Bei ya Vanilla yaporomoka kwa kasi Mkoani Kagera, sasa kilo ni Tsh. 3,000

Bei ya Vanilla yaporomoka kwa kasi Mkoani Kagera, sasa kilo ni Tsh. 3,000

Kwan hakuna strategy's za kubalance demand na sapply ?

Kama serikali iliwapa promise ya bei na inajua wakulima wengi wako limited financial

Serikali ilitakiwa inunue hizo vanilla kutoka kWA wakulima then zihifadhiwe till bei itakapokua na tija ziuzwe .
Tunashindwa ku-balance kwenye mazao ya chakula unataka tu-balance kwenye cash crops ?. Ndio maana hapo juu niliuliza serikali ilipanga hio 15k kwa vigezo gani ? Fluctuation ya bei huwa inapanda na kushuka kiasi gani ? Je quality ni nzuri kiasi gani na Je Serikali imesha-source soko la kutosha (sababu unaposema serikali inunue kwa tshs 15k kuna uhakika itauza kwa 16k hapo mbeleni ? Na cost of storage wakati inasubiri ita-offset hio difference; sababu kumbuka hizo pesa za serikali ni kodi zetu na inapaswa tujiuliza kama ni good strategy / usage of our taxes....

Ingawa ingekuwa ni zao la chakula mfano mahindi na kuna miaka yanaozea mashambani na kuna miaka bei inapanda, serikali ingeweza kununua kila ambapo bei inashuka sana kuyatunza na bei inapopanda kidogo kuyaachia hivyo kubalance mfumuko wa bei

Kwenye hizi cash crops kinachoweza kufanyika ni either waungane wawe na bodi au ushirika ambao utatafuta masoko ya Jumla na wawe na bei realistic, huenda hio elfu tatu kwa kilo ndio bei halisi hivyo wajipange kwa hio bei (worse case scenario) waone kama inalipa na kama kila mwaka huwa inapanda mpaka 15k basi wawe na storage ikifika huko wauze kama vipi inahitaji kukaushwa vizuri ili bei ipande na ukaushaji una-justify ongezeko la bei basi wafanye hivyo...., Vinginevyo welcome to dog eat dog world...., ni mwendo wa exploitation na mkulima always has a raw deal (unless they unite)
 
Jamani, Mimi kwa uelewa wangu mdogo bei ya bidhaa husika inategemea mahitaji (demand) na Uzalishaji au usambazaji wake (Supply). Kadri aina fulani ya bidhaa inavyozidi kua nyingi ndivyo bei hiyo ya bidhaa inavyozidi kushuka na vilevile bidhaa hiyo inavyozidi kuadimika sokoni ndivyo jinsi inavyo ongezeka bei na thamani.

Inawapasa wakulima walime mazao mchanganyiko, mahindi, maharage, alizeti, mpunga, choroko, kunde, ngano, maparachichi n.k, hii itawafanya kutokosa soko la mojawapo ya mazao waliyolima.

Epukeni kulima mazao yanayotangzwa Sana na wazee wa fursa; wanalima wengi mwisho wa siku mnunuzi anazidiwa....bei inashuka Kama vanila....
 
Hakuna mtu ambaye hajui kina Azam wanachofanya bali barrier of entry ndio inayowazuia; huenda leo wewe ukapata chimbo la weze cheaper kuliko Lake Oil ila sababu hao wameshachukua locations nzuri nzuri na wateja wa muda mrefu wewe mpaka wateja wakugundue mkopo wako usha-mature na nyumba zako kuuzwa....

Anyway mkulima ni mtu wa kunyonywa ulimwenguni kote; kilichopo ni hawa wakulima ku-form cooperatives zao, kwa umoja wao watakuwa na bargaining power, bila hivyo wataendelea kupelekwa na kupelekeshwa na kila mpelekeshaji
Umenena nililia siku home tukiuza choroko kilo elfu 1 mia 7 wakati sokoni kilo ilikuwaga elfu 3 mia 5 tena wahindi wanagombania kabisa
 
Jamani, Mimi kwa uelewa wangu mdogo bei ya bidhaa husika inategemea mahitaji (demand) na Uzalishaji au usambazaji wake (Supply). Kadri aina fulani ya bidhaa inavyozidi kua nyingi ndivyo bei hiyo ya bidhaa inavyozidi kushuka na vilevile bidhaa hiyo inavyozidi kuadimika sokoni ndivyo jinsi inavyo ongezeka bei na thamani.

Inawapasa wakulima walime mazao mchanganyiko, mahindi, maharage, alizeti, mpunga, choroko, kunde, ngano, maparachichi n.k, hii itawafanya kutokosa soko la mojawapo ya mazao waliyolima.
Na unadhani kulima mchanyato huu ni rahisi ? Economy of Scale unless unalima vitu ule na ndugu zako au premium products (horticulture, viungo n.k.) unahitaji volume kubwa ili upate faida.., Na hio volume inaweza ikapatikana vipi wakati hawa so called wakulima ni peasants ?!!! (Wajiunge kwenye Ushirika ili wauze kwa pamoja; hata mwenye debe mbili apeleke huko yakawe magunia) Mtu hawezi kuchoma mafuta kufuata debe kila nyumba ndio maana kuna madalali wanaokusanya mizigo (madalali wanaongeza middlemen hence kupunguza faida kwa mkulima)
 
Poleni sana kwa hasara na maumivu mnayoyapitia, tuna safari ndefu sana kumkomboa mkulima, na hayo mabadiliko yataanzia kwa wakulima Mwenyewe kuwa na umoja.

