Bei ya ku-print na photocopy zimepanda maradufu

Bei ya ku-print na photocopy zimepanda maradufu

Sasa hivi bei ya ku print na photocopy zimepanda maradufu, wataalam wa stationary wanasema sababu kuu ni kupanda kwa bei ya rim paper za size ya A4, wanasema bei ya sasa ni almost 90 elfu Tsh, ambapo zamani ilikuwa ina range 35 elfu.

Na zipo fununu hawa watu wa stationary wanasema huyo supplier ni mmoja ndio analeta izo papers ...

Serikali itusaidie maana hali sio nzuri
Carton saiv 100,000,ream moja ni tsh 20,000 japo Lazima bei ya kopi ipande.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilianzisha ka kiwanda cha kutengeneza karatasi za khaki kwa ku recycle na box used. Hizo hekaheka nilipokutana nazo kwenye namlaka siwezi kuzisahau, niliamua kuachana na miradi nikaenda kufanya biashara nyingine ambako nako nikipoteza kama milioni 30.

Hii nchi ina wapa favour wafanyabishara wakubwa au wakigeni na kuendekeza kuagiza vitu nje hata vile ambavyo vinawezekana kuzalishwa hapa nyumbani kupitia viwanda vidogo vidogo.

Sent from my TECNO LC6a using JamiiForums mobile app
Na tukishapoteza self reliance popote tunabaki kuwa watumwa wa bei zao wanazojisikia, nini kiliua uzalishaji wa karatasi Iringa.?

Na hizi urasimurasimu kwa wajasiriamali inamsaidia nani exactly?? Pole sana........ kwa hali hii tutabakia kusema ooh wasomi wa nchini hawatusaidii. Sasa kama tunazuiwa kujitanua achilia mbali mazingira mengine kama kodi si wote tutaukimbia uzalishaji tubakie machinga.

Tukiwa machinga tena watukimbize tena yaaani, ivi kama taifa tuna mpango gani..... either way lazima tuanzie kwenye ujasiriamali tu
 
Vitu vinapanda bei hovyo halafu walio kwenye mamlaka wao ni kusifia royo tua tu.

Media nazo zimwtutupa kabisa wananchi, hakuna habari za kupanda kwa vitu ni kawa waandishi sa habari hawaishi bongo.

Yote hii alieharibu na kutia woga watu ni mwendazake, walau kipindi cha jk watu walioiga kelele na baadhi ya mambo kua solved lakini sasa hali ni mbaya wa kusema hakuna.
 
Inasikitisha sana..
 
Ukisimama nchale, ukikaa nchale, ukikimbia nchale[emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji1787]
20220527_100123.jpg
20220618_112935.jpg
 
Haiwezekani ku scan vitu na kuvituma kielektroniki zaidi?
 
Haiwezekani ku scan vitu na kuvituma kielektroniki zaidi?
Inawezekana lakini mifumo yetu mingi hairuhusu hilo.
Mfano hizi barua zinazotakiwa kupigwa mihuri na watumishi wa kitengi fulani ..
 
Haiwezekani ku scan vitu na kuvituma kielektroniki zaidi?
Hivyo unavyiscan si ndio hardcopies?
Alafu Kuna baadhi ya vitu huwezi kuacha kutumia hardcopies mfano; mitihani
 
Sasa hivi bei ya ku print na photocopy zimepanda maradufu, wataalam wa stationery wanasema sababu kuu ni kupanda kwa bei ya rim paper za size ya A4, wanasema bei ya sasa ni almost 90 elfu Tsh, ambapo zamani ilikuwa ina range 35 elfu.

Na zipo fununu hawa watu wa stationery wanasema huyo supplier ni mmoja ndio analeta izo papers ...

Serikali itusaidie maana hali sio nzuri
kweli hata nami naona.
 
tatizo watanzania tumekalili product moja ambayo inatoka kaburu.
yani tokea niache kutumia hizo rim zilizopanda na kuingia product niliyoagiza mwenyewe sijawai kuona zikikwama kwenye mashine.
watanzania mnakilili mtaki kuamini hata wengine wana vitu vizuri.
 
...Ungefanya la maana Sana kama ungeitaja hio Bei mpya illiyoongezeka!
 
tatizo watanzania tumekalili product moja ambayo inatoka kaburu.
yani tokea niache kutumia hizo rim zilizopanda na kuingia product niliyoagiza mwenyewe sijawai kuona zikikwama kwenye mashine.
watanzania mnakilili mtaki kuamini hata wengine wana vitu vizuri.

Ukienda Zanzibar unakuta product nyingi tafauti zimeenea.
 
Na zipo fununu hawa watu wa stationery wanasema huyo supplier ni mmoja ndio analeta izo papers ...

Serikali itusaidie maana hali sio nzuri

Mbona makabila yapo mengi sana. Kikawaida ni kila product moja ina supplier wake, sasa sijui huko ulipo wewe huwa kuwa kuna mtu mmoja anaeleta ama vipi.
 
Kwa nini kiwanda Chetu Cha karatasi Mufindi maarufu Kama mgololo hakifanyi kazi, Nani amekihujumu? Karatasi zote zilikuwa zinatoka pale, tumeamua kuwachekea wahuni, sawa!!

Kataa wahuni by slow slow.
 
Inawezekana lakini mifumo yetu mingi hairuhusu hilo.
Mfano hizi barua zinazotakiwa kupigwa mihuri na watumishi wa kitengi fulani ..
Hapo ni mfumo tu, kwenye mihuri watu walishafikiria na ku solve hilo zamani tu.
 
Hivyo unavyiscan si ndio hardcopies?
Alafu Kuna baadhi ya vitu huwezi kuacha kutumia hardcopies mfano; mitihani
Mitihani siku hizi watu wanafanya online, mimi sihafanya mitihani online nchi za watu huku.

Ni mifumo tu.
 
Back
Top Bottom