haiwezekan kupunguza bei ya bidhaa mbalimbali kam bei ya mafuta ipo juu, hapa tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu, serikal inapaswa kubeba lawama juu ya suala hili, kwani katika hali ya kawaida tu hakuna jitihada zozote zile zinazofanywa na serikali katika kuhakikisha maisha ya Watanzania yanakuwa bora kama wanagamba walivyoahidi katika kampeni zao zisizotekelezeka. mfno ni kwamba wakati hii serikal inapandisha kima cha chini cha mishahara ya watumishi wake mwaka jana sukari ilikuwa 800-1000 lakini leo hii sukari ni kuanzia 1600-2000 imeapanda kwa 1000% lakini serikali bado ipo ipo tu, huyu mtu atamudu vip maisha yake. Viongozi wa serikali wanalipa posho tu kuptia kodi za hawa watanzania ambao inawadhulumu, zaidi ya nusu ya bajet ni kuendesha serikali tu, sasa kweli hapa kuna maisha gan ambayo ni bora zaidi ya kuchoshana tu. Watanzania wana kila sababu ya kuilaumu serikal ya Kikwete na wangamba wenzie. wao wanakula maisha sisi tunateseka tu, kwa kweli tumefika wakati tuwakatae hadharani kwani watanzania walalahoi wamechoshwa na matuimiz mabovu ya rasilimali zao. MH. kikwete Tambua kwamba Watanzania walitegemea maisha bora na sio maisha bora. Lawama zote zinaelekezwa kwako kwa kuwa wewe ndo kiongozi uliyepewa dhamana ya kuongoza nchi hii. Usipoamua kufanya maamuzi amgumu na mazito sio siri hii inaweza kukupa wakati mgumu sana katika kutekeleza majukumu yako. Watanzania tunaomba utekeleze yale uliyoahidi watanzania. Vua gamba Mh. chinjilia baharini hawa mafisadi ili urejeshe imani na matumaini kwa Watanzania, sikiliza maoni ya Watanzania bila kujali itikadi za kisiasa. ni hayo tu kwa leo!