Bei ya mbolea: Waziri Bashe amepotosha Bunge na kushangiliwa kwa kelele tu

Hiyo graph Ina interval ya miaka miwili miwili, ilianza kupanda 2021. Lakini pia Ni ukweli Bei ilianza kupanda baada ya bajeti mpya ya 21-22, sijui mliweka nn huko
 
Tender ya manunizi ya mbolea yote imewekwa wazi kwa yule atayeweza kumpelekea Bashe nchi ambayo mbolea ipo bei chini.
Kachukue tender hiyo mkuu upige pesa.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Bashe nae ni kama haelewi, mfumo wa kuagiza pamoja Kama kwenye mafuta si waliufuta. Sasa hiyo tender anampa Nani ikiwa kampuni zinaagiza zenyewe kulingana na bajeti zao
 
Ili ueleweke vizuri,ungefafanua kwa kutumia jedwali linalooneshe Mwaka na Bei na Mwaka ambao Corona na Vita vya urusi vimeanza. Otherwise graph itasumbua wengi
 
Miaka 60 ya Uhuru nchi ya wakulima hutana viwanda vya mbolea vinavyoeleweka ni aibu kubwa sana
 
Bei imeanza kupanda July mwaka Jana, na ilitoka 50k na kwenda 70k.
Kuhusu kwa nn sasa ipo 150k, bashe anajua anachofanya nyuma ya pazia
Ukiangalia hiyo graph huoni kama bei imepanda? Au unafanya kusudi
 
2008 shipping ilikuwa very cheap kulikuwa na crisis au recession duniani leo shipping ni mara 4 kutoka mwaka jana, container labda mwaka jana lilikuwa dola 2000 leo sio chini ya dola 6000 mambo mengine bei zinachangiwa sio na commodity tu ila shipping na other factors.
 
Unaona vizuri kweli? Hiyo graph ni ya interval ya miaka miwili miwili. Na hapo inaonyesha 2020 ilishuka zaidi na 2021 ilipaa sana. Sababu za waziri ni Vita ya Ukraine Ila 2021 hakukua na Vita
Hoja ya msingi ya Bashe ni kwamba Mpina anadai nchi jirani za Rwanda, Malawi na Zambia bei ya mbolea ni chini kuliko sisi kwa sababu ya rushwa na upigaji uliopo. Bashe amejibu vizuri tuu kwamba ni kweli kabisa hizo nchi bei ya mbolea iko chini but kwa sababu zinatoa RUZUKU kwenye mbolea wakati sisi hatutoi.. Na akasema kwa trend ilivyo sasa kama serikali haitotoa ruzuku kwenye mbolea basi tusitegemee mbolea kushuka bei.
 
Sasa hiyo ni personal... Pambana na hoja zake...
 
Bei imeanza kupanda July mwaka Jana, na ilitoka 50k na kwenda 70k.
Kuhusu kwa nn sasa ipo 150k, bashe anajua anachofanya nyuma ya pazia
Acheni upuuzi, unataka ufananishe Dollar 1000 ya 2008 na Dollar 1000 ya 2022?
 
Unajua watu ni wajinga au wanachuki zao binafsi. Kwa nadharia ya kawaida kabisa, huwezi kufananisha dola 100 ya 2008 na dola 100 ya 2022. Kwahiyo kufananisha bei ya 2008 na 2022 ni kujidanganya.
 
Tuangalie suala hili zaidi ya Waziri kupotosha. Hali halisi ni kwamba bei ziko juu. Tunachotakiwa kujadili ni kama bei hizo zitashawishi wakulima wengi kutumia mbolea au vipi. Na kama watafanya hivyo bei za vyakula zitakuwaje na zitapokelewaje na walaji kama kwenye tozo tu kelele ndivyo hivyo.
 
Bashe amewaambia nyie vibwengo nendeni mpewe vibali vya kuleta mbolea ya Bei rahisi badala yake mnaharisha mausaha yenu hapa .
 
Bashe nae ni kama haelewi, mfumo wa kuagiza pamoja Kama kwenye mafuta si waliufuta. Sasa hiyo tender anampa Nani ikiwa kampuni zinaagiza zenyewe kulingana na bajeti zao
Kwanza ulisikiliza majibu yake Bashe kwenda kwa Mpina?.Mimi nimekazia tu maelezo yake.
 
Nafikiri hii ndio sababu kuu ya vitu kupanda bei

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Umeielewa hizo graph vizuri? Au umechangia tu maneno
 
Nafikiri hii ndio sababu kuu ya vitu kupanda bei

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Hii ndio ukweli na nimejaribu kuuliza ni kwanini kuna mtu anafanya kwenye sector hii anasema kuna uhaba mkubwa wa ma containers duniani na sababu kuu wakati wa corona China walichukuwa asilimia kubwa ya containers duniani empty china kwa hiyo haya machache duniani tunayagombania yaani demand and supply. China ndio kasababisha yote haya kusafirisha toka China ni rahisi kuliko nchi zingine duniani, lakini hali baade itarudi sawa katika usafirishaji. Na rafiki yangu Dubai anasema alikuwa anapeleka container Nigeria kama dola 2500 leo mpaka dola 8000.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…