Bei ya mafuta yashuka kwa 54%

Hapa kijijini kwangu bei ya petroli imeshuka kutoka $3.95 wiki chache zilizopita na sasa ni $2.49. Hata nimeanza kupunguza kutembea kwa mguukwenda kununua soda na bia.


Hapa kijijini kwangu kwenye vibanda vya BJ'S yameshuka toka $4 kwa galon wiki chache zilizopita na leo jioni ni $2.40.Nitaanza kuzurura upya kwenda kusoma JamiiForum kwa jamaa zangu walioko vijiji jirani kwani naona kusoma tena jamiiForum pekee yangu hainogi.Nitaanza kushindana na wasipainishi kupiga malesi kwenye kigari changu tukiwa mbioni kwenda kuvua samaki.
 
Mungu awape nini tena ndugu zetu wa ughaibuni? sisi hapa tz mwendo mdundo kwa kuwa kila kitu ni siasa, wahindi wanakutana jamatini wananchanga pesa kupekeka ewura, jamaa wa ewura wanadai kama bei ni kubwa tafuteni vito vinavyouza kwa bei rahisi
 
Hapa kijijini kwangu bei ya petroli imeshuka kutoka $3.95 wiki chache zilizopita na sasa ni $2.49. Hata nimeanza kupunguza kutembea kwa mguukwenda kununua soda na bia.

Jasusi,

Kweli ndio maana mnaenda kupiga Waarabu ili bei ya mafuta iendelee kuwa chini. Yaani $2.49 per gallon? Kwa wengine pia imeshuka lakini bado iko juu, imetoka £1.30 per liter
na sasa iko £1.07 diesel na petrol iko chini ya £1. Bado ni juu sana ukilinganisha na USA
 
Hehe na Vijiji vyengine haviko pedestrian friendly kabisa, linishajaribu kutembea sidewalk ikakatika ghafla ikabidi nigeuze!! Mtapata nafuu sasa.
 
Tanzania wafanyabiashara wa mafuta huwa wao ni faida tu. Ikipandishwa kodi ya mafuta tu, nao hupandisha mafuta, bila kujali kuwa wanatakiwa kumaliza mafuta kwanza ambayo yaliingia kabla kodi haijapanda. Pia Mafuta yakipanda tu katika soko la dunia, wao hupandisha bei wakati huohuo. Sasa yakishuka katika soko la dunia husema kuwa wanayo kibao wakishaagiza yako kwenye "sock" yao, hivyo hawawezi shusha bei mpaka yaishe.

Sijui kama EWURA wanajua kuwa BP, Oilcom nk kwamba wameingiza kiasi hani cha mafuta kwa mwezi, na ni rahisi kama mfuo ungekuwa wazi kujua wamesambaza kiasi gani kwa vituo vyao. Manake kuna mafuta yanaingizwa na kusemekana yanaenda Burundi, Rwanda ama Uganda, lakini yanaishia kuuzwa TZ, hakuna usimamizi, yani kila mtu anaendesha mambo atakavyo. INAUDHI mno!.
 
EWURA imetoa kipindi cha wiki 1 bei ya mafuta iwe imeshuka. Haruna Masebu anasema bei imeshuka kwa kiwango kikubwa hivyo basi wauzaji wa mafuta sharti washushe bei
 
Bora watanzania tutapumua kidogo, maana kila kitu kilikuwa bei juu kwa sababu ya bei ya mafuta kuwa juu, nadhani sasa na na ukali wa bei nao utapungua.

Swali je MADALADALA nayo yatashusha bei????
 
EWURA imetoa kipindi cha wiki 1 bei ya mafuta iwe imeshuka. Haruna Masebu anasema bei imeshuka kwa kiwango kikubwa hivyo basi wauzaji wa mafuta sharti washushe bei

Usitake nicheke! wasiposhusha bei ana ubavu wa kuwafanya chochote?
 

