Bei ya luku ishuke, viwanda vifufuliwe, wananchi wapikie majiko ya umeme kuzuia uharibifu wa mazingira

Wazo zuri sana
 
Sie enzi hizo tulipikia maharage jiko la umeme.

Saizi una kipato Cha zaidi ya 1m lakini huwezi kupikia jiko la umeme,

Sasa uchumi wa kati tulioufikia ni upi sasa!!
Ila mkuu ukitafakari hii nchi huwezi kuielewa! Wanasema tunasonga mbele wakati kuna mambo tunarudi nyuma! Sasa umeme upo mwingi mpaka wamezimia mitambo lakini gharama bado iko juu! Mibunge yetu nayo mi hopeless kabisa!
 
Sie enzi hizo tulipikia maharage jiko la umeme.

Saizi una kipato Cha zaidi ya 1m lakini huwezi kupikia jiko la umeme,

Sasa uchumi wa kati tulioufikia ni upi sasa!!
Kuna mwaka nilienda hapo kwa majirani zetu Zambia aisee wao umeme inaoneka cheap sana..Maana familia nyingi nilizo bahatika kutembelea wanatumia sana vifaa vya umeme..majiko ,mashine za kufulia na wana vifaa vingi mno vya kutumia umeme majumbani na wakati mwingine hata taa kuzima wanaona tabu .Nikauliza wakasema umeme kwao sio kilwazo sana.

Ukiitafakari nchi yenu..Nina amini soon Mungu wetu alie hai atatupatia uhuru toka katika mifumo onevu..Tuzidi kuiombea sana nchi yetu ufungulivu wa kila idara maana kila nikitafakari juu ya nchi yangu kwakweli napata tabu sana na haswa vile wananchi hatupendi kuipa changamoto serikali kwa kuipa maswali.Hofu na mashaka vimeruhusu kukandamizwa sana kwa wananchi ndani ya nchi yetu.

Ee Mungu wangu na Baba ninakuomba utuinulie wakina Yehu wa kizazi hiki katika nchi yetu katika jina la Yesu kristo.
 
Hiyo Bado kubwa,

Unit 1 iwe sh 10.

Hapo Hadi maharage utapika bila shida.
Hiyo itafanya shirika lishindwe kabisa kujiendesha. Piga hesabu tunazalisha Kwh ngapi kwa mwaka halafu uuze kila moja Tsh 10! Hii bei ni sawa na bure.
 
Ila mkuu ukitafakari hii nchi huwezi kuielewa! Wanasema tunasonga mbele wakati kuna mambo tunarudi nyuma! Sasa umeme upo mwingi mpaka wamezimia mitambo lakini gharama bado iko juu! Mibunge yetu nayo mi hopeless kabisa!
Imeandikwa ,RUSHWA hupofusha ufahamu.

Ndiyo maana bungeni wapo maproffessor lakini wameshindwa kuhakikisha wananchi wananufaika na utajiri wa Nchi Yao kupitia raslimali zao.

Tuongeze nguvu katika kudai tume HURU ya UCHAGUZI na KATIBA mpya kabla ya Uchaguzi wowote, mema yatakuja nchini.
 
Inabidi vijana waanzishe chama chao ili wapiganie uhuru kwa mara ya pili, Haya mapinzani yaliyopo nayo ni maslahi tu hayawezi kutukomboa!
 
Yehu ni Gwajima.

Ameshaingia katika mfumo,

Mungu ameshasema na watumishi wake kuwa huyo ndiye atakayeivusha Taifa bila kujali chama,

CCM wakimteua tutavuka, la wakimkataa akaingia CDM tumevuka,

Tusikae nyumbani, tujitokeze kuhakikisha nchi yetu inapata hatua.
 
Inabidi vijana waanzishe chama chao ili wapiganie uhuru kwa mara ya pili, Haya mapinzani yaliyopo nayo ni maslahi tu hayawezi kutukomboa!
CCM wavurugane Ili ipatikane upenyo.
 
Hili suala nilishashauri kitambo yaani hakuna sababu ya watu kutumia gesi ambayo tunaagiza kutoka nje....

Ushauri mzuri.
 
Ni wazo zuri sana.
Kuliko kufunga mitambo eti umeme imekuwa mwingi ni bora kushusha bei ili viwanda vingi vijengwe kutoa ajira Kwa wananchi.
Sambamba na hilo vifaa vinavyotumia umeme vitaongezeka Kwa wingi ili wananchi wapate unafuu wa nishati Kwa matumizi ya nyumbani ili kuokoa mazingira.
Matumizi ya nishati ya Gesi yabaki kwenye kuendesha mitambo na kuuza nje ya Nchi tupate fedha za kigeni.
Lakini pia ni vizuri kuliko kufunga mitambo eti kwa sababu umeme umezidi mahitaji itafutwe namna ya kuvuna umeme wakati huu palipo na mvua nyingi na kuuhifadhi kwa matumizi ya baadae.
 
Uzalendo uko chini,

Wanajua,maisha ya Mwananchi maskini yakiboreka, itakuwa ngumu kutawalika.

Tukatae hii Roho ya kuzimu Toka Kwa viongozi wetu.
 
Uzalendo uko chini,

Wanajua,maisha ya Mwananchi maskini yakiboreka, itakuwa ngumu kutawalika.

Tukatae hii Roho ya kuzimu Toka Kwa viongozi wetu.
Yawezekana uzalendo ukawa juu SEMA tu resources zikawa hazipo.
Kwa kuwa tayari tunayo miundombinu wezeshi wale think tank wa Nchi wafanyie kazi ushauri na tafiti za namna ya kutokomeza umaskini.
Sio sifa kumtawala maskini kwa kumnyima huduma muhimu.
Ni dhambi kubwa kwa Mwanasiasa kudhani ni lazima awatawale watu wenye dhiki,taabu na ufukara kwamba eti ndio msingi wake muhimu.
Huo ni uoga.
 
Wabunge wanagawa mitungi ya gesi tu. Hawatoa maoni kuhusu bei ya gesi. Sasa mitungi bila gesi, inasaidia nini. Uharibifu wa mazingira utaendelea...mbaya zaidi kukata miti asili, na kupanda miti ya kisasa
 
Wabunge watokanao na wizi wa kura lazima akili waziache nyumbani
 
Faida ya gesi ndiyo takrima kwa viongozi wenu, hata magwanda ya kaki wakipewa nchi kwa hiyo bei hawatoboi, labda kidogo unit ikiuzwa kati ya sh 150/= na 200/= itawezekana ukiweka na gharama za uendeshaji....
 
Biashara ni mizunguko,

Unit 1 ikiuzwa sh 10, watapata faida kubwa sababu ya mizunguko mkubwa.

Ajira zitatengezwa kupitia umeme nafuu, Uchumi utaimarika, Kodi itakusanywa zaidi.

Ngoja tuchague CDM itoe Rais nao tuwapime, CCM imezeeka.
 
TANESCO nao wasanii...Kijijini nguzo moja ni Laki 5. na kuunganisha ni 27000

Yaani ni miti aina gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…