Bei ya nyumba za kulala wageni Kampala zikoje kwa sasa?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Heri ya Krismas na mwaka mpya!

Wiki ijayo nitakuwepo Kampala, na ninatarajia kuwepo huko kwa siku kadhaa!

Tafadhali mliopo huko, na hata kwingineko wenye "taarifa" mnisaidie yafuatayo:

1. Bei za nyumba za kulala wageni(za kawaida, siyo za kifari), zina kawaida ya kubadilika mwishoni mwa mwaka?

2. Usalama ukoje kwa nyumba za kawaida za kulala wageni hasa mwishoni mwa mwaka?

3. Naweza kutajiwa lodge za bei rahisi lakini salama kwa jiji la Kampala?

4. Nauli ya kutoka Mutukula hadi Kampala ni sh ngapi kwa sasa? Mara ya mwisho kusafiri pande hizo ilikuwa ni December 2023, nililipa Ush 30,000 kutoka Kampala hadi Mutukula. Kuna mabdaliko ya nauli?

5. Taarifa zingine zozote za kusaidia "will be appreciated"🙏🙏🙏
 
Mkuu kulala Hotel za chini taifa la kigeni ni kutuwakilisha vibaya , unaharibu image ya taifa haswa kwa taifa la wala bata kama Uganda😁😁😁😁
Nashukuru kwa maoni yako mkuu, lakini siendi kutalii mkuu! Naenda kwa jambo la muhimu sana, na sijui itanichukua muda gani kulifanikisha, hivyo ninataka kubana matumizi kwa kadiri iwezekanavyo!

Nitakapoenda awamu nyingine, nitafikia hoteli nzuri kama SERENA HOTEL au HILTON HOTEL, hoteli ambazo hata hapa nyumbani bado sijatia mguu. Mwakani nitalala kwenye hizo hoteli!
 
Oooh sawa mkuu kapige kazi kila la heri .
 
Totoz za huko kama za Bukoba tu water table iko juu, ndiyo maana hotel lazima magodoro yawekewe mipira yasiloane.
 
Nashukuru kwa maoni yako mkuu, lakini siendi kutalii mkuu! Naenda kwa jambo la muhimu sana, na sijui itanichukua muda gani kulifanikisha, hivyo ninataka kubana matumizi kwa kadiri iwezekanavyo!

Nitakapoenda awamu nyingine, nitafikia hoteli nzuri kama SERENA HOTEL au HILTON HOTEL, hoteli ambazo hata hapa nyumbani bado sijatia mguu. Mwakani nitalala kwenye hizo hoteli!
Ni furaha kwa kila mtu Siku mtu akifungua mlango wa Five star⭐ hotel 😊
 
Nawashukuru wote mliotoa maoni yenu. Nilishafika Kampala kitambo. Maisha ya Kampala siyo gharama sana. Kuna gesti mpaka za Ugx 13,000, ila za bei hiyo
1. Zipo nje ya mji
2. Ni single (siyo self contained)
 
Watoto wa 2000 vipi huko? Hujakamata mmoja?
 
Nawashukuru wote mliotoa maoni yenu. Nilishafika Kampala kitambo. Maisha ya Kampala siyo gharama sana. Kuna gesti mpaka za Ugx 13,000, ila za bei hiyo
1. Zipo nje ya mji
2. Ni single (siyo self contained)
Kwani chumba kuwa cha single ni lazima kisiwe self contained?
 
Ni l"ugha" ya mtaani kwetu, kwamba single ni chumba kilocho peke yake (hakina sebule wala choo cha ndani) wakati double inaweza ikawa ni ama self au kina sebule na chumba cha kulala.
 
Ila mimi nijuavyo chumba cha single (single bedroom) ni kile chumba ambacho ndani yake kutakuwa na kitanda cha wastani ambacho kinafaa kulaliwa na mtu mmoja na bado chumba hicho kinaweza kuwa self contained kama ni lodge ya kueleweka au hotel au kikawa siyo self contained kutegemea na ubora wa lodge. Na chumba cha double (double bedroom) ni chumba ambacho ndani yake kuna kitanda kikubwa cha kutosha kulala watu wawili au wakati mwingine ndani ya chumba hicho kunawekwa vitanda viwili tofauti. Si ajabu ukakuta hicho "chumba cha double" kwenye lodge za kawaida na hotelini zikawa self contained au siyo self contained kwenye hizi lodge za bei chee. Issue ya chumba kuwa single bedroom au double bedroom kiufupi inahusiana na ukubwa wa kitanda au idadi ya vitanda iliyomo ndani yake na haina uhusiano na self containment.
 
Back
Top Bottom