Bei ya Vifurushi itamuondoa mtu next week..

Bei ya Vifurushi itamuondoa mtu next week..

Randy orton

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2019
Posts
1,338
Reaction score
3,561
Nafahamu kwamba huu mchakato wa kupandisha gharama za vifurushi ulianza tangia zamani, nafahamu pia moja ya mbinu za kisiasa ni kutengeneza tatizo na kulitatua mwenyewe hata kama ulikuwepo kwenye jopo la waliofanya maamuzi kufikia kupatikana kwa tatizo hilo.

Serikali ina kiongozi mpya ambaye pamoja na yote lazima aonyeshe amesimama upande wa watu wengi wanaolalamika kwa upandaji holela wa vifurushi ambao sio tuu utainyima serikali mapato bali utarudisha watu nyuma kutoka katika matumizi ya TEHAMA , kwa maana nyingine atajitenga na maamuzi ya kupandisha vifurushi.

Hivyo natabiri kuwa kuna vichwa vinaenda kuliwa pale TCRA na Wizara ya mawasiliano, maboss wote wanaohusika na haya maamuzi wajiandae, hii pasaka itakuwa pasaka yao ya mwisho kama maboss au viongozi wa sehemu husika..

Kama ni wajanja wachukue hatua za mapema sana kuonyesha wamesimama upande wa watu ili waokoe nafasi zao za kisiasa, kwani atakayeliwa kichwa hapa ndio atakuwa amekufa kisiasa na kiutumishi.
 
😂😂😂Magu angekuwepo ungesikia mpk saiv hao ma Director wa haya makampuni wapo central kwa mahojiano.

Jamaa alikua hataki mbwembwe oooh mara sijui mazungumzo mezani tupange tujadiliane kwanza.
Huu ubishi wa haya makampuni usingekuwepo
Yule jamaa alikua hataki utani utani

Wameambiwa warudishe vifurushi kama ilivyokua mwanzo mpk saiv bado yani,wanatunyonyaa kwanza,wanabahati sana mzee baba hayupo wangenyooka mpk saiv

Napenda sana kiongozi mwenye misimamo,sio wananchi wanalia kiongozi nae analia. Cjui tukimbilie wapi sasa
 
😂😂😂Magu angekuwepo ungesikia mpk saiv hao ma Director wa haya makampuni wapo central kwa mahojiano.
Jamaa alikua hataki mbwembwe oooh mara sijui mazungumzo mezani tupange.
Huu ubishi wa haya makampuni usingekuwepo
Wewe unadhani ni maamuzi ya hayo makampuni ndio yameamua hivyo?,Serikali yako kandamizi tena ya huyo marehemu unayemsifia sifia,lengo Lao mpunguze kuwakosoa mitandaoni,kodi ikiongezwa siku zote mtumiaji wa mwisho ndio anayeumia idiot..
 
Tusinunue vifurushi kwa hata wiki moja tu akili yao mbona itakaa sawa?
Anza wewe mzee baba
Kuanzia Sasa hivi usinunue kifurushi tena
Kwa hiyo sitegemei kuona post zako humu tena
 
Mnamuonea kindugulile bure tuu. Yeye hana mamlaka ya kupandisha wala kushusha.
 
Anza wewe mzee baba
Kuanzia Sasa hivi usinunue kifurushi tena
Kwa hiyo sitegemei kuona post zako humu tena
Kifurushi ni kama kifungua kinywa aina ya colgate aka dawa ya mswaki. Lazma daily ujiunge
 
Jumanne kuapishwa waziri mwengine, aliyepo amepwaya sana, na hili amelipwa fedha na haya makampuni, ili kukomoa wananchi hasa wana -CCM wanaoshinda mtandaoni kuitetea serikali dhidi ya mabeberu.
 
Kwa nchi kama Tanzania ambako more than 89% ya wananchi wake hawajui hata kushika mouse ya computer wala hawaelewi hata vitu vidogo vidogo kama RAM na ROM ilitakiwa bei ya 1GB iwe 250 ili kuangalia uwezekano wa kupunguza computer illiterates
 
Anza wewe mzee baba
Kuanzia Sasa hivi usinunue kifurushi tena
Kwa hiyo sitegemei kuona post zako humu tena
www.freebasic.com
Hapo utapata
1.Jamii forum
2.BBC swahili
3.BBC world news
4. Wikipedia
Na vingine vingi for free (Totally free) kupitia Halotel.
Hapo nitakuwa naunga bando kwa issue maalum tu.

Ila pole kwa wanaotegemea internet kuingiza kipato.
 
Back
Top Bottom