Bei ya kuku wa kienyeji imekuwa juu sana

MKIBAIGWAsharkss

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2017
Posts
572
Reaction score
1,331
Kuna jamaangu mmoja yupo Dar juzikati akaniuliza kuhusu bei ya kuku Dodoma.nikamwambia sijui mana mm nipo mjini ngoja niulizie watu wa vijijini.

Nilivyouliza watu wa vijijini wakaniambia kuku mkubwa kabisa Tsh 7000 hadi 8000. Jamaa akaniomba nikamnunulie kuku 200 nikasema ngoja niende nikajifunze biashara ya kuku,Leo nimeenda mnadani na bodaboda nikakuta kuku bei juu kweli wanaaanzia 12000 jogoo mkubwa kabisa na kuku wa wastani 8000.

Nikaishia kununua kuku 100 Kwa wastani wa 9800 waliobaki nitaenda kununua kesho mnada mwingine. Wameniambia kuku huwa wanakuwa bei chee sana kuanzia mwezi wa 11.

Ila fursa zingine nilizoziona ni ununuzi wa mbuzi na ng'ombe wamasai wanapiga hela sana unakuta Dogo hana hata suruali anauza madume 20 ya ng'ombe.

 
Hapo wastani wanakufa wangapi kabla hawajafika sokoni na unategemea huko sokoni uwauze kwa bei gani na kwa muda gani?

Angalia huyo jamaa yako wa Dar asikulaze mlango wazi....
 
Mnanunua kuku wa kienyeji 7000 - 12,000? Uku kwetu visiwani wa kienyeji alieshiba anaanzia 20,000 hao wa buku 7 huwa wale reject wa Europe na uturuki na ile mikuku ilojazwa upepo kutoka Brazil
Mkuu kama hawa niliowabeba sh ngapi huko kwenu????
 
Hio ni bei ya jumla sio kwa reja reja. Wakifika sokoni ndo watauzwa kwa bei ya 18000 hadi 20000
Mnanunua kuku wa kienyeji 7000 - 12,000? Uku kwetu visiwani wa kienyeji alieshiba anaanzia 20,000 hao wa buku 7 huwa wale reject wa Europe na uturuki na ile mikuku ilojazwa upepo kutoka Brazil
 
Naona SOKO LA WANYONGE lipo poa kabisa wakati MABEBERU wakifanya shopping MLIMANI CITY KWENYE AC, na hao mabeberu nyie ndio mnawapa kura.

Ipande tu, kwanza hiyo ulonunulia ni ndogo, wanyaturu wapandishe tu maana huko mjininmnakula hela sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…