Bei ya mafuta ghafi duniani na gharama za kusafisha (Crude oil Price)

Mbona hujamaliza kukokotoa hiyo hesabu hadi mwisho kwa kituo cha mafuta kilichopo hususani mwisho wa reli aka Kigoma? Kwa kukuongoza:

1. Weka faida ya muagizaji wa hayo mafuta kwa litre.
2. Weka kodi na tozo lukuki kwa kila lita ifikapo bandarini.
3. Weka gharama ya kusafirisha hayo mafuta per litre hadi mwisho wa reli.
4. Weka faida ya mmiliki wa kituo cha mafuta (petrol station) per litre

Jumulisha vyote hivyo, halafu tupe jibu. Baada ya hapo ndipo tutaweza kushauri wapi tunaweza kupunguza bei hizo.

Maeneo ambayo tunaweza kwa kiasi fulani ni haya yafuatayo:

1. Kupunguza baadhi ya kodi na tozo za serikali. Hii ni ngumu kwani watakwambia serikali itakosa pesa za kununua dawa, kutoa elimu bure, kutoa posho za wabunge na kadhalika.

2. Serikali kurejesha na kuiongeza ruzuku kwenye mafuta haya iliyoisitisha kuanzia January 2023. Hili nalo si jambo rahisi kwani pesa hii ya ruzuku itatokana na serikali kupunguza hela ya kununulia dawa, posho za vigogo, V8 za vigogo na kadhalika.

3. Serikali kukunua hayo mafuta moja kwa moja kutoka huko Uarabuni au Urusi kupitia shirika letu la TPDC badala ya makampuni binafsi kama ivyo sasa. Hili nalo ni gumu sana kwani makampuni haya ya binafsi ndiyo yanayowaneemesha vigogo wa serikali na mengine ni ya kwao binafsi. Hata ungalikuwa ni wewe hili usingalikubali hata kidogo.

4. Shirika letu la reli ndilo pekee litumike kuyasambaza hayo mafuta kutoka bandarini hadi mwisho wa reli. Ugumu wa hili ni sawa na ule wa namba 3 hapo juu. Malori yanayosambaza hizo bidhaa toka bandarini nchini na nje ya nchi, wanufaika ni hao vigogo na mengine ni mali yao. Hata hiyo SGR ikamalizika, hayo malori yataendelea kufanya hivyo, bei ya usafiri wa SGR itawekwa kuwa kubwa zaidi ili malori na mabasi ya vigogo yaendelee.

5. Tujenge refinery yetu kubwa pale Dar es Salaam kwa pesa ya mkopo toka World Bank, Africa Development Bank, marafiki zetu wa Dubai, UAE, China, Russia etc. Hii itatuwezesha kununua crude oil badala ya refined oil na kuifanya nchi yetu kuwa hub ya mafuta haya ambayo tutaziuzia nchi zote za SADEC na za Afrika Mashariki na kupata faida kubwa na kuachana kukimbizana na walala hoi mitaani kusaka tozo za kuendeshea serikali.

Yote haya tumwachie Dr Doto Biteko ambaye rais wetu amempa rungu kubwa (la unaibu waziri mkuu) la kupambana na haya mambo magumu ya nishati. Ni kijana mpambanaji na bila shaka atatuvusha.
 
Tutafute kwa pesa zetu za kitanzania 2,385.80 Tanzanian Shilling
Nashukuru sana kwa muda wako kuandaa bandiko hili. Ni mwanzo mzuri sana katika kutafuta ukweli.

Kwenye gharama Umeweka na gharama za bima kusafirisha hayo mafuta...mpaka Omukihisi na Mwemage !? Yaani , kwa ufupi tusaidiane kupata takwimu halisi tuone ni akina nani wanatuumiza sisi watanzania! Tunataka kujua wabaya wetu ni akina nani ili tutafute namna nzuri ya kuwadhibiti.

Asante.
 
Wanaohujumu mafuta ya Petroli ni serikali wenyewe,CCM ni mafisadi hawafai kuwa madarakani
Your browser is not able to display this video.
 
Hamjamwelewa mleta mada! Mwishoni ameuliza shida ni nini?
 
Hamjamwelewa mleta mada! Mwishoni ameuliza shida ni nini?
Mbona kama tumemuelewa vizuri tu. Jana EWURA ilitangaza bei mpya ya mafuta haya kupanda hadi TZS 3,500 kwa lita (dizeli) huku mwisho wa reli, kutoka bei ya Sh 3,080 ya mwezi uliopita. EWURA walitoa sababu kadhaa zilizosababisha upandaji huo wa 20%. Mleta mada kafanya utafiti na kupata bei ya mafuta haya kuyanunua hadi kuyafikisha bandari ya Dar es Salaam (CIF price per litre). Utafiti wake unapinga sababu zilizotolewa na EWURA. Lakini utafiti wake umegundua kwamba gharama ya mafuta haya hadi kuyafikisha DSM ni kama USD 0.9 kwa kila lita, sawa na Sh 2,300. Sasa anauliza shida ni nini? Maana yake inakuwaje EWURA watangaze bei ya Sh 3,500 kwa lita? Au wewe umemwelewaje?
 
Asante
 
Shida ni utitiri wa tozo kwenye biashara ya mafuta!! Utafiti wako uingie kwenye wingi wa tozo kwenye biashara ya mafuta, ujue na road licence imo humo!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…