Bei ya luku ishuke, viwanda vifufuliwe, wananchi wapikie majiko ya umeme kuzuia uharibifu wa mazingira

TANESCO nao wasanii...Kijijini nguzo moja ni Laki 5. na kuunganisha ni 27000

Yaani ni miti aina gani?
Nguzo Huwa zinanunuliwa miti yake mafinga, zinapigwa stika ya south Afrika, tanesco wanazinunua Kwa Bei ya sa, pesa zinaingia mifukoni mwa wakubwa.

Wizi na RUSHWA ndo chanzo Cha gharama kubwa ya uendeshaji na HASARA tanesco tunaongezewa Bei ya luku.
 
Bei ya umeme ishuke Ili kufufua viwanda na kuchangamsha Uchumi wa wananchi.
 
Taarifa: Wingi wa jiko ni meko na siyo majiko. Omba mods wakurekebishie heading.
 
Taarifa: Wingi wa jiko ni meko na siyo majiko. Omba mods wakurekebishie heading.
Loh, sikulijua hili, ngoja nipitie kamusi,

Hata hivyo NENO " Meko ya Umeme" wengi hawaujui msamiati huo.

Acha ibaki hivyo hivyo imeeleweka.

Ahsante Kwa ufafanuzi, na karibu utoe michango wako.🙏
 
Chama cha Ma-vampire kimetugeuza wananchi Mazombi
Wanataka Wananchi walipe Kodi ilhali Bei za umeme ziko juu,

Sasa Bei ingepungua, viwanda vidogo vidogo vingeongezeka sababu ya nafuu ya Bei ya nishati!!

Hawa sijui uchumi wamesomea wapo🤔
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…