Bei ya Umeme kupanda kwa asilimia 50 kuanzia January 2013

Uswe

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
2,204
Reaction score
627
taarifa kutoka vyanzo vyangu vya kuaminika bei ya Umeme itaongezeka kwa asilimia 50 kuanzia mwezi wa kwanza.

Sababu inayotajwa ni gharama kubwa ya kuendesha shirika, kwa kiasi kikubwa bei hii huchangiwa na umeme ambao TANESCO inabidi inunue kutoka makampuni mengine.

My Take
Ingekua bora kama TANESCO wangejikita katika upunguza gharama zao za uendeshaji kwa kuzalisha wenyewe umeme wa bei nafuu kuliko kukimbilia tu kutupa mzigo kwa walaji
 
Hahaha hawa jamaa wa capacity charge wanarudi tena du mwaka huu ntanunua sola niachane na mambo ya dwasco sasa.Sie tunajilemaza tu lakini kusema ukweli kuna sola nzuri na zinazofaa kuliko hiyo tanesco yao
 
as long as lami zimejengwa...wadanganyika watatoa kura zao 2015
 
Duh! Juzi bungeni wamesema wanateremsha leo vyanzo lengwa vinasema inapanda!

Ama kweli ccm janga kwa Taifa.
 
This was to be expected,ndilo shirika pekee la uma linalo mo-nopolise soko lake hivyo wajanja wachache kuwa na uhakika wa kuchota mamilioni pasipo tatizo.While a small and unstable country like Ethiopia produces 10,000MW while their power demand is not more than 2000MW,We have failed even to reach our demand since independent and now we are negotiating to purchase power from Ethiopia. Just think,most of our power stations like Hale,Kidato,Nyumba ya mungu were constructed few years after indepent,since that time havent they generated enough capital to be re invested in other sources?Hydro power is the CHEAPEST but unreliable due to weather YET we cant afford that.Running cost will always be high.Dont expect the same people managing the same company to come up with new ideas.Chukua hatua................
 
sioni faida ya TANESCO kuendelea kuwa shirika la umma
 
kuna haja gani la hili shirika kuwa la UMMA wakati haliwatendei haki UMMA wenyewe,kuna haja kwa hili shirika KUBINAFSISHWA au kuruhusu wadau wengine nao wazalishe UMEME ili kuleta ushindani na kupunguza bei kwa WALAJI
 
tuna mpango kamambe wa kuhama kabisa na umeme wa tanesco,ni uhuni wa hali ya juu
 
Wataua..Hapa tu watu tunalia je wakiongeza

hawa jamaa badala ya kuja na mipango ya kutengeneza ubebe wa bei nafuu wako busy kupandisha bei ile waendelee kutegemea umeme wa diesel ambao ni ghali, kwa nini wasiwekeze kwenye solar, upepo au hata maji zaidi?

 
........Laiti kama Waislamu walioandamana Zanzbar na Dar.........wangeandamana tena safari hii sio mambo ya mkojo la hasha...... waandamane kwa ajili ya kupinga bei kubwa ya umeme na kupanda kwa bei ya vyakula..................... aah! jamani
 
Sirikali inapaswa kueleza kweli kuhusu mpango mkakati huo,ili watanzania tujue maamuzi ya kuchukua kama wateja tanesco kabla 2013.Wanajamvi tupeane ufumbuzi;maana tanesco yaweza kuwa janga kwa watanganyika !
 
Aisee, hawa jamaa kila wakijisikia kupandisha bei za umeme wanapandisha tu!!! Mbona mishahara haipandi kwa viwango hivyo vya asilimia 50??
 


Hiyo ni kazi ya kujilimbikizia mali kwa JK na makuwadi wake.

NB: read my signature below ... .... .... .... ..

 
Kupandisha gharama kwa asilimia fulani ni kujipandishia gharama serikali yenyewe ambayo ni mtumiaji namba moja wa umeme na hivyo kuaccumulate madeni ambayo baade inashindwa kulipa na kuona shirika halina faida!!!!

Katika hali ya kawaida kama wakifanya hivyo watakuwa wamewapa wapinzani pa kusemea au sera 2015.
 
Umeme hautapanda wala hakutakuwa na bei mpya January 2013, hii ni kauli ya Waziri wa Nishati na Madini alipokuwa anahojiwa na ITV- Kipindi dakika 29/10/2012.
 
Umeme hautapanda wala hakutakuwa na bei mpya January 2013, hii ni kauli ya Waziri wa Nishati na Madini alipokuwa anahojiwa na ITV- Kipindi dakika 29/10/2012.

chief, tumebakiza miezi miwili tu, tutasikia, ndio maana hii post niliiweka kwenye Jamii Intelligence

ninafahamu nilichoandika, kama waziri atenda extra mile to prove me wrong i will be more than happy, lakini kwa plan zilivo sasa, bei lazima itaongezeka, tena kwa asilimia 50 kama nilivodokeza.

MARK MY WORDS!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…