Bei ya mahindi nchini inasikitisha

Bei ya mahindi nchini inasikitisha

Fanya unga. Utalipa zaidi.

Signature yako hujaikosea unaitendea haki.

Kuna mengi ya kujifunza kutoka kwako. Ushauri wako kwa mtu makini ni wa thamani sana! na huenda ikawa ni mwanzo wa kubadili maisha ya watu hapa. Ubarikiwe.
 
tunataka bei ifike mpaka sh.700-800 kwa kilo then gunia iwe kati ya 70 to 80,000 tsh per gunia tofauti na sasa kg 400 wakati ulinunua sh.480 kwa kg

bei ya leo tandale ni sh. 500 per kilo kwa mahindi ta dodoma na sh. 450 kwa mahindi ya iringa

na kwa mombasa/nairobi ni sh 600 per kilo.

Mind you soko kubwa la unga wa kenya lilikuwa south sudan, baada ya machafuko biashara haipo ndio maana mwaka huu soko limeyumba
 
Mahindi km we ulinunua ili uje uuze kw bei kubwa hailipi..ila km we n mkulima mahndi bdo yanalipa kwa hzo bei
 
wadau naomba kuuliza , baada ya kukoboa na kusaga, kilo moja ya mahindi ya dodoma yanaweza yakatoa unga kiasi gani?
 
kwa kweli bei inasikitisha mkuu katika wilaya ya mbozi leo nimetembelea sokon nimekuta bei mpya ya mahind mapya kwa gunia ni sh 27000/= sasa kwa mtindo hii kilimo kinaweza mkomboa mtanzania kweli.wakati gharama za uzalishaji kuanzia mbolea,madawa na gharama za kulimia ziko juu mno!!!
 
yaani mkuu juzi nimetembea kucheki ya shambani yamestawi vizuri huku ya mwaka jana yamedoda stoo ni hatari sana mengine tulinunua kwa hela za mikopo
Asante Mungu kwa kustawisha mazao ili tuweze kuwa na chakula cha kutosha!!!:smile-big:
 
Wakuu ni masikitiko makubwa kwa wajasiriamali wote waliohifadhi mahindi ghalani kwa kuwa mwaka huu hakuna bei kabisa na inaonekana kuna chakula cha kutosha pia katika mizunguko yangu katika mikoa mbalimbali nimeona mahindi yamestawi vizuri sana; sasa wadau kwa nini serikali isiruhusu wafanyabiashara kuuza nje? na kwenye mashirika kama WFP wakapeleke Somalia na CAR? kwa kweli inasikitisha kwani mipango ya wengi inakwama
hata mchele bei iko chini sana,naona biashara ya nafaka imeloga hii miaka mitatu
 
suala siyo kukataliwa kuuza the big deal hapa ni bei, gharama za kilimo haziendani na Bei kwa waliotunza baada ya kununua kwetu sisi wakulima sijui ila mimi mkulima nasema gharama za kilimo ni kubwa sana ukilinganisha na unachokipata.
 
Huku kigoma kasulu wanauza kwa bakuli 1 =1.5kg kwa 300 mpaka 250
 
Back
Top Bottom