Tetesi: Bei ya mafuta kupanda kuanzia tarehe moja novemba!!

Tetesi: Bei ya mafuta kupanda kuanzia tarehe moja novemba!!

Mafuta yakipanda bei kila kitu kinapanda bei vyakula masokoni bei juu nauli ya magari bei juu matrekta ya kulimia bei juu nk tutasoma namba sana.
 
EWURA itapandisha bei za mafuta kuanzia tarehe moja novemba,hii ni kwa mujibu wa tetesi kutoka chanzo cha uhakika.

Baadhi ya vituo vya mafuta vimekuwa vikijizuia kuuza mafuta katika maeneo yao kusubiri ujio wa bei mpya

Tujiandae kwa pigo hili watanzania

Ni kawaida kila jumatano ya mwanzo wa mwezi EWURA wanatoa bei elekezi ya mwezi husika na hii inategemea inaweza ikapanda au ikashuka kutokana na mzunguko wa bei ktk soko la dunia ulivyo
 
Acha yapande watu wajenge nyumba.
Maana kila Mtu Dar anataka kuwa na Gari,foleni zogooo
Kila kitu kina muda wake,mie nilioa mahari 250,000 tu leo hii the same family mahari 1m kwenda juu.

Sasa maisha hayawezi kula siku kuwa pale pale,hembu tujifunze
 
1477947507903.jpg
 
daaah! na gari sinunui tena..!

habari za kuwa na ndinga alafu daily ipo uwani ukiulizwa vipiii?? aah! EWURA wamefanya yao bwanaaa

Makufuri bwana!
 
Huo ni wazimu,bei ya mafuta imeshuka duniani,na sio leo au kesho itakuwa afueni,mafuta ni mengi kuliko soko yamezagaa,yataendelea kushuka zaidi kwa kuwa Marekani ana zalisha zaidi kwa kutumia tekinologia mbadala,na huku Mrusi akizalisha mengi mno na kuuza kwa bei ya chini zaidi.Hata kama Opec wakikubaliana kupunguza uzalishaji,kitu ambacho hakiwezekani,bado mafuta ni mengi mno.
Yabidi Eura atambue mafuta sio deal tena,afadhali mineral water.
Nimependa uzamiaji wako kupata habari [emoji122] sasa naomba embu zamia hii gesi yetu ya hapo mtwara .inakuwaje imeshindwa kabisa kupunguza bei ya uzalishaji umeme ,ilitupunguziwe bei ya umeme kama walivyotuahidi kuwa gesi ikianza kutumika ingepunguza bei kwa 50% bei ya sisi watumiaje baadala yake walipunguza kwa 1.07%
Nategemea uje na Maelezo mazuri zaidi ataa kushinda haya ya nchi za watu huko mbali ukizingatia ni hapo hapo tuu Dar-Mtwara
 
EWURA itapandisha bei za mafuta kuanzia tarehe moja novemba,hii ni kwa mujibu wa tetesi kutoka chanzo cha uhakika.

Baadhi ya vituo vya mafuta vimekuwa vikijizuia kuuza mafuta katika maeneo yao kusubiri ujio wa bei mpya

Tujiandae kwa pigo hili watanzania
Itabidi mkasome namba iliyoongezwa, maana hakuna namna!
 
Bei hazijawa confirmed, watu wanatokwa povu na kulaani kila kitu. Hizi ni tetesi, hazijawa reality bado. Hii ni kwa wale wataalam wa kuponda kila kitu...
 
Huu ni wizi wa mchana kweupe, katika soko la dunia bei ya mafuta inashuka kutokana na kutoelewana kati ya nchi za OPEC na zile ambazo hazimo OPEC katika kupunguza viwango vyao vya uzalishaji, lakini hapa nchini inapandishwa!

Nimependa uzamiaji wako kupata habari [emoji122] sasa naomba embu zamia hii gesi yetu ya hapo mtwara .inakuwaje imeshindwa kabisa kupunguza bei ya uzalishaji umeme ,ilitupunguziwe bei ya umeme kama walivyotuahidi kuwa gesi ikianza kutumika ingepunguza bei kwa 50% bei ya sisi watumiaje baadala yake walipunguza kwa 1.07%
Nategemea uje na Maelezo mazuri zaidi ataa kushinda haya ya nchi za watu huko mbali ukizingatia ni hapo hapo tuu Dar-Mtwara

Mkuu bahati mbaya sana nipo katika uzalishaji na ujenzi wa miundo mbinu ya gesi asilia na mafuta ghafi baharini sehemu za Asia Pacific kwa kipindi kirefu.
Kwa kifupi ni kwanini ahadi ya punguzo la 50% limegeuka kuwa1%?
1.Yawezekana walijenga mitambo na miundo mbinu kwa kulenga wateja wakubwa kama viwanda vyakutumia umeme mkubwa,ambao nafikiri ni wachache sana kwa sasa.Lakini kasi ya kujenga viwanda vizito angalau 20 hadi 50 vitakavyozalisha BY PRODUCTS za gesi asilia au Gesi asilia ikiwa CHACHU ya viwanda kama Cement n.k
Wakiweza kufanikiwa kwa hilo wananchi wa kawaida matumizi yao ya umeme ni madogo sana watatoa hudumu hiyo karibu ya bure siku za mbeleni.
2.Sijui vizuri uhusiano uliopo kati ya-:
Mzalishaji gesi yaani mmiliki wa visima,
Msambazaji wa gesi kutoka kwenye visima hadi kwenye mashine za kufua umeme(gas pipeline)
Mfua umeme
Msambaza umeme
Utilili wa watoa hudumu yawezekana ukasababisha mkanganyiko kama hakupangiliwa vizuri kwa maslahi mapana ya mradi.
Labda ni inbox tunaweza kubadirishana mawazo mkuu
 
Back
Top Bottom