Behind every successful man is a great woman/behind every happy woman is a wise man!!

Dr Lizzy

Platinum Member
Joined
May 25, 2009
Posts
31,009
Reaction score
60,629
Kakaz na dadaz katika harakati za kuianza wiki tukumbushane kitu......

Siku zote baba huchukuliwa kama kichwa cha familia na mama ndiye shingo.Shingo inaweza kuelekeza kichwa popote inapotaka, ila ikitokea kichwa kikawa kizito sana itasababisha shingo ielemewe kitu kinachoweza kupelekea shingo kuvunjika.Hivyo hivyo shingo nayo ikiwa lege lege sana inapelekea kichwa kuanguka.

Hivyo basi....kina kaka/baba wasaidieni kina mama kwenye majukumu yao mnayoyaita ni ya wamama ili wasizidiwe sana.Enzi za kusema kulea watoto na shughuli za nyumbani ni za mama tu zimepitwa na wakati.Usiwe mzigo wa kumfanya mwanamke ajutie kukufahamu au aishie tu kuona wenzake wakufurahia maisha, msaidie mwenzako ili mwisho wa siku awe na nguvu za kukusaidia na wewe kwenye majukumu yako.Kusaidiana hakuishii hapo tu....hata kitu kama kupunguza pombe na kumsikiliza/kufuata ushauri wake iwapo una tija ni kumsaidia pia.

Kwa kina dada....wazungu wanasema ''Behind every successful man is a great woman''.Be that woman!Sisi kama wanawake(shingo) tuna nafasi kubwa sana katika maamuzi yanayopelekea mafanikio au maanguko ya wanaume.Kumkejeli mwenzako kwa maneno kama ''we ni mwanaume suruali'' ''huna maana '' na mengine kama hayo haifai.Kama angekua hayo yote usingekua naye!Mpe moyo linapokuja swala la kujiendeleza na kwenye maisha yote kwa ujumla...kumkatisha moyo kwa maneno kama '' huwezi kumfikia fulani...ana pesa sana yule'' ''kazi yenyewe unayofanya hata hailipi vizuri'' n.k kutampunguzia kujiamini.Katika watu wote wewe ndo unatakiwa kuwa mstari wa mbele kumpa moyo na kumuaminisha anaweza na sio kumponda alafu unabaki kushangaa mbona kina fulani wana mafanikio zaidi yetu wakati hatukua mbali sana.

Mwisho....furaha ya kila mmoja wenu inamtegemea mwenzake kwahiyo heshima iwepo(kupeana na kulindiana)..mapenzi ya dumishwe..kusameheana na kuombana samahani kupewe kipaumbele.. kusifiana na kukosoana kistaarabu nako kusikosekane!!All in all usimtendee mwenzako usiyopenda kutendewa(furahisha kufurahishwa...heshimu kueshimiwa n.k.)

Nawatakia wiki njema ndugu zangu wa JF!!!

Nawakilisha!
 
Thats my girl,you said it well!

Nakutakia pia wiki njema yenye baraka tele kutoka kwa Mungu.
 
Maneno mazuri ya busara na mafunzo.
Wababa wakishaoa wanajisahau sana na wakati kabla hawajaoa walikuwa wanajipikia, wanafua, wanaosha vyombo na kazi zote zinazomuhusu.
 
Yani wanavyozikataaga utadhani hawajawahi kabisa kufanya!!
 
Waafrika wengi tumerithi hulka ya kifikra kwamba malezi ya watoto au mtoto ni kazi ya mama na baba jukumu la kuadhibu inapobidi. Madhara yake twayaona kizazi kilichokulia malezi ya aina hiyo hakiambiliki wala kuwa flexable kwa masuala ya kijamii na kisiasa. Mwingiliano wa watu wa mataifa mbalimbali kumetufanya tujifunze baadhi ya tamaduni zenye kutufunza mengi mazuri katika malezi ya familia.
 
sasa hapa masuala ya mkutano wa Beijing na "usawa" yanaingia vipi? Maana siku hizi swali ni "kwanini mwanamke awe shingo na siyo kichwa".. matokeo mwili unakuwa na vichwa viwili. Angalau kwenye hilo la vichwa viwili wanaume wamekuwa wakihangaika nalo tangu enzi za Adam na Hawa. Labda inabidi watu wake chini na kuandikiana mkataba wa Dos and Donts ili angalau kusiwe na matatizo. Manake itakuwaje kama mwanamke is more smarter, anatoka familia "bora" ( i hate that description!) na mwanamme ndio "wa kule kule". Kweli mwanamke akubali kuwa shingo? Why not switch the positions?
 
Nawe pia nakutakia wiki njema,nitatafakari na kukujibu kesho kwakuwa unafahamu msimamo wangu,cheers.
 
1.Kwasababu yeye sio mwanaume!Hata kama kielimu na kifedha amemfikia au kumpita bado hakumfanyi yeye mwanaume!!

2.Uduni wa mwanaume kwa hali yoyote ile haimnyang'anyi uanaume wake.Sema ni kosa tu tunalolifanya kwa kudhani pesa na elimu vinatuweka juu ya mwanaume!Japo si-entertain idea ya yeyote kujiona juu ya mwenzake.

