Bei ya Petrol Ngara yafikia 5000 kwa lita. Mamlaka ya Maji yashindwa kutoa huduma

Wafanyabiashara hawajaishiwa mafuta wameyaficha maana jumatano EWURA watatangaza bei mpya ambayo ni ya juu kwahiyo wenye mzigo wa zamani wataongeza faida maradufu. Huu mchezo mbona mdogo sana mnashindwa kuelewa.
 
Hao watu wa Ngara watata Sana. Sijuagi kwann
😄😃😀😁😆😅🤣😂😆😁😄😃😀Nilifika Ngara Na Kayanga Ukiwaona Hawafanani Na Utata Lakini Ukweli Ni Full Watata
 
Hamna picha?
Hiyo ni bei ya ulanguzi kutokana na tatizo la uhaba wa Mafuta,Sasa itakuwaje na picha!? Ukitaka bei ya Serekali ndiyo unajibiwa kuwa hakuna mafuta,lakini ukikubali bei ya Ulanguzi unapewa Mzigo bila shida!!
 
Teremkeni hapo kobero mkanunue petrol kwa bei poa ila diesel ni mziki kuipata kwa huko Burundi.

Mafuta yanapanda bei kuanzia jumatano ya terehe 6 hivyo ni watu wanafanya kutokuyauza kwa sasa ili faida iwe mara 2.

Poleni sana ndugu zangu wa ngara,benaco,shanga,rulenge na kabanga.
 
Mna-act
Hiyo ni bei ya ulanguzi kutokana na tatizo la uhaba wa Mafuta,Sasa itakuwaje na picha!? Ukitaka bei ya Serekali ndiyo unajibiwa kuwa hakuna mafuta,lakini ukikubali bei ya Ulanguzi unapewa Mzigo bila shida!!
Mna-act very weird mmezoea mapigano ya msituni Kama ndugu zenu Burundi
 
Hii ni chai maharage kwa sababu warundi wenyewe hawana mafuta yameadomika labda Burundi ya Ukraine
 
Wingu limetanda,
Limetanda.
Na kutughubika ghubi,

Mvua,
Lakini hainyeshi,
Hainyeshi,
Ukame umetanda waa!


Nimeikumbuka mistari ya shairi la Wingu kutoka kwa Mohamed S. Khatib
 
Bila kuisahau Murgwanza, mukanywampezi, muchinyiri-runzenze na mukagugo
 
Sasa nyie mmepandisha kabla ya bei mpya ya chief hangaya,

Nyie mtanunua lita sh elf 15 bei mpya ikija
 
Waituu masibota!
Tuko bize kumpongeza Kinana tukimaliza tutalishughulikia!
 
Sema Waangaza watu watata lakini Good-hearted tofauti na Wasomire sifa Kama zote
 
Hili la mafuta ni la kidunia kwa sasa tusinyooshene vidole hata ukiangalia nchi za jirani kama zambia nao wanalia .Tuombe Mungu mzozo wa urusi na uirein uishe haraka .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…