Nadhani wafanyabiashara wengi huwa hawanunui mchele kama mchele bali mpunga na kisha kuukobolesha kupata huo mchele.
Kwa Mbeya sina uhakika lakini Ifakara (ule mchele wa kunukia sana) bei yake ni sh. 50,000/= kwa gunia la debe 6.
Kiufupi ni kwamba kipindi hiki biashara ya mpunga/mchele sio dili sana kwani umejaa sana kwa wakulima na bei yake iko chini sana. Nadhani serikali ilizuia kupeleka nje.
Labda kama una sehemu ya kuhifadhia basi waweza nunua mpunga mwingi sana ukauhifadhi then miezi michache ijayo bei ya mchele itakuwa juu sana, kwani watu ndio watakuwa wanalima (Msimu wa kilimo bei za vyakula huwa juu sana).
Hapo waweza piga faida kubwa.