SoC04 Bei nafuu ya uniti za umeme itaongeza uzalishaji na kukuza uchumi wa taifa letu

SoC04 Bei nafuu ya uniti za umeme itaongeza uzalishaji na kukuza uchumi wa taifa letu

Tanzania Tuitakayo competition threads

omary mhwelo

New Member
Joined
May 2, 2024
Posts
2
Reaction score
1
Umeme ni nishati muhimu sana na tunu katika manufaa makubwa ya maisha yetu ya kila siku. Umeme unaumuhimu mkubwa sana katika nyanja zifuatazo;

1. Uendeshaji wa viwanda vikubwa na vidogo vidogo. Umeme husaidia sana kuendesha viwanda hivyo gharama zikiwa kubwa ata bidhaa zitauzwa kwa bei kubwa na gharama zikiwa ndogo pia bidhaa zitakua na bei ndogo.

2. Ufugaji wa wanyama na ndege. Ufugaji wa kisasa unategemea sana umeme kwa kuwa umeme husaidia kutotoresha vifaranga na kuhifadhi vifaranga pia. Umeme pia husaidia katika uhifadhi wa maziwa ambayo nibiashara pia ya wafugaji wengi.

3. Uendeshaji wa biashara. Asilimia kubwa sana ya biashara hutumia umeme kama vile saloon, mashine za kusagaa nakukoboa nafaka na kuchomelea. Watanzania wengi hujishughurisha na huduma hizo, hivyo umeme ni kitovu pekee sana cha biashara.

4. Matumizi ya nyumbani kwa ujumla wake. Umeme hutumika kwa matumizi ya nyumbani kama vile kutoa mwanga, kuwasha vifaa tofauti kama vile pasi, runinga na jokofu. Watanzania tunahitaji huduma hii ili ituwezeshe kuishi maisha yanayoendana namabadiliko ya sayansi na teknologia.

5. Shughuri za usafirishaji mfano treni ya umeme. Usafirishaji ni secta moja wapo inayo kuza sana uchumi wetu, hivyo umeme husaidia kutoa nishati yakuendesha huduma hii. Serikali yetu inajitaidi sana kwenye secta hii mpaka sasa imekamirisha treni ya SGR kwa safari ya kuanzia dar es saalam mpaka dodoma.

6. Kuongezeka kwa uwekezaji. Sehemu yenye umeme wa uhakika wawekezaji wengi huenda sehemu hiyo kwa sababu yakurahisisha uendeshaji wa viwanda na huduma. Serikali yetu inajitaidi sana kuboresha huduma hii ambayo mpaka sasa tunawawekezaji wengi wanakuja kuwekeza nchi kwetu.

7. Nishati mbadala yakupunguza uharibifu wa mazingira. Kwakutumia umeme tunaweza kutunza sana mazingira yetu nakuboresha sana matumizi yake ili kuachana kabisa na matumizi ya mkaa au kuni, ambazo uharibu sana mazingira yetu. Nishat ya umeme hutumika kwa kupikia na kuendesha mashine mbalimbali.

Kutokana na shughuri muhim ambazo umeme unafanya katika maisha yetu bila kuchagua mtanzania ana aina gani ya maisha umeme kwake ni muhimu sana. Tanzania imebarikiwa kuwa na vyanzo mbalimbali vya umeme na serikari yetu sikivu imefanyia kazi vyanzo hivyo nakufanikisha kuzarisha umeme wakutosha. Mfano wa vyanzo hivyo ni pamoja na GesI kinyerezi, bwawa la nyumba ya mungu, mtera, kidatu na bwawa la nyerere. Pamoja na mazuri serikali inayo yafanya lakini pia kuna changamoto zinazotokana na gharama hiyo ya unit za umeme, hivyo serikali inapaswa kuangalia changamoto zifuatazo ili iweze kusaidia watanzania wengi kwakupunguza bei.
CHANGAMOTO ZA BEI KUBWA ZA UNITI ZA UMEME
Gharama za umeme zinachangia kwa kiasi kikubwa kupandisha gharama za maisha yetu watanzania. Mfano umeme unapokua ghari mambo yafuatayo hutokea
1. Gharama za uzalishaji wa bidhaa huongezeka hivyo bei za bidhaa huongezeka pia. Hivyo hufanya watanzania wengi tuishi maisha ya chini sana kutokana nakutohumudu huduma na bidhaa hizo.

