Stralis
JF-Expert Member
- Dec 8, 2013
- 618
- 613
group linahusu nn hasa mkuu, fee sio shida tatizo ni content ya group
Fee sio shida kwenu hamna hata baiskeli content unataka ya nin unadhan group tunauza mapazia lala mbele
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
group linahusu nn hasa mkuu, fee sio shida tatizo ni content ya group
mbona umetumia kalories nyingi sanaa kujibu bila sababu.Fee sio shida kwenu hamna hata baiskeli content unataka ya nin unadhan group tunauza mapazia lala mbele
mbona umetumia kalories nyingi sanaa kujibu bila sababu.
Na kweli wekeza nguvu kuwaza vitu vya msingi usiwe kama ccmNimetumia Horsepower 400 braza......!!!!
Na kweli wekeza nguvu kuwaza vitu vya msingi usiwe kama ccm
PeriodTuliza mpapa we dada euginia
Period
Elfu 5
Karibu [emoji4]
Mara moja kwa mwezi!Ni ya kudumu au kila makala natakiwa kujiunga upya?
The bold we ni changamotto sana mzee. Mi napenda sana maswala ya Intelligencia, Nakuomba ukishusha mzigo mpy unitag please. Najua hata movie/series huwa unaangalia vitu vitamutamu kama hivi mzee, nipe majina ya movie ama series boss wangu
Mkuu George Dalali,The Bold, mkuu wangu na role model wangu, kipaji chako cha kufuatilia, kutafiti, kuchambua, kutathmini, kujumuisha na ku wasilisha ni zaidi ya kipaji cha kawaida hasa kwa hoja kwamba kipaji hicho kimejumuisha vipaji vingine ambavyo si kawaida kuwa pamoja. Kwamba wewe unavyo pamoja (kwa maoni yangu) ni sawa na mfano wa kukuta shimo moja la madini lina almasi, dhahabu, ruby, uranium, nk.
Watu waliobahatika kuwa na kipaji cha namna hii ni watu walio bahatika kuwa na jumuiya njema kabisa ya vipaji. Wapo na wewe ni mmoja wao. Ni package inayofaa sana kwa Dunia tunayo ishi.
Kwa namna inayo shawishi utafiti watu wa namna hii pia wanaweza kuwa wahanga wa kipaji husika. Kwa ruksa, niruhusu kugusia baadhi ya changamoto zinazo weza kumkabili mtu mwenye kipaji cha aina yako.
Tahadhari: sina taaluma yeyote ya psychology wala mfanano wa hilo:
1. Kuwa muhanga wa kukosa mfanano. Yaani mtu mwenye kipaji cha kufanana nawe anaweza kuishi pweke hasa kwenye maisha ya kipaji chake. Mfano mzuri wa hili ni upweke wa maumbo mbalimbali kwenye universe. Yaani, kila akijaribu kutafuta wa kufanana naye analazimika kuishia kwenye tumaini kwamba yupo ila kwa wakati huo hamfahamu. Changamoto hii ingawa ni hasi ikikomaa huzaa tunda ambalo kwa kushangaza na kwa maoni yangu ni positive. Mhanga hufikia wakati wa kukubali kwamba hadi wakati huo atakapo pata mfanano anatakiwa kufananisha kipaji chake na watu wanao miliki sehemu tu ya kipaji chake. Mfano, mtu huyo hujenga urafiki na watafiti wasio wachambuzi, wachambuzi wasio wawasilishi nk. Madhara ya tunda hili kwa mhusika ni kuishi kwenye dunia yake lakini kwa kushirikiana na dunia fikirishi ya wengine.
2. Hamu ya kutafuta mfanano. Mtu mwenye kipaji cha namna hii huwa pia ni Mhanga wa kutafuta mfanano. Hoja hii kwa kiasi hufanana na hoja ya kwanza. Hatahivyo inatofautiana na hoja ya kwanza kwa msingi kwamba kama mwenye kipaji husika asipokuwa makini anaweza kuwa muhanga wa matarajio ya kupata mfanano wa wenye sehemu tu ya kipaji chake. Kuweka maneno vyema na kwa kuzingatia mfano wa mchimbaji wa madini, mtu huyu anaweza kutamani kuchimba madini kwenye shimo lake ila akaona inafaa kutoonesha kwamba shimo lake linatoa madini mengine mbali na madini yanayo shabikiwa na wachimbaji wengine!.
3. Mtafaruku wa kukidhi mahitaji ya wafuasi wanao hitaji zaidi ya matunda ya kipaji. Kipaji tajwa cha mhusika chaweza kwa kiwango kikubwa kuridhisha umma wenye sehemu tu ya kipaji hicho. Hatahivyo hili haliondoi uwezekano wa baadhi ya wafuatiliaji kujaribu na hasa kupenda package ya kipaji cha mhusika igusie vipaji vingine. Huu huwa ni mtihani sana kwa mwenye kipaji tajwa.
4. Vyovyote vile iwavyo, ujumbe wangu ni kusema: "the Bold wewe unakipaji adimu, mimi nakufuatilia kwa sababu ya kipaji chako, ni imani yangu kwamba utafika mbali sana. MWENYEZI MUNGU AKUPE NGUVU ZAIDI".
Shukrani sana mkuu!kila neno ninalofikiri kulitoa naona halifai. Labda niseme tu, Shikamoo The Bold!! Fikiria kuandika vitabu, uweke kama riwaya ili kuepusha wafitini na wenye roho mbaya wa nchi hii kukudisturbalize. Jazakharah khair!!