Masalu Jacob
JF-Expert Member
- Jul 26, 2017
- 1,446
- 1,645
Habari Tanzania !.
Hii ni chemsha bongo.
Naziomba Halmashauri zote hapa nchini wafanye maamuzi waonavyo kulingana na uwezo wao kuweka ruzuku kwenye (Petrol & Diesel) ili kuimudu mfumuko wa bidhaa hizo kwenye maeneo yao. Maana hatari kuu itawapa mtake msitake mtakapokuwa mnataka kukusanya mapato au kujiweka na jamii karibu.
Hii iwe ni utamaduni kuwa endapo tukiona maamuzi ya nchi yamefanyika kwa ujumla wake; basi sisi kama Halmashauri tujue namna bora na nzuri ya kutafsiri dhana ya Maendeleo na Uwajibikaji kwa vitendo.
Mfano, Kupaa kwa bei ya bidhaa za Petroleum hapa nchini zimeathiri sana maisha ndani ya muda mfupi. Nilitegemea halmashauri wakae na wadau wao watoa huduma za wese namna watakavyoweza kupunguza maumivu kwa jamii wanayoihudumia kila siku.
Tuwe na tabia ya kulipenda Taifa letu na watu wake.
NB
Ruzuku itapunguza sana machungu na maisha kwa jamii za wilaya fulani; sio lazima Halmashauri zote muigane bei ya pamoja hapana mnaweza kila mmoja akaja na njia nzuri zaidi lengo ni maendeleo kwa jamii.