Bei ya mafuta ya kupikia yapaa!

Usisahau nyanya zilituozea huku ndani! Unaikumbuka sababu?
 
Hapo ndo ilipo tofauti ya maendeleo na wivu, kuwa saloon car sio luxury tena, kwa usafiri upi wa umma mpaka ufikiri hivyo? Bil 180 zingeweza kuongeza km ngapi za barabara? Unajengea daraja la upande mmoja! Ongeza road network.
 
Usisahau nyanya zilituozea huku ndani! Unaikumbuka sababu?

hapo pia tunataka mjitokeze wenye mitaji muwekeze katika viwanda vya kusindika nyanya badala ya kuuza raw nyanya. Kazi ya serikali ni kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji ikiwemo hiyo ya kuweka kodi kwenye bidhaa zinazotoka nje kwa bidha ambazo pia inazalishwa ndani ya nchi ili kuwalinda waliowekeza katika sekta hiyo. Ukiwekeza katika kusindika nyanya tutaweka kodo katika nyanya zilizosindikwa kutoka nje ya nchi maana wewe utakuwa umetoa na ajira na soko la uhakika kwa walukima wetu wa ndani.
 
Sukari ilivyopaa bei niliachana na chai, sasa wacha nianze kula chukuchuku tu hakuna namna.
 
Sina hakika kama hilo ndilo jibu!
 
tuna alizeti na viwanda vya kutosheleza?
 
Mbona tuna viwanda vya majani ya chai nchini lakini kawaangalie wakulima walivyochakaaa kiuchumi.Ishu ni kuwepo kwa ushindani bidhaa za nje zije na za ndani zishindane
 
Mbona tuna viwanda vya majani ya chai nchini lakini kawaangalie wakulima walivyochakaaa kiuchumi.Ishu ni kuwepo kwa ushindani bidhaa za nje zije na za ndani zishindane

fanya utafiti wa kutosha wa kulinganisha sub sector hizo mbili za Chai na Alizeti kabla ya kuhalalisha ubovu wa maisha ya wakulima wa mazao hayo. Alizeti kwa asilimia 99 inalimwa na wakulima wadogo wakati chai asimilia 99 ni inalimwa na wawekezaji ambapo wananchi ni vibarua. Hivyo mapato wakubwa ya Chai inaishia kwa wenye mashamba na wenye viwanda. Mkulima anaambulia wage ya kusustain ili aendelee kuwa kibarua. Kwenye alizeti hali ni tofauti. Mimi nimetoka Manyara, large share of the profit in Sunflower Value Chain goes to farmers compared to Tea industry.

Hiyo falsafa ya ushindani haiwezi kufanya kazi kwa nchi maskini kama yetu. Utashindanaje na Jitu kama Goliath wakati hata kilo 50 huna? Wakulima wa huko nje karibu kila kitu wapo subsidized na kilimo chao is very cheap due to technology.
 
Crude oil ni raw materials inazalisha
1. Mafuta ya kula
2. Siagi
3. Wahuni
4. Chanzo cha ajira kwa vijana

Je alizeti, ufuta na vyanzo vingine kutoka kwa wakulima vinatosha kulisha wananchi wote mwaka mzima?
 
Ni muhimu sana kwa viongozi wetu kuwa makini na kauli zao maana zinaathari sana aidha positive au negative kwenye maisha kiujumla maana huchukuliwa kama ndio tamko halali la serikali hata kama utekelezaji wake ni muda mrefu ujao

Wafanyabiashara hureact haraka kutokana na kauli hizo kwa kubadili supply yao ili waavoid hasara

Kwa hiyo inahitajika kufanyika utafiti wa kutosha kujua uwezo wetu wa ndani kwanza wa uzalishaji bidhaa kabla ya kiongozi kusema lolote linaloweza kupelekea shortage ya bidhaa husika ikiwa uzalishaji wetu ni mdogo na hivyo kuleta shida kwa wananchi kwa bidhaa husika kupanda bei
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…