Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko amesema Gharama za kufanya vipimo vya Vinasaba vya Binadamu “Human DNA” zimeongezeka kutoka Laki moja kwa sampuli moja hadi kufikia Laki mbili na kumi na mbili kwa sampuli moja kutokana na Gharama za mchakato wa vipimo hivyo.
“Gharama kwa Sampuli moja ni 212,000/= kwahiyo kwa Kesi ya Baba Mama na Mtoto unazidisha mara tatu , Gharama zinazosalia zinalipwa na Serikali ya Tanzania kwani ilipaswa kuwa Laki saba mpaka nane kwa sampuli moja” alisema Dkt. Mafumiko.
Dkt. Mafumiko ameyasema hayo hii Machi 11, 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari Maelezo uliyopo katika jengo la Wizara ya Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mtumba jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.