Bei ya mahindi kwa sasa

Bei ya mahindi kwa sasa

Gwallo

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Posts
3,408
Reaction score
4,392
Wanabodi habari za leo!

Naomba niende kwenye mada moja kwa moja, nimelima mahindi na nikayahifadhi store maguni si mengi kama 200 hivi. Je kuna mdau yeyote anayejua bei ya kilo ni Shilingi ngapi kwa sasa kwenye eneo lako ulipo?

Kwa Mkoa wa Arusha na maeneo mengi ya Wilaya zake bei ina-range kati ya 50,000-60,0000 kwa gunia. Je hapo kwako bei ikoje?
 
Singida 60,000 hadi 70,000.

Mkuu ulilima heka ngapi ukapata gunia 200?
Asante sana mkuu kwa feedback hii.

Ilikuwa ni eka 25 kwa ujumla ilizidiwa sana na Mvua za Mwaka huu na wale wadudu waitwao kanitangaze....
 
Nami najichimbia shamba nikakomae na mhind msimu huu kiteto.
Mkuu naomba kukuuliza mashamba kiteto yanaanza kuandaliwa Muda gani nina trekta mwezi December mwishoni inaelekea Kilindi kupitia Kiteto ....je naweza kupata kibarua ya kulima mashamba kwa wananchi?
 
Gunia la debe ngapi mkuu? Au tuseme debe wanauza sh ngapi?
Wanapima kwa kilo. Kiloba kimoja chenye kilo 120 wananunua kwa elfu 72,000.

Kilo zikizidi bei hiyo inaongezeka, au kilo zikipungua wanagawnya ili kupata bei halisi ya mzigo wako.
 
Wanapima kwa kilo. Kiloba kimoja chenye kilo 120 wananunua kwa elfu 72,000.

Kilo zikizidi bei hiyo inaongezeka, au kilo zikipungua wanagawnya ili kupata bei halisi ya mzigo wako.
That means debe litacheza kati ya 10,000/- hadi 12,000/- bado sio bei mbaya japo mwaka bei za mazao ziko chini sana sijui shida nini; mpunga ndo umegoma kabsa kupanda
 
Mkuu naomba kukuuliza mashamba kiteto yanaanza kuandaliwa Muda gani nina trekta mwezi December mwishoni inaelekea Kilindi kupitia Kiteto ....je naweza kupata kibarua ya kulima mashamba kwa wananchi?
Asilimia kubwa wanaanza december mwishoni had january,nafikiri utakuwa mda sahihi.
Nikishaingia kiteto mid december nitakutafuta tuyajenge.
 
Asilimia kubwa wanaanza december mwishoni had january,nafikiri utakuwa mda sahihi.
Nikishaingia kiteto mid december nitakutafuta tuyajenge.
Nitashukuru sana Mkuu...
 
Asante sana mkuu kwa feedback hii.

Ilikuwa ni eka 25 kwa ujumla ilizidiwa sana na Mvua za Mwaka huu na wale wadudu waitwao kanitangaze....
Mbona huyu Kantangaze au kitaalam tita absoluta huathiri nyanya,vitunguu hoho na viazi? Labda mdudu mwingine.
 
Back
Top Bottom