Vanilla international wanao tuhadaa kununua kilo moja kwa 1m wapo wapi?
Wale wakisepa na pesa za watu
 
Tunashindwa ku-balance kwenye mazao ya chakula unataka tu-balance kwenye cash crops ?. Ndio maana hapo juu niliuliza serikali ilipanga hio 15k kwa vigezo gani ? Fluctuation ya bei huwa inapanda na kushuka kiasi gani ? Je quality ni nzuri kiasi gani na Je Serikali imesha-source soko la kutosha (sababu unaposema serikali inunue kwa tshs 15k kuna uhakika itauza kwa 16k hapo mbeleni ? Na cost of storage wakati inasubiri ita-offset hio difference; sababu kumbuka hizo pesa za serikali ni kodi zetu na inapaswa tujiuliza kama ni good strategy / usage of our taxes....

Ingawa ingekuwa ni zao la chakula mfano mahindi na kuna miaka yanaozea mashambani na kuna miaka bei inapanda, serikali ingeweza kununua kila ambapo bei inashuka sana kuyatunza na bei inapopanda kidogo kuyaachia hivyo kubalance mfumuko wa bei

Kwenye hizi cash crops kinachoweza kufanyika ni either waungane wawe na bodi au ushirika ambao utatafuta masoko ya Jumla na wawe na bei realistic, huenda hio elfu tatu kwa kilo ndio bei halisi hivyo wajipange kwa hio bei (worse case scenario) waone kama inalipa na kama kila mwaka huwa inapanda mpaka 15k basi wawe na storage ikifika huko wauze kama vipi inahitaji kukaushwa vizuri ili bei ipande na ukaushaji una-justify ongezeko la bei basi wafanye hivyo...., Vinginevyo welcome to dog eat dog world...., ni mwendo wa exploitation na mkulima always has a raw deal (unless they unite)
Hawa wakulima waliachaje kulima mazao yao waliokuwa wanalima kila mwaka? Ni serekali ndo iliwashawishi waache na walime vanila ambayo bei yake ni 15,000 kwa kg 1? Kama walitapeliwa na wafanyabiashara, kiongozi wa wakulima/wizara ya kilimo mkoa, wilaya, kata hawa wote msaada wao ni nn kwa wakulima, yaani kazi yao ni nn?

Akitokea mfanyabiashara akashawishi watanzania tulime miwa na bei itakuwa 100,000. Kwa kila muwa. Tuachane na nafaka! Hii wizara itakaa kimya tu!?
Sioni ni kwa vp serekali isilaumiwe na hata kudaiwa fidia.
 
Ilibaki kidogo sana niweke milioni kadhaa kwenye hili zao; uzuri ni kwamba mke wangu ni mtu wa kunusa hasara sana.
Akaniambia biashara ikishaimbwa sana ukae ukijua kuwa baada ya hapo ni maumivu tu.
 
Hawa wakulima waliachaje kulima mazao yao waliokuwa wanalima kila mwaka? Ni serekali ndo iliwashawishi waache na walime vanila ambayo bei yake ni 15,000 kwa kg 1? Kama walitapeliwa na wafanyabiashara, kiongozi wa wakulima/wizara ya kilimo mkoa, wilaya, kata hawa wote msaada wao ni nn kwa wakulima, yaani kazi yao ni nn?
Hayo mazao yao wanayolima kila Mwaka yamewasaidiaje mpaka sasa; Wanaolima, Tumbaku, Miwa, Korosho, Kahawa n.k. wamefaidika nini ? Kama Serikali through Wizara za Biashara na Kilimo wanashindwa kuwatafutia watu masoko wanafanya nini pale si waje kitaa kuliko kuendelea kulipwa mishahara
Akitokea mfanyabiashara akashawishi watanzania tulime miwa na bei itakuwa 100,000. Kwa kila muwa. Tuachane na nafaka! Hii wizara itakaa kimya tu!?
Aliyesema tuache kulima nafaka ni nani na waliokuwa wanalima nafaka kila siku wanapigwa danadana mara msiuze nje mara mtaauza mara vibali n.k. unasemaje hapo ? Issue ya Vanilla ni moja ila wakulima kutokunufaika na Wizara na Serikali kwa ujumla hilo lipo wazi
Sioni ni kwa vp serekali isilaumiwe na hata kudaiwa fidia.
Aliyesema Serikali ilipe fidia ni nani ? Mimi nalaumu Serikali kutokuweka platform nzuri na elimu kwa wakulima ili wanufaike na jasho lao - Tena hawa wa Vanilla huenda ni watu / wakulima wenye pesa wale peasants kule wanaokula mpaka mbegu ndio wengi zaidi na hii serikali ya wafanyakazi na wakulime imegeuka ya madalali na wanyanganyi
 
Waziongezee thamani tu ndio kilichobaki..atokee mwekezaji mmoja afungue kiwanda cha kutengeneza vanilla essence and extract etc..soko la ndani lipo (akina bakhresa) etc na la nchi jirani maana vanilla essence nyingi zinatoka nchi za mbali....
Maajabu ya bongo unaweza kuta sie tunailima vanilla na kuiuza

Halafu hicho tunachoimport na kutumia ni artificial flavour tu za vanilla. Vanilla yenyewe huikuti kwwnye hizo keki na biskuti zetu.

Kwanza ndo hivyo.

Kuna rafki angu aliwahi sema, usifanye biashara ya kuuza sumu. Ikidoda huwezi kula mwenyewe. Bora uuze nguo na nafaka.

Sasa vanilla ukiichakata mbongo atasema ni bei kubwa anaenda kuinunua ile feki yake unakula hasara.
 
Back
Top Bottom