Tetesi: Bei ya mafuta kupanda kuanzia tarehe moja novemba!!

iparamasa

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2013
Posts
13,437
Reaction score
14,927
EWURA itapandisha bei za mafuta kuanzia tarehe moja novemba,hii ni kwa mujibu wa tetesi kutoka chanzo cha uhakika.

Baadhi ya vituo vya mafuta vimekuwa vikijizuia kuuza mafuta katika maeneo yao kusubiri ujio wa bei mpya

Tujiandae kwa pigo hili watanzania
 
kila janga huambana na msindikizaji wake,

japo kuna ugumu wa maisha,mafuta pia yatapanda, kwa mujibu wa tetesi
 
Ni njia nzuri ya kupunguza umiliki wa magari na kuepuka uchafuzi wa mazingira
 
EWURA itapandisha bei za mafuta kuanzia tarehe moja novemba,hii ni kwa mujibu wa tetesi kutoka chanzo cha uhakika.

Baadhi ya vituo vya mafuta vimekuwa vikijizuia kuuza mafuta katika maeneo yao kusubiri ujio wa bei mpya

Tujiandae kwa pigo hili watanzania

Huo ni wazimu,bei ya mafuta imeshuka duniani,na sio leo au kesho itakuwa afueni,mafuta ni mengi kuliko soko yamezagaa,yataendelea kushuka zaidi kwa kuwa Marekani ana zalisha zaidi kwa kutumia tekinologia mbadala,na huku Mrusi akizalisha mengi mno na kuuza kwa bei ya chini zaidi.Hata kama Opec wakikubaliana kupunguza uzalishaji,kitu ambacho hakiwezekani,bado mafuta ni mengi mno.
Yabidi Eura atambue mafuta sio deal tena,afadhali mineral water.
 
Huu ni wizi wa mchana kweupe, katika soko la dunia bei ya mafuta inashuka kutokana na kutoelewana kati ya nchi za OPEC na zile ambazo hazimo OPEC katika kupunguza viwango vyao vya uzalishaji, lakini hapa nchini inapandishwa!

EWURA itapandisha bei za mafuta kuanzia tarehe moja novemba,hii ni kwa mujibu wa tetesi kutoka chanzo cha uhakika.

Baadhi ya vituo vya mafuta vimekuwa vikijizuia kuuza mafuta katika maeneo yao kusubiri ujio wa bei mpya

Tujiandae kwa pigo hili watanzania
 
Inawezekana hawa Ewura wamepewa maagizo ya kusaidia kuiingizia mapato serikali chovu hii kwa kuongeza bei ya wese.
 
Huu ni wizi wa mchana kweupe, katika soko la dunia bei ya mafuta inashuka kutokana na kutoelewana kati ya nchi za OPEC na zile ambazo hazimo OPEC katika kupunguza viwango vyao vya uzalishaji, lakini hapa nchini inapandishwa!
Tupe data za bei ya pipa la mafuta ghafi kwa leo katika kutibitisha hoja yako.
 
HAWA EWURA WALAGAI SANA MAFUTA HUKO NJE YAMESHUKA ILA WAO HUKU KUTWA WANATAKA KUYAPANDISHA....

OVA
 
Back
Top Bottom