Karibu mwezi unaisha tangu mafuta yashuke bei na jana yameshuka zaidi. Ajabu lakini hapa Tanzania mafuta bado bei iko juu na na haijashuka hata kwa 25% hasa Dar es salaam bei ni juu kuliko mikoani yaani utaifikiri Tanzania kuna Vijamuhuri vingine! Ewura wamenyoosha mikono limewashinda (Nashauri Ewura ifutwe maana hawana faida kesi wanashindwa na tunauziwa mafuta machafu wkati tunalipa 1% kwenye umeme kwa ajili yao) na Serikali yetu imeuchuna (sijui maisha bora yatatoka wapi, maana hiyo ilikuwa ni golden chance hata ya kuwadanganya WaTz kwa muda).

Maoni yangu:
nahisi kwenye biashara ya Mafuta hapa nchini kuna Mafisadi wanaimiliki na wameiweka Serikali mifukoni mwao kwa gharama ya watanzania.
 
Price ya mafuta sasa iko kwenye exactly price. Speculator walikuwa wanacheza na demand and supply kwa kubid kwenye future delivery za mafuta. Kwa dolla 60 a barral still makampuni ya mafuta wanamake good profit.

Kuhusu Tanzania huwezi kuona changes mara mmoja, sababu supply wengi wa mafuta nchini Tanzania wana hold inventory, kwa hiyo huwezi kuslash price wakati ulinunua kwa high price. However, sababu tuna loophole nyingi basi hata kama kampuni itaingiza inventory mpya inaweza kumanipulate bei na hakuna atakae wababaisha.

Kama tungekuwa na refinery zetu, basi tungekuwa tunaona changes mara moja. Na kama tungekuwa na viongozi wenye brain, tungebana loophole za hawa kina Ally Yushumu na waarabu wenzie wanao supply Blood oil nchini kwetu.
 


Mkuu haya uliyosema ni facts.

Niongezee senti zangu mbili...kwenye hili la mafuta ya Burundi na nchi nyingine za jirani kuuzwa TZ. Ufumbuzi wa hili ulishagunduliwa na mafuta ya kwenda nchi hizo siku hizi yanakuwa na rangi tofauti. Ili kuyafanya yatambulike kirahisi yakiwa sokoni Tanzania (kwenye vituo vya mafuta). Sasa sina uhakika iwapo hiyo rangi inawekewa hapo Tanzania huwa yanakuja TZ yakiwa tayari yameshawekwa.

Tatizo linakuja Je, watanzania wanalifahamu hilo. Iwapo siku wakijikuta wanauziwa Petroli ya Blue watajua kuwa hii haijalipiwa kodi? Na wakisha jua wanatakiwa kufanya nini?
 
Mimi nafikiri serikali inajuana na hawa wauzaji wa mafuta nchini kwanini basi bei za nauli kwa walalahoi isipungur anagalau wakajinasua kwenye huu umasikini? Hivi kweli haya ndio maish bora kwa kila mtanzania?
 
Ewura wamenyoosha mikono limewashinda (Nashauri Ewura ifutwe maana hawana faida kesi wanashindwa na tunauziwa mafuta machafu wkati tunalipa 1% kwenye umeme kwa ajili yao) na Serikali yetu imeuchuna (sijui maisha bora yatatoka wapi, maana hiyo ilikuwa ni golden chance hata ya kuwadanganya WaTz kwa muda).

Mkuu Ibrah haya maneno ni mule mule kabisa.....!

Inashangaza sana kwa kweli! Hawa EWURA mimi nawalinganisha na Bodi ya mikopo, hivi vyombo naona vimeundwa kwa maslahi ya kisaisa zaidi kuliko kiuchumi na kijamii!

Kwanza, hivi hawa EWURA kwenye maji na mafuta huchukua fees kama 1% ya TANESCO? Kama wanachukua chochote basi hii mamlaka haina maana yoyote kuwepo, kwasababu itakuwa na migongano ya maslahi''conficts of interests'' cause km ilivyo kwa Tanesco wanachukua 1% ya mauzo which means the earnings are directly proportional to the mauzo, yaani kadiri bei inavyo kuwa kubwa ndivyo revenue inaongezeka na ndivyo 1% yao inakuwa kubwa hivyo hivyo!

Kwahiyo kwa mtindo huo, uwepo wa chombo hiki hapa TZ hauna maana yoyote ile, tena ni bora miaka minne iliyopita wakati ambapo hatukuwa na EWURA!
 

