Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
Mbona hujamaliza kukokotoa hiyo hesabu hadi mwisho kwa kituo cha mafuta kilichopo hususani mwisho wa reli aka Kigoma? Kwa kukuongoza:Ndugu zangu wana JF baada ya kutoka bei za mafuta kupitia EWURA nimeona niingie kufanya utafiti niweze kujua bei za mafuta ghafi na gharama zake za kuyasafisha na kusafirisha mpaka kufika kwetu hapa Tanzania.
Hapa nitaleta taarifa za kina kuona namna gani tunaweza kufanya au kujua dunia jinsi ilivyo.
Nimetumia mitandao kadha wa kadha ambayo inaleta taarifa live za bei ya Barrel moja na mafuta ghafi.
Kwanza Barrel ni nini?
Ni kipimo ambacho kimepitishwa duniani kwaajili ya kuuziana mafuta.
Barrel = 158.987 Liter tunaweza kusema 159 Liter
Maana yake ukinunua barrel moja utakuwa umenunua Lita 158.9 za mafuta.
Source: Convert Barrel (oil) to Liter
View attachment 2740681
BEI ZA MAFUTA GHAFI DUNIANI
Bei za mafuta duniani zinabadilika badilika, lakini siyo sana. Na mafuta haya yanatofautina bei kulingana na gharama zake za kuyasafisha. Mafuta Ghafi yenye gharama ya juu sana ni Arab Light kutoka Saudia bei yake ni $92.56/bbl
View attachment 2740703
Source:-
![]()
Crude Oil - Price - Chart - Historical Data - News
Crude Oil decreased 0 USD/BBL or 0.00% since the beginning of 2025, according to trading on a contract for difference (CFD) that tracks the benchmark market for this commodity. Crude Oil - values, historical data, forecasts and news - updated on February of 2025.tradingeconomics.com
GHARAMA YA KUSAFISHA MAFUTA GHAFI
Kulingana na tafiti zilizo kwa kiwanda kikubwa kabisa cha kusafisha mafuta mfano kilichopo marekani Texas Exxon Baytown Gharama zake ni $3–4/Bbl
Lakini kama refinery ni ndogo ngarama inaenda juu ni $10–12 per bbl.
GHARAMA ZA USAFIRISHAJI KWA BARREL MOJA
KUsafirisha barrel moja gharama zake zipo standard ni $10-$15 per barrel
SASA NAOMBA TUPIGE HESABU SASA GHARAMA HALISI YA MAFUTA KWA LITA
Naomba katika hesabu zangu nipige kwa kuangalia gharama za juu.
Bei ya Crude oil per barrel = $92.56
Bei ya Kusafisha = $12
Bei ya Kusafirisha = $15
Gharama zingine = $10
JUMLA =$129.56
Tutafute bei ya mafuta hayo kwa litre moja
129.56/158.987 = 0.81
Maana yake bei ya mafuta ni $0.81
Naomba niongezee na gharama zingine 20% ya International Tax
Ni sawa na $0.162 kwa kila lita jumla itakuwa
0.972
Kwahiyo bei halisi ya mafuta ni $0.972
Tutafute kwa pesa zetu za kitanzania 2,385.80 Tanzanian Shilling
View attachment 2740732
JE SHIDA NI NINI?
1. Weka faida ya muagizaji wa hayo mafuta kwa litre.
2. Weka kodi na tozo lukuki kwa kila lita ifikapo bandarini.
3. Weka gharama ya kusafirisha hayo mafuta per litre hadi mwisho wa reli.
4. Weka faida ya mmiliki wa kituo cha mafuta (petrol station) per litre
Jumulisha vyote hivyo, halafu tupe jibu. Baada ya hapo ndipo tutaweza kushauri wapi tunaweza kupunguza bei hizo.
Maeneo ambayo tunaweza kwa kiasi fulani ni haya yafuatayo:
1. Kupunguza baadhi ya kodi na tozo za serikali. Hii ni ngumu kwani watakwambia serikali itakosa pesa za kununua dawa, kutoa elimu bure, kutoa posho za wabunge na kadhalika.
2. Serikali kurejesha na kuiongeza ruzuku kwenye mafuta haya iliyoisitisha kuanzia January 2023. Hili nalo si jambo rahisi kwani pesa hii ya ruzuku itatokana na serikali kupunguza hela ya kununulia dawa, posho za vigogo, V8 za vigogo na kadhalika.
3. Serikali kukunua hayo mafuta moja kwa moja kutoka huko Uarabuni au Urusi kupitia shirika letu la TPDC badala ya makampuni binafsi kama ivyo sasa. Hili nalo ni gumu sana kwani makampuni haya ya binafsi ndiyo yanayowaneemesha vigogo wa serikali na mengine ni ya kwao binafsi. Hata ungalikuwa ni wewe hili usingalikubali hata kidogo.
4. Shirika letu la reli ndilo pekee litumike kuyasambaza hayo mafuta kutoka bandarini hadi mwisho wa reli. Ugumu wa hili ni sawa na ule wa namba 3 hapo juu. Malori yanayosambaza hizo bidhaa toka bandarini nchini na nje ya nchi, wanufaika ni hao vigogo na mengine ni mali yao. Hata hiyo SGR ikamalizika, hayo malori yataendelea kufanya hivyo, bei ya usafiri wa SGR itawekwa kuwa kubwa zaidi ili malori na mabasi ya vigogo yaendelee.
5. Tujenge refinery yetu kubwa pale Dar es Salaam kwa pesa ya mkopo toka World Bank, Africa Development Bank, marafiki zetu wa Dubai, UAE, China, Russia etc. Hii itatuwezesha kununua crude oil badala ya refined oil na kuifanya nchi yetu kuwa hub ya mafuta haya ambayo tutaziuzia nchi zote za SADEC na za Afrika Mashariki na kupata faida kubwa na kuachana kukimbizana na walala hoi mitaani kusaka tozo za kuendeshea serikali.
Yote haya tumwachie Dr Doto Biteko ambaye rais wetu amempa rungu kubwa (la unaibu waziri mkuu) la kupambana na haya mambo magumu ya nishati. Ni kijana mpambanaji na bila shaka atatuvusha.