Behind the curtain: September 11

Behind the curtain: September 11

Endelea kufuatilia mkuu.. Hasa hasa nikiweka sehemu ya pili na ya Tatu.. Kuna mambo yenye utata sana yalifanywa na "US Intelligence Community" kabla na baada ya tukio ambayo yanatia shaka mno..
Mkuu siyo tu inatilia shaka bali hakuna hata ndege iliyogonga WTC....

Acha watu wapate uhondo wa hii story mkuu tusiwaharibie....
 
Swali kutoka Whatsapp

Je, Usama aliwahi kuishi nchini Marekani? Na je mafunzo yake ya kivita aliyapata wapi?



JIBU:


Nijibu swali la kwanza kwa uchache tu kwa sababu mwishoni mwa makala nitaongelea masuala yenye utata kuhusu Osama, Marekani na Tukio la 9/11.. Mojawapo ni kama je Osama alikuwa "mshirika" wa Marekani..

Kwa sasa ni jibu tu kama Osama aliwahi kuishi Marekani??



Well, ifahamike kwamba rekodi nyingi sana za Idara ya Uhamiaji ya Marekeni za miaka ya 1970 na kurudi nyuma nyingi hazipo au zimepotea au Kuharibika kwa hiyo ni vigumu kupata taarifa kutoka serikalini kuhusu kama Osama aliwahi kuingia Marekani (au yafaa kusema Serikali ya US inataka watu waamini hivyo)


Lakini uko ushahidi unaoonyesha kwamba miezi michache kabla ya Urusi kuivamia Afghanistan Osama bin Laden alitembelea Marekani..


Ushahidi hii unaungwa mkono na mke wa kwanza wa Osama anayeitwa Najwa bin Laden pamoja na rafiki wa Osama wa ujanani anayeitwa Khaled Bartarf..
Wote wanasema kuwa wanakumbuka hii ilokuwa ni mwaka 1979.


Katika kitabu cha Najwa kinachoitwa "The Bin Ladens: An Arabian Family in the American Century", kuna kurasa Najwa anaeleza kuwa, kuna siku Osama alirudi Nyumbani usiku na kumueleza wajiandae wanasafiri kwenda Marekani siku chache zijazo.

Najwa anasema alishangaa safari hii ya ghafla kwani Osama alikuwa na desturi ya kushauriana naye kuhusu mambo yahusuyo familia yao, lakini kutokana na mila za Kiarabu hakuhoji chochote kuhusu safari hii.


Najwa anaeleza kuwa katika safari yao hii walipitia London na baadae wakaelekea Marekani maeneo ya Indiana.

Wakiwa Indiana mtoto wao mmoja aliyeitwa Abdul Rahman akaapata homa kali, na hivyo wakampeleka hospitali.
Najwa anaeleza kuwa hii ilikuwa ni moja kati ya mara yake ya kwanza kuwa karibu kiasi hicho na wazungu, ambapo ni daktari aliyekuwa anamtibia mtoto wake Abdul Rahman.


Najwa anadai kuwa daktari na manesi walikuwa ni wapole kwake na wakarimu mno na hii ilimfanya abadili mtazamo wake juu ya wazungu tofauti na alivyokuwa anaamini.

Najwa anaeleza kuwa siku chache baadae Osama aliwaacha Indiana na yeye akaelekea Los Angels ambako inaaminika kuwa alienda kukutana na 'mentor' wake Abdullah Azzam ambaye alikuwa Marekani kipindi hiki. (Ikimbukwe kuwa kilindi hiki Marekani waliunga mkono waislamu wenye msimamo mkali wa Mujahedeen, miaka ya baadae hata MAK (Muktab al-khidamt) walifungua ofisi Marekani).


Najwa anaeleza kuwa walipokuwa wanarejea Saudi kuna mahala walikuwa kwenye uwanja wa ndege wa Marekani na alikuwa amevalia Abaya jeusi na Hijab.. Anaeleza kwamba wazungu walimshangaa sana na wengine wakaanza kumpiga picha.


Rafiki wa Osama wa kipindi hiki cha ujana Bw. Khaled Bartarf anaeleza kuwa Osama aliliongelea sana tukio hili alipotudi Saudi, na aliliongea sio kwa kuchukia au kuudhika bali aliongea kwa utani.! Khaled anakumbuka Osama alikuwa anasema kwa utani kuwa "it was like being in a show" (kwa kiarabu).


Hii ni moja ya visa vilivyothibitika kuwa Osama aliwahi kuingia Marekani.


The Bold

je ni kweli osama alikufa huuu mwaka 2011 na aliuwawa na wale askari wa majini??
 
Mkuu The Bold Mimi ninaomba uwe unanitag katika nyuzi zako natanguliza shukran
 
Ukiiusoma ulimwengu wa sasa na phase zake itakubidi uwe deep sana, Kuna huyu jamaa anaitwa RIK MAYALL, sasa ni marehemu, uyu jamaa alikufa Kwa kujaribu ku expose 9/11 na ile ya Landon booming, ningekuona mjanja kama ungekua unawaletea watu habari za Geoengineering uzi wako hauna mashiko, kama bado una angaika na makundi feki yakigaidi ambayo si ya kweli na unayatengenezea bado headlines, wewe unasoma soma ili uje kudanganya watu au unatengeneza mazingira ya icho unachokiandika??

Angalia iyo picha then endelea kutudanganya..​
 

Attachments

  • IMG_8889.jpg
    IMG_8889.jpg
    72.5 KB · Views: 206
Ukiiusoma ulimwengu wa sasa na phase zake itakubidi uwe deep sana, Kuna huyu jamaa anaitwa RIK MAYALL, sasa ni marehemu, uyu jamaa alikufa Kwa kujaribu ku expose 9/11 na ile ya Landon booming, ningekuona mjanja kama ungekua unawaletea watu habari za Geoengineering uzi wako hauna mashiko, kama bado una angaika na makundi feki yakigaidi ambayo si ya kweli na unayatengenezea bado headlines, wewe unasoma soma ili uje kudanganya watu au unatengeneza mazingira ya icho unachokiandika??

Angalia iyo picha then endelea kutudanganya..​
Ungetakiwa ulete wewe hayo unayoyajua wewe, yeye kashafanya yake.
 
Back
Top Bottom