Bei ya mafuta Kenya yashuka

rushanju

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Posts
3,238
Reaction score
5,106
Wakuu... Nimeangalia taarifa ya habari ya KBC sasa hivi na habari kuu ilikuwa ni kuhusu bei ya mafuta ya petrol kushuka. Kwa mujibu wa kitengo cha udhibiti wa nishati (kawi) bei ya pertol imeshuka kwa sh saba za kenya na bei mpya itakuwa ni sh 108. Hii ni kutokana na kushuka kwa nishati hiyo katika soko la dunia. Bei hiyo itatumika hadi tarehe 15 mwezi ujao. Wakuu sijuhi Exchange rate ya sasa imesimama wapi yaani kati ya Tsh na Kshs.

Nawasilisha

SOURCE: KBC. Taarifa ya habari saa moja
 
We acha tu. Wenzetu hawa wako mbali sana na sio mafuta tu bali pia umeme pia wameshusha. Mkuu ha mie ekisichenji sijui ikoje sasa. ngoja wataalam watujuze
 
mkuu ni pefrol tu au na mafuta mengine, eg dezel ya taa nk. Mi mtumba wangu unatumia dixel afu niko mpakani kabisa.
 
Yameshuka yote isipokua mie nimeangalia pale panaponihusu tu maana nami mkweche wangu watumia petrl yakhe
 
Imepungua kwa Tzs 127. . .
Na hiyo 108 ni sawa na 1955 Tzs

Kwahiyo inabidi muangalie kiasi hicho kinachouzwa kwa Kes 108 (1955 Tzs) huko Kenya kinauzwa kwa bei gani bongo ili kujua tofauti iliyopo baada ya wao kupunguziwa bei.
 
Imepungua kwa Tzs 127. . .
Na hiyo 180 ni sawa na 3253 Tzs

Kwahiyo inabidi muangalie kiasi hicho kinachouzwa kwa Kes 180 (3253 Tzs) huko Kenya kinauzwa kwa bei gani bongo ili kujua tofauti iliyopo baada ya wao kupunguziwa bei.

Bei 108 siyo 180.
 
Bei hiyo itatumika hadi tarehe 15 mwezi ujao.
Mnaona hapo wenzetu walivyo makini?
Wanajua bei mpya inadumu kwa muda fulani ambao wanaamini akiba yao ndo itakuwa imeisha kabla ya kuanza kutumia mpya na bei mpya,ila kwa sisi ungekuta bei inapanda leo then baada ya siku 4 imebadilika hata km bado bidhaa maghalani hazijaisha.
 
Mh! Jana nilitizama on tv Pump ilisomeka ksh 111.9 sikujua kama ni Diesel au Petrol nikazidisha kwa 18 nikaona kama wanauziwa kwa tsh 2014.2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…