Bei ya kitunguu ikoje mtaani kwako?

Bei ya kitunguu ikoje mtaani kwako?

Inatokeaga hii

Kitungu tokea mwezi wa 12 kilianza kuadimika,watu wa mashambani wanajuwa kwanini?

Ova
 
Lkn tunapswa kujua hivi mnajua ghalama ya kuhudumia heka moja ya kitunguu?
Heka moja sio chini ya 4.5 Millions maximum
 
Ngoja nimkumbushe waziri wangu bashe ikiwezekana hii meli iliyotuletea Sukari nyingi kutokea Brazil.....afanye mpango meli nyingine muda huu ianze kupakia na vVitunguu,naona sasaivi wakulima kutajirika
 
Vitunguu vyekundu vinakwenda sana Nairobi na wao wanavifunga vizuri kwenye maboxi kama wao ndio Wakulima na kuviuza nje wengine wanakuja kulima hapa hapa kabisa na inavyoonekana huko kwenye soko la Kitunguu tutaendelea kununua kwa bei juu kwa muda mrefu kidogo..
 
Watatumia fursa kukataza matumizi ya vitunguu.

Kitunguu ni kiungo muhimu kwenye kachumbari sasa kachumbari inasababisha minyoo aina ya Enterobius ambao hupatikana kwa wingi katika kitunguu, Dkt Mohamed Janabi.

Pia Prof, Dr Mohamed Janabi ameongeza kwa kusema yeye ameacha kutumia kitunguu yapata mwaka wa 12 sasa na hajasumbuliwa tena na minyoo hiyo. 😁
 
kitunguu kwa kipindi hiki ni kawaida kupanda bei hii imedhibitiwa hata hivyo bei si mbaya sana
 
Juzi jumapili sokoni Mbezi nimenunua 2kg kwa 10,000/=.

Siyo vitunguu tu hata hoho hazikamatiki mwanzo 1kg ilikuwa 1,500/2,000/= ila sasa ni 4,000/=,niliuliza nikaambiwa vitu vipo juu kwa sababu kilimo msimu huu mvua zilikuwa nyingi so mazao mengi yaliharibika.
 
Yaani vitunguu,sukari nyanya na karoti nihatari kwa afya , chukieni hii fursa msile kwa ajili ya afya zenu.

Alisikika kilaza mmoja serikalini nchini Cuba
 
baada ya kusomasoma mambo ya vitunguu na mwenzie nyanya nimepata hamu ya kachumbari ile mbaya[emoji1786][emoji1786][emoji1786]
lazma hii kitu isakwe na iliwe leo aisee babaangu
 
Back
Top Bottom