Bei ya Petrol Ngara yafikia 5000 kwa lita. Mamlaka ya Maji yashindwa kutoa huduma

Bei ya Petrol Ngara yafikia 5000 kwa lita. Mamlaka ya Maji yashindwa kutoa huduma

Wafanyabiashara hawajaishiwa mafuta wameyaficha maana jumatano EWURA watatangaza bei mpya ambayo ni ya juu kwahiyo wenye mzigo wa zamani wataongeza faida maradufu. Huu mchezo mbona mdogo sana mnashindwa kuelewa.
 
Hamna picha?
Hiyo ni bei ya ulanguzi kutokana na tatizo la uhaba wa Mafuta,Sasa itakuwaje na picha!? Ukitaka bei ya Serekali ndiyo unajibiwa kuwa hakuna mafuta,lakini ukikubali bei ya Ulanguzi unapewa Mzigo bila shida!!
 
Wilaya ya Ngara mkoani Kagera inakumbana na changamoto ya ukosefu wa bidhaa ambapo sasa lita moja ya Petrol inauzwa tsh 5000.

Wakati hayo yakijiri, mitambo ya kusuma maki imezimwa kwa siku tano sasa kutokana na upungufu wa umeme.

Kwa upande wa mafuta ya magari, vituo rasmi vya kuuza bidhaa hiyo havina petrol tangu juzi, hivyo wajanja wamechukua fursa hiyo kujineemesha.

Wafanyabiashara wajanja wameyafuata Burundi na kuyauza wilayani ngara kwa bei ya tsh 5000 kwa lita.

Wauzaji wa mafuta wanadai kuishiwa bidhaa hiyo wakidai yatafika jumapili wiki hii.

Aidha, mamlaka ya maji ya Mjini Ngara imetoa tangazo kupitia Radio kwizera kuwa haiwezi kusuma maji kutokana na umeme mdogo usio weza kusukuma mitambo hiyo

Kadhalika TANESCO kama kawaida hawajatoa taarifa ingawa inadaiwa kuwa kuna hitilafu katika mitambo yake
Teremkeni hapo kobero mkanunue petrol kwa bei poa ila diesel ni mziki kuipata kwa huko Burundi.

Mafuta yanapanda bei kuanzia jumatano ya terehe 6 hivyo ni watu wanafanya kutokuyauza kwa sasa ili faida iwe mara 2.

Poleni sana ndugu zangu wa ngara,benaco,shanga,rulenge na kabanga.
 
Mna-act
Hiyo ni bei ya ulanguzi kutokana na tatizo la uhaba wa Mafuta,Sasa itakuwaje na picha!? Ukitaka bei ya Serekali ndiyo unajibiwa kuwa hakuna mafuta,lakini ukikubali bei ya Ulanguzi unapewa Mzigo bila shida!!
Mna-act very weird mmezoea mapigano ya msituni Kama ndugu zenu Burundi
 
Hii ni chai maharage kwa sababu warundi wenyewe hawana mafuta yameadomika labda Burundi ya Ukraine
 
Wingu limetanda,
Limetanda.
Na kutughubika ghubi,

Mvua,
Lakini hainyeshi,
Hainyeshi,
Ukame umetanda waa!

Nimeikumbuka mistari ya shairi la Wingu kutoka kwa Mohamed S. Khatib
 
Teremkeni hapo kobero mkanunue petrol kwa bei poa ila diesel ni mziki kuipata kwa huko Burundi.

Mafuta yanapanda bei kuanzia jumatano ya terehe 6 hivyo ni watu wanafanya kutokuyauza kwa sasa ili faida iwe mara 2.

Poleni sana ndugu zangu wa ngara,benaco,shanga,rulenge na kabanga.
Bila kuisahau Murgwanza, mukanywampezi, muchinyiri-runzenze na mukagugo
 
Sasa nyie mmepandisha kabla ya bei mpya ya chief hangaya,

Nyie mtanunua lita sh elf 15 bei mpya ikija
 
Waituu masibota!
Tuko bize kumpongeza Kinana tukimaliza tutalishughulikia!
 
Sema Waangaza watu watata lakini Good-hearted tofauti na Wasomire sifa Kama zote
 
Hili la mafuta ni la kidunia kwa sasa tusinyooshene vidole hata ukiangalia nchi za jirani kama zambia nao wanalia .Tuombe Mungu mzozo wa urusi na uirein uishe haraka .
 
Back
Top Bottom