa ajili ya kuanza.
 
Kwa Tanzania yanaitwa mapya, kwa bara la ulaya mabehewa aina hiyo ya maghorofa yaliishapitwa na wakati. Kwenye baadhi ya nchi za ulaya bado yanatumika kwenye reli za kizamani, yakivutwa na injini za dizeli.... Haya yatatumika kwenye meter gauge au standard?... Hata hivyo tusubiri kuona "Rolling Stock" nazo zitakuwa na usasa kiasi gani. 🤔
 
Back
Top Bottom