2. Wawekezaji hupungua, uwekezaji unaendana na huduma nzuri ya umeme hivyo watashidwa kuja kwa wingi nakusababisha kuwanyima fursa na ajira kwa watanzania wengi, ila gharama zikiwa chini wawekezaji watakuja wengi nakufanya ajira kuwa nyingi kwa watanzania.

3. Hupelekea huduma zingine kupanda kwa gharama kama vile huduma ya maij,
huduma ya maji inategemea sana umeme kwakuendesha mashine za kuvuta na kusambaza maji. Hivyo gharama zikiwa kubwa za umeme lazima na maji pia gharama zitaongezeka.

4. Kushidwa kutumia umeme kama nishati kwamatumizi ya nyumbani kama kupikia. Gharama za unit zikiwa na bei kubwa watanzania wanashindwa kutumia umeme ipasavyo kwakuogopa gharama hivyo utumiaji wa kuni na mkaa utaendelea nakuleta madhara makubwa ya uharibifu wa mazingira.pamoja na changamoto hizo pia kuna faida nyingi za kushusha gharama za unit za umeme kama ifuatavyo.
FAIDA ZA BEI YA UNITI ZA UMEME KUWA NDOGO
TANESCO inafanya kazi nzuri sana katika nchi hii yakuhakikisha huduma ya umeme inaenea kila sehemu katika taifa letu. Pamoja na hivyo bado gharama za ununuzi wa unit bado zipo juu ukizingatia saiv tuna umeme wakutosha mpaka mwingine unabaki. Endapo gharama za unit za umeme zikishushwa yafuatayo yatatokea hivyo yataleta ukuzaji wa uchumi katika taifa letu.

1. Gharama za uzarishaji wa bidhaa zitapungua hivyo bei za bidhaa zitapungua pia. hii hali itaongeza mzunguko wa kibiashara.

2. Asilimia kubwa ya watanzania watakua na uwezo wakuumudu huduma hii. Hivyo urahisi wa maisha yao utaongezeka

3. Gharama za huduma kama maji, usagaji nafaka na biashara za vinjwaji barid zitapungua.

4. Inapunguza gharama za maisha mfano shughuri nyingi zinategemea umeme hivyo
watanzania watapata nafuu kubwa yakupungua kwa bei za bidhaa na huduma.
MAPENDEKEZO YA BEI RAFIKI YA UNITI ZA UMEME
Serikali yetu na shirika la umeme Tanzania (TANESCO), napendekeza bei za uniti za umeme zipungue kwakua hivi sasa tuna umeme wakutosha mpaka unabaki. Hivyo watanzania inabidi wanufaike zaidi na huduma hii na kwakua kuna mpango wakuuza umeme nje ya nchi ili kukuza zaidi mapato ya serikali shirika litaendelea kunufaika. Watanzania kupata umeme bila mgao haitoshi inabidi bei pia ipungue, Uniti 1 iwe chini ya Tsh 100, badala ya TSH. 300, na wale wenye punguzo wanunue uniti 1 iwe chini ya Tsh. 50. Badala ya Tsh 100. Naimani kubwa na serikali yangu ya Tanzania hivyo jambo hili namatumaini litachukuliwa na kufanyiwa kazi kwa manufaa ya watanzania na taifa letu kwa ujumla.
HITIMISHO
Naiomba serikali ikishirikiana na shirika la umeme Tanzania (TANESCO), ichukue hatua kuhusu hili swala lakupunguza bei za unit za umeme kwakua asilimia kubwa umeme ndio kichocheo cha maendeleo ya uchumi wa watanzania. Ukizingatia Mungu katujalia vyanzo vingi vya umeme hivyo nivyema watanzania wanufaike zaid kwa rasilimali hizi. Natoa pongezi za dhati kwa serikali yetu kufanikisha kuzalisha umeme wakutosha mpaka unabaki hivyo basi uzidi kua una tunu zaidi kwa watanzania kwakuweza kuupata kwa bei nafuu ili uendelee kurahisisha maisha yetu watanzania.

 
Upvote 9
Back
Top Bottom