3.Hapo sio swala la kukubali au kukataa!!Kwani kua shingo kuna ubaya gani???Kinadharia shingo inaweza kukifanya kichwa chochote kile...iwe kuangalia chini au juu..kulia au kushoto!!Tunachotakiwa ni kila mtu kutambua role yake na kusaidia ya mwenzake sio swala la kutake over...maisha ya wawili sio vita wala ushindani!!!
 
Nawe pia nakutakia wiki njema,nitatafakari na kukujibu kesho kwakuwa unafahamu msimamo wangu,cheers.

Hahahhaaha!!!Uporotooooo....naona umeanza!!!Haya nenda kesho uje na mapoints ya ukweli!
 
Sasa tutafanya nini na kina dada wanaotaka kuwa vichwa!? ambao wanaona kuwa hainogi na haiwi sawa hadi wawe kama wanaume.
 
Kakaz na dadaz katika harakati za kuianza wiki tukumbushane kitu......

Siku zote baba huchukuliwa kama kichwa cha familia na mama ndiye shingo.Shingo inaweza kuelekeza kichwa popote inapotaka, ila ikitokea kichwa kikawa kizito sana itasababisha shingo ielemewe kitu kinachoweza kupelekea shingo kuvunjika.Hivyo hivyo shingo nayo ikiwa lege lege sana inapelekea kichwa kuanguka.

Hivyo basi....kina kaka/baba wasaidieni kina mama kwenye majukumu yao mnayoyaita ni ya wamama ili wasizidiwe sana.Enzi za kusema kulea watoto na shughuli za nyumbani ni za mama tu zimepitwa na wakati.Usiwe mzigo wa kumfanya mwanamke ajutie kukufahamu au aishie tu kuona wenzake wakufurahia maisha, msaidie mwenzako ili mwisho wa siku awe na nguvu za kukusaidia na wewe kwenye majukumu yako.Kusaidiana hakuishii hapo tu....hata kitu kama kupunguza pombe na kumsikiliza/kufuata ushauri wake iwapo una tija ni kumsaidia pia.

Kwa kina dada....wazungu wanasema ''Behind every successful man is a great woman''.Be that woman!Sisi kama wanawake(shingo) tuna nafasi kubwa sana katika maamuzi yanayopelekea mafanikio au maanguko ya wanaume.Kumkejeli mwenzako kwa maneno kama ''we ni mwanaume suruali'' ''huna maana '' na mengine kama hayo haifai.Kama angekua hayo yote usingekua naye!Mpe moyo linapokuja swala la kujiendeleza na kwenye maisha yote kwa ujumla...kumkatisha moyo kwa maneno kama '' huwezi kumfikia fulani...ana pesa sana yule'' ''kazi yenyewe unayofanya hata hailipi vizuri'' n.k kutampunguzia kujiamini.Katika watu wote wewe ndo unatakiwa kuwa mstari wa mbele kumpa moyo na kumuaminisha anaweza na sio kumponda alafu unabaki kushangaa mbona kina fulani wana mafanikio zaidi yetu wakati hatukua mbali sana.

Mwisho....furaha ya kila mmoja wenu inamtegemea mwenzake kwahiyo heshima iwepo(kupeana na kulindiana)..mapenzi ya dumishwe..kusameheana na kuombana samahani kupewe kipaumbele.. kusifiana na kukosoana kistaarabu nako kusikosekane!!All in all usimtendee mwenzako usiyopenda kutendewa(furahisha kufurahishwa...heshimu kueshimiwa n.k.)

Nawatakia wiki njema ndugu zangu wa JF!!!

Nawakilisha!
Thamu ka pirimendi....thante!!
 
kuna mengi ya kujadili kwenye hili, lakini naomba nikubaliane na jambo moja............wanawake ni shingo, ni nukweli usiopingika. Ukimpata anayejua anapokwenda, anaweza kupeleka kichwa chako huo kunakofaa, na haijalishi ka akichwa ni cha maana au la....sisi kwenye mechanics, tuchukulie msemo wa mtaani kuhusu Land cruiser ingine ile inayojulikana kwa ubora...mfano rahisi, ile iliyopo kwenye Hardtop n.k. huw tunaziita jiko la maana..........sasa kama mume ni jiko la maana, shingo inaweza kuamua jiko lichome nyumba au lioke mikate na cake.

sijui kama nimeeleweka!! Nitarudi.
 
ndoo maana nakupenda bure dear..
ukiamuaga kumwaga unamwaga haswa..

yes ur a great thinker.
thanx
 
Behind every successful man is a great woman/behind every happy woman is a wise man

Thanks Lizzy... its a fairly balanced quote... what lies behind a happy man? dont we deserve happiness too (in addition to success?
and what about behind a successful woman?? hata hapo si panahitaji something behind? au success of a woman haiko realized?:suspicious:
 
Sasa tutafanya nini na kina dada wanaotaka kuwa vichwa!? ambao wanaona kuwa hainogi na haiwi sawa hadi wawe kama wanaume.
swali la haja hili.... umeshawahi kusikia nyoka ndumilakuwili? basi ndio zao la familia ambayo inakua na wawili wenye kuwa vichwa nyumbani
 
Back
Top Bottom