Nadhani tatizo linakuja sababu wasambazaji wengi wa mafuta Tanzania wana hold inventory kwa muda mrefu. Ili kuona changes soon inatakiwa tuwe na system kama ya just in time, yaani una order then supply nae ana order kisha ana deliver. Lakini huwezi kufanya kitu kama nchi Tanzania sababu watu wanaweza kumaliza mwezi hawajapata mafuta sababu ya poor infrastructure.

Hata hivyo, serikali yetu haiana watchdog ambao wanaweza kuangalia kama wasambazaji wa mafuta wana manipulate price. Watanzania bado tumelala, wachache ndio tuna idea kwamba mafuta yameshuka kwenye world market, lakini OIL com wanauza kwa bei ya juzi.
 
Ni vigumu mno kukontrol bei ya mafuta kama huna refinery na sisi kwa sababu ya ufala wetu tumeua ile tipper (Well I am not sure iwth the story behind). Halafu kuna hii biashara ya soko huria where by kila mtu anaagiza mafuta anakokujua na therefore kusema I bought at this $$$$$$$$$$ Tukumbuke kwamba biashara ya mafuta Tanzania haina ushindani ni some sort of a cartel........ Just imagine nchi nzima ina vituo kama 1200 na kati ya hivyo around 280 vipo Dar.
 

That is why we are saying, under those circumstances gvt's intervention was necessary! And it should have done that through its teethless EWURA!!
 

Muungwana, si kweli. Napenda kukwambia kuwa kituo cha mafuta hakiwezi kukaa na inventory ya mafuta kwa zaidi ya mwezi, ikiwa hivyo hicho kitio lazima kifungwe fanya utafiti utaona. Napenda kukwambia kuwa hakuna biashara inayokwenda haraka kama mafuta na demand yake inazidi kila siku. Juzi nlikuwa nafutailia namba ya gari lamgu TRA jamaa yangu anayenisaidia akaniambia imechukua muda (wiki moja) kwa kuwa ndani ya wiki mbili kuna meli zimetema magari 2500 pale Dar Port!

Na kama madai ya inventory kutosiha mapema mbaona bado tumeshuhudia bei ya mafuta kushuka lau kidogo mikoani na sio Dar (kumbuka kuwa mafuta mengi yanashushiwa Dar). Ni ufisadi tu ndiyo unaosababisha bei kutoshuka na naamini Serkali haijachukua hatua madhubuti ya kuwaita importers wa mafuta ili wa-justfy kwa nini bei haishuki nchini. Ni juzi tu Mkuu mmoja wa Serikali amekanusha sababu za Waagizaji mafuta kuwa na extra inventory kweny vituo vyao na akasema haya nayokwambia kuwa mafuta hayakai muda mrefu bila kuisha. Kuna kituo fulani vha mafuta huku Arusha kiko nchi ya mji kama km 15 kila wiki kinaleta mzigo wa mafuta pale inagwa vituo vingi vilivyopo mjini bei iko juu kuliko kituo hicho. NI UFISADI TU AMBAO UNAFUNGIWA MACHO NA SERIKALI YETU. LABDA NI EPA YA UCHAGUZI WA 2010, SI WAFANYABIASHARA HAWA WA MAFUTA WATAWACHANGIA PESA ZA UCHAGUZI?
 
Hivi
Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC)
wanasimama wapi juu ya hili?..

ufisadi tu nasikia wakubwa ndo wanaosababisha hili shirika lisianze kazi wanaingiza mafuta yao sasa litawazibia riziki mhhh!
 
ufisadi tu nasikia wakubwa ndo wanaosababisha hili shirika lisianze kazi wanaingiza mafuta yao sasa litawazibia riziki mhhh!

Duu, ubinafsi usio fikrika! Yaani mamilioni ya watanzania tunateseka kwa kupanda garama za maisha kwa ajili ya vi fisadi visivyo zidi hata miamoja?
 
CNN Breaking news: Oil dips below $50 a barrel on New York exchange for the first time since reaching record high of $147 in July.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…