Andre02150
JF-Expert Member
- Feb 2, 2010
- 332
- 129
Saruji (cement) imepanda ghafla hadi kufikia 12,500 kwa mfuko wa kilo 50. Wiki 2 zilizopita, bei ya saruji ilikuwa 9700 kwa mfuko. Wafanyabiashara wamekuwa wakihusishwa kupanda kwa bei na kusimamishwa kwa shughuli za uzalishaji katika kiwanda cha Dangote-Mtwara. Ni vyema mamlaka husika za serikali zikatupia macho hali hii kwani kupanda kwa saruji kwa takriban asilimia 30 imatuumiza sana sisi walaji (consumers)