BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Bei ya mafuta ya petroli imepanda leo Desemba 6, 2022 kwa asilimia 2 na kufikia dola 87.3 kwa pipa, saa chache baada ya kuanza kutekelezwa kwa hatua kadhaa za mataifa ya magharibi zinazolenga kupunguza mapato ya Urusi katika sekta yake ya nishati.
Ongezeko hilo limeshuhudiwa baada kuanza kufanya kazi kwa azimio la mataifa ya magharibi la kuweka ukomo wa bei kwa mafuta ya Urusi pamoja na marufuku ya Umoja wa Ulaya ya kuingizwa mafuta ya Urusi yanayosafirishwa kwa njia ya bahari.
Wanasiasa wa nchi za magharibi wanatarajia hatua hizo zitavuruga uwezo wa Urusi kifedha na kuilazimisha nchi hiyo kuachana na vita vinavyoendelea nchini Ukraine.
Hata hivyo tayari kuna wasiwasi kwamba uamuzi wa kudhibiti bei ya mafuta ya Urusi kwa hadi dola 60 kwa pipa, utapunguza kiwango cha nishati hiyo kwenye soko la dunia na kupandisha zaidi bei ya petroli.