Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 31,009
- 60,629
Kakaz na dadaz katika harakati za kuianza wiki tukumbushane kitu......
Siku zote baba huchukuliwa kama kichwa cha familia na mama ndiye shingo.Shingo inaweza kuelekeza kichwa popote inapotaka, ila ikitokea kichwa kikawa kizito sana itasababisha shingo ielemewe kitu kinachoweza kupelekea shingo kuvunjika.Hivyo hivyo shingo nayo ikiwa lege lege sana inapelekea kichwa kuanguka.
Hivyo basi....kina kaka/baba wasaidieni kina mama kwenye majukumu yao mnayoyaita ni ya wamama ili wasizidiwe sana.Enzi za kusema kulea watoto na shughuli za nyumbani ni za mama tu zimepitwa na wakati.Usiwe mzigo wa kumfanya mwanamke ajutie kukufahamu au aishie tu kuona wenzake wakufurahia maisha, msaidie mwenzako ili mwisho wa siku awe na nguvu za kukusaidia na wewe kwenye majukumu yako.Kusaidiana hakuishii hapo tu....hata kitu kama kupunguza pombe na kumsikiliza/kufuata ushauri wake iwapo una tija ni kumsaidia pia.
Kwa kina dada....wazungu wanasema ''Behind every successful man is a great woman''.Be that woman!Sisi kama wanawake(shingo) tuna nafasi kubwa sana katika maamuzi yanayopelekea mafanikio au maanguko ya wanaume.Kumkejeli mwenzako kwa maneno kama ''we ni mwanaume suruali'' ''huna maana '' na mengine kama hayo haifai.Kama angekua hayo yote usingekua naye!Mpe moyo linapokuja swala la kujiendeleza na kwenye maisha yote kwa ujumla...kumkatisha moyo kwa maneno kama '' huwezi kumfikia fulani...ana pesa sana yule'' ''kazi yenyewe unayofanya hata hailipi vizuri'' n.k kutampunguzia kujiamini.Katika watu wote wewe ndo unatakiwa kuwa mstari wa mbele kumpa moyo na kumuaminisha anaweza na sio kumponda alafu unabaki kushangaa mbona kina fulani wana mafanikio zaidi yetu wakati hatukua mbali sana.
Mwisho....furaha ya kila mmoja wenu inamtegemea mwenzake kwahiyo heshima iwepo(kupeana na kulindiana)..mapenzi ya dumishwe..kusameheana na kuombana samahani kupewe kipaumbele.. kusifiana na kukosoana kistaarabu nako kusikosekane!!All in all usimtendee mwenzako usiyopenda kutendewa(furahisha kufurahishwa...heshimu kueshimiwa n.k.)
Nawatakia wiki njema ndugu zangu wa JF!!!
Nawakilisha!