Bei ya mazao ikoje katika mkoa unaoishi?

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Nipo Iringa inavyoelekea mwaka huu Mahindi hayashikiki. Ikiwa ni kipindi cha mavuno(June -July), bei ya debe inacheza kati ya elfu 13 hadi 14. Lita ya mafuta ya alizeti ni kati ya 5000 na 5500. Mchele safi 2000. Lete updates ya huko uliko hali ipoje?
 
wilaya ya masasi- mtwara bei ya mahindi debe tsh elfu 10.
 
Morogoro mpunga gunia debe 7 80,000
 
Simiyu debe la mahindi elfu 15, mpunga gunia debe sita elf 90000
 
Hivi yule jamaa alieanzisha uzi wa gunia la mahindi kuwa 180k, yeye alisema yupo mkoa gani?
 
Kwakweli mwaka huu ni balaa mfano kwa kilombeeo debe moja la maindi ni tsh elfu 13 wakati mwaka jana muda kama huu ilikuwa ni sh elf 7.
debe la mpunga ni tsh elfu 13 hadi 14 wakati mwaka jana mwezi june tulinunua tsh elf 5 hadi elf 6 na hapo kuna muindi(mfanyabiashara) yeye ananunua mpunga kwa kilo (kilo moja tsh 900).
Rais samia asipoingilia kati suala hili kwa kufunga mipaka tutarajie njaa kali saana maana na mwaka huu mvua haikunywsha ya uhakika.
Mchele supa tsh 2000.
sabuni ya kipande jamaa tsh 800.
Mafuta ya kula lita moja tsh elfu 7500.
Mafuta ya petrol tsh 3057.
 
Nimependa sana uchambuzi wako
 
Sisi tuliolima tufurahia bei kuwa juu zaidi alafu wewe unataka mteremko?.Acha wakulima na sisi tuneemeke,tulivurugwa sana huko